Unapojipa jukumu la kuzuia uchaguzi Mkuu wa Kikatiba unaoipatia nchi viongozi ni sawa na kujitangazia kifo. Nchi haiwezi kubaki bila viongozi baada ya muda wao wa miaka 5 kutamatika. Hayo ni sawa na mapinduzi, uhaini baridi.
Tumeshamaliza ku describe WHO, WHERE na WHEN waliotaka kupindua, sasa hivi tuko kwenye kutafuta WHY ili tuwe ba uhakika.
Kwa mujibu wa Katiba yetu ni haramu nchi kuongozwa na viongozi ambao muda wao umekwisha, chadema walitaka hilo litokee tz ili waje na hoja nyingine mpya na yenye mashiko. Watanzania wako macho kuweni na kiasi.
Samia ni mama mstaarabu kwelikweli, ni muumini wa demokrasia ya staha. Alipovifungulia vyama vya siasa alidhani anafanya jambo jema lenye utu na utanzania, ila vyama alivyovifungulia vilimuangusha vibaya sana. Vimempatia roho ngumu, ujasiri na ukakamavu ambao hakuwa nao kabla. Anaongoza kulingana na mazingira yanavyomtaka. Watanzania tumemkabidhi nchi safi yenye amani, hivyo hawezi kuturudishia nchi iliyochomwa kila pahala. Atafanya kila kitu kuihami na kujihami. Mimi ninamuelewa sana.