Tochi za kupima mwendo(speed) zinatumika vibaya Mdaula

Tochi za kupima mwendo(speed) zinatumika vibaya Mdaula

wajinga sana hawa jamaa mi ndo maana nawasiliana na mabasi au malori kujua kama niendako kuna tochi.barabara imenyooka vizuri unakutana na kibao cha 50 km per hour....nampenda sana aliyeweka vibao vya 100 km per hour ukitokea nzega kuitafuta shinyanga
 
Wale wapo wanakusanya za kamanda hata 1000 awaachi ukiwa unasafirir we chenchi kabisa mpunga arafu ukimwona mkali ujue anataka huongeze
 
We nawe kwa kujifanya mjuaji!!!
Si ameshaeleweshwa kule juu? Uwe unapitia kwanza comments za wengine kabla hujapost we Bibi!!

IQ ndogo inaposhindana na IQ kubwa. Majanga.

Wewe utakuwa chadema.
 
IQ ndogo inaposhindana na IQ kubwa. Majanga.

Wewe utakuwa chadema.

Kwa hiyo wewe unaewaelewesha watu mara mbili mbili ndio mwenye IQ Kubwa?
Kweli CCM mnadanganyana sana!!
 
kuna kifaa jamaa yangu anacho kinafungwa mbele kwenye dashbodi kinagusa kioo kikubwa yaani kinamulika unako elekea kazi yake kubwa ni kukamata aina yoyote ya rada ....

Tumieni kifaa kinaitwa SPEED TRAP DETECTOR, unakiseti, ukikaribia kufika sehemu yenye tochi bado kama km 3 kinakupigia alarm kwamba kuna tochi (Traffic Camera), sasa ni wewe ukifika kwenye kibao cha 50 ndio utatembea kwa speed isiyozidi 50 na kinafanyakazi kwa asilimia 100 sababu ndicho nachokitumia. GPS Navigators za kisasa kina iyo detectors pia kama mtu anayo anaweza akaitumia.

Kwa wenye simu za iPhone mnaweza mkadownload iSpeedCam kwenye Apple Store, nayo inadetects baadhi ya Tochi. Sababu nilishaitumia sehemu nyingi iliweza kunitahadharisha kuna tochi na kweli nilipofika nikakuta tochi, sehemu chache haikunitahadharisha ila bahati nzuri walioshika tochi hawakuwa wamenipiga tochi, nadhani inawezekana likawa tatizo la mtandao wa simu kwenye hayo maeneo.

CC: mabesela, Uswe, genekai, gide MK, killuminat, sinafungu, Tiba
 
Unapita kasi unajiona mjanja subiri siku ule mzinga utatamani ardhi ipasuke.

Afadhari umesema.. Maana watu wanalishana sumu hapa! Eti nakwenda mbinga zaid ya km 1000, so kama zaid ya km 1000 ndo uendeshe unavyotaka? Kila siku tunalia ajali tena nyingi za hizi ajali niza kusababishwa na ujuaji wa kupindukia tuwapo barabarani
 
Sheria za barabarani lazima zifuatwe kwani tunapoteza watu na mali nyingi barabarani kwa ajali. dereva makini lazima aone vibao vyoote vya 50 km na zebra zote. pamoja na kuzingatia mstari wa kati. Kwenda mbinga sio sababu ya kutuulia wananchi wetu. kama hakuna alama ya max speed endesha utakavyo.Siku ukiona unaenda safari ya mbali anza safari jana yake. TII SHERIA BILA SHURTI

Aisee umeongea vizuri sana, nahisi ni post bora kabisa kwa mwaka huu
 
Afadhari umesema.. Maana watu wanalishana sumu hapa! Eti nakwenda mbinga zaid ya km 1000, so kama zaid ya km 1000 ndo uendeshe unavyotaka? Kila siku tunalia ajali tena nyingi za hizi ajali niza kusababishwa na ujuaji wa kupindukia tuwapo barabarani

Ni kweli ndg..Ninawaasa watu tujenge utamaduni wa kufuata sheria hii itatusaidia sana kupunguza ajali ambazo nying tunamsingizia mola kuwa ni mpango wake kitu ambacho si kweli..!! Mf. Mtu wa pikipiki havai helmet mpaka ajue kuwa mbele kuna trafiki polisi wakati ile ni kwa usalama wake mwenyewe.
 
Kawaida yangu wakitokelezea kwa kujificha huwa sisimami hata kidogo kwa sababu naweza kusababisha ajali
 
Afadhari umesema.. Maana watu wanalishana sumu hapa! Eti nakwenda mbinga zaid ya km 1000, so kama zaid ya km 1000 ndo uendeshe unavyotaka? Kila siku tunalia ajali tena nyingi za hizi ajali niza kusababishwa na ujuaji wa kupindukia tuwapo barabarani

Unajua kusoma? naongelea 57km kwa saa! rudia kutizama hilo bandiko.

kwa nini umpotezee muda mtu anayeenda 57km kwa saa kisa unataka akupe elfu 5 kwa jina la overspeed ili hali huyo mtu yuko na safari ndefu mbele?
 
Afadhari umesema.. Maana watu wanalishana sumu hapa! Eti nakwenda mbinga zaid ya km 1000, so kama zaid ya km 1000 ndo uendeshe unavyotaka? Kila siku tunalia ajali tena nyingi za hizi ajali niza kusababishwa na ujuaji wa kupindukia tuwapo barabarani

hujui unachoongea, kuna sehemu nyingi katika hiyo barabara, hasa baada ya iringa unakuta mwanzo wa katazo (eneo ambalo huruhusiwi kwenda zaidi ya 50km kwa saa) lakini hakuna mwisho wa katazo, utakuja tu kushangaa unaona katazo lingine, ikimaanisha hawajaweka kibao linapoisha katazo
 
Juzi nimeendesha kutoka Dar kwenda Mbinga, hii ni safari ndefu ya kilomita zaidi ya 1,000

Kipande cha Mlandizi hadi Morogoro kimekua na usumbufu sana, kutoka kwa baadhi ya hawa ndugu zetu.

Hivi ni kwa nini mtu anajificha kichakani na tochi? Uko na km zaidi ya 900 kufika mtu anakupiga tochi eti kwa nini unaenda 57km saa wakati kuna kibao kimeandikwa 50 max

Ina maana niwe naendesha huku macho yako katika speed meter na si barabarani? Ni kweli tofauti ya 7 ni hatari kiasi cha kustahili kulipishana?

Ninafahamu Askari wengi na waaminifu na wanafanya kazi vizuri, lakini wapo wanaoharibu kazi nzuri na sifa nzuri ya jeshi letu la polisi, hawa wachache wasifumbiwe macho, ninaomba Uongozi wa Jeshi la Polisi wwachunguze na kuwachukulia hatua stahiki wale watu walioko MDAULA, wanatumia vibaya zile tochi zilizonunuliwa kwa pesa za walipa kodi kwa faida yao.

Hata kama anajificha ndani ya shimo haikuhusu, wewe tii sheria za barabarani kama kuna kibao kinasema speed mwisho 0.0008KPH wewe tii sheria bila shuruti! Acha ubishi wa kingoni!
 
Mimi huwa nafata sheria tu, lakini wakinishika sehemu ambayo kisheria inaniruhusu kukanyaga kwakweli huwa sisimami......mfano singida kuna eneo huwa wanakaa wazee wa fedha karibu na puma lakini hakuna kibao
 
Tumieni kifaa kinaitwa SPEED TRAP DETECTOR, unakiseti, ukikaribia kufika sehemu yenye tochi bado kama km 3 kinakupigia alarm kwamba kuna tochi (Traffic Camera), sasa ni wewe ukifika kwenye kibao cha 50 ndio utatembea kwa speed isiyozidi 50 na kinafanyakazi kwa asilimia 100 sababu ndicho nachokitumia. GPS Navigators za kisasa kina iyo detectors pia kama mtu anayo anaweza akaitumia.

Kwa wenye simu za iPhone mnaweza mkadownload iSpeedCam kwenye Apple Store, nayo inadetects baadhi ya Tochi. Sababu nilishaitumia sehemu nyingi iliweza kunitahadharisha kuna tochi na kweli nilipofika nikakuta tochi, sehemu chache haikunitahadharisha ila bahati nzuri walioshika tochi hawakuwa wamenipiga tochi, nadhani inawezekana likawa tatizo la mtandao wa simu kwenye hayo maeneo.

CC: mabesela, Uswe, genekai, gide MK, killuminat, sinafungu, Tiba
Hii nzur sana
 
hujui unachoongea, kuna sehemu nyingi katika hiyo barabara, hasa baada ya iringa unakuta mwanzo wa katazo (eneo ambalo huruhusiwi kwenda zaidi ya 50km kwa saa) lakini hakuna mwisho wa katazo, utakuja tu kushangaa unaona katazo lingine, ikimaanisha hawajaweka kibao linapoisha katazo
Hili ndio tatizo kubwa mkuu. Hakuna consistency ya alama, haziko wazi. Yaani nchi yetu Mungu tu ndio anajua lakini kusema kweli ni hovyo sana. Hao wanaokaidi usikute hata gari hawajui au hawajawahi kuendesha gari safari ndefu Tanzania. Hawa watu ni wasumbufu kuliko maelezo.
 
mleta mada labda nikuulize tuu kati yako wewe na trafiki nani analeta usumbufu?? kama izo 7 ni ndogo kwanini uongeze?? usumbufu mwingine wa kujitakia tuu na tochi hizi za sasaivi hazina cha wiper wala nyororo kokote zinatusua hata usiku salama iko pale picha yako isionekane tuu
 
1. hii mada niliiweka June 2014, miaka miwili kabla wewe hujaijua JF.

2. Kama umeendesha gari, hata kama ni la kuazima, lazima utajua a difference btn 50kph na 57kph ni negligible.

3. kuna kitu kinaitwa common sense, umewahi kukisikia?
 
Tatizo lingine la matumizi mabovu ya hivi vifaa (torch) na police ni ile wanajificha na kutuma picha ya gari lako kwa askari mwingine aliye mbele na mbali sana kiasi ambacho hata wewe dereva hutakumbuka kama kweli eneo hilo lilikuwa na kibao au la.hata kama ni njia ya kutafuta income naona hii si sahihi na mara nyingi inaleta usumbufu na mabishano yasiyo na maana! Tulishawahi kurudi kwenye hilo eneo walilosema kumbe hakuna hata kibao cha speed limit hiyo
 
Km kuna kipande kina mgogoro kwenye central highway basi ni Dar- Moro. Wale jamaa ni balaa. Dawa yao ndogo tu, ukikaribia kibao ukaona uko speed, tupia neutral au mwaga maji kwenye kioo na upige wiper au weka wire au mnyororo kwa mbele na uuning'inize uguse lami njia nzima. Kila wakipiga uko 120 tochi zao zitakuwa zinasoma 0km. Labda kama wameboresha matochi yao!!!!
Juzi hapo Chalinze kurudi Dar baada tu ya kuwa namalizia ule mteremko jamaa eti wanapiga tochi kwa nyuma unaenda kusimamishwa mbelee. Just imagine sehemu unakaribia kumalizia 50km per hr just aproximately 5meters wakatag 61km per hr tulibishana sana bt kuepuka usumbufu nililipa nikasepa zangu..
In short naona siku hz lengo limebadilishwa siyo lile la awali tena..
 
Hiyo speed ya Km 900 ni ya Supersonic hilo gari lako lilikuwa angani? Acha kulalamika hujui kuendesha speed 50 basi bado utakuwa Lena.
Hajasema speed ya km900, bali kasema uko kilometa 900 kufika, yaani wastani wa umbali wa safari iliyobaki.
 
Back
Top Bottom