Tochi za kupima mwendo(speed) zinatumika vibaya Mdaula

Tochi za kupima mwendo(speed) zinatumika vibaya Mdaula

Hiyo speed ya Km 900 ni ya Supersonic hilo gari lako lilikuwa angani? Acha kulalamika hujui kuendesha speed 50 basi bado utakuwa Lena.
Hajasema speed ya km900, bali kasema uko kilometa 900 kufika, yaani wastani wa umbali wa safari iliyobaki.
 
Safiri usiku kwa usiku...tena Dar to mbinga pitia dar 2 MASASI 2 tunduru 2 songea 2 mbinga.
 
wewe una matatizo na haujui sheria za barabara, hapo walipokupiga tochi ni lazima kulikuwa na Kibao ambacho kinaonyesha 50km/saa yaani usiendeshe zaidi ya hapo na ni lazima kulikuwa na kijiji au shule au Wanyama kwa kawaida kuna kuzidisha kunakokubaliwa nako ni mpaka 55 km/saa kuanzia 56 k/saa hakukubaliwi...

Hivyo acha kulalama angalia na zingatia alama za barabarani...

Hawa jamaa ni bure kabisa. Level ya uadilifu wao inatia mashaka.
 
Mkuu ni vizuri tukaheshimu sheria na alama za barabarani. Lakini hawa jamaa wa tochi wakati mwingine ni wazushi tu. Siku moja nikiendesha Segera - Chalinze, nilikiona kibao cha speed limit nikapunguza mwendo mpaka speed iliyotakiwa. Nilipofika jamaa alipojificha akajitokeza na kunisimamisha. Akanionyesha tochi yake ikisoma km 90 kwa saa wakati mimi nilikuwa naendesha km 50 kwa saa. Nikamwambia hiyo tochi yake imekosea mimi nilikuwa naendesha kwa speed inayotakiwa. Tulibishana kwa karibu dakika 10 halafu akaanza kuniuliza fire extinguisher, triangle, na box la first aid. Nikamwonyesha kila kitu isipokuwa sikuwa na box la first aid. Hapo napo ikawa shida, nikamwambia box la first aid sina kwa kuwa hiyo sio gari ya abiria ni gari yangu binafsi.

Point yangu hapa ni kwamba hawa jamaa wanaweza kukubambikia speed ambayo sio ulikuwa unaendesha wewe usipokuwa makini.

Tiba
Box la First Aid? Hii sheria imeanza lini?
 
Km kuna kipande kina mgogoro kwenye central highway basi ni Dar- Moro. Wale jamaa ni balaa. Dawa yao ndogo tu, ukikaribia kibao ukaona uko speed, tupia neutral au mwaga maji kwenye kioo na upige wiper au weka wire au mnyororo kwa mbele na uuning'inize uguse lami njia nzima. Kila wakipiga uko 120 tochi zao zitakuwa zinasoma 0km. Labda kama wameboresha matochi yao!!!!
Hakuna kitu rahsi hapa duniani kama kumdanganya mtanzania.
Rahsi sana asikwambie mtu.
 
1. hii mada niliiweka June 2014, miaka miwili kabla wewe hujaijua JF.

2. Kama umeendesha gari, hata kama ni la kuazima, lazima utajua a difference btn 50kph na 57kph ni negligible.

3. kuna kitu kinaitwa common sense, umewahi kukisikia?
Kwaiyo ndo ukaanza pekua pekua ujue nilijoin lini jf hahahah kwani watu hamuwezi toa point mpka mzamie profile za watu kwanza??[emoji23][emoji23][emoji23] anyway kama ni 2014 na kulikuwa na tochi za aina nyingine sio izi ila malalamiko yako yako pale pale alafu Nikuambie kitu izo tochi usiziogope we ukitaka kujua kazi yake nenda kwa DTO au RTO alie karibu nawemueleze shida yako kuna uwezekano wa kupewa iyo tochi ujihakikishie binafsi nimeshawahi fanya ivyo ndio maana nakumegea ndugu tangu nawe ufaidike sio kulalama coz hakukusaidii na tochi utapigwa na kulipa utalipa sometime utomaso ni mzuri.
 
Juzi nimeendesha kutoka Dar kwenda Mbinga, hii ni safari ndefu ya kilomita zaidi ya 1,000

Kipande cha Mlandizi hadi Morogoro kimekua na usumbufu sana, kutoka kwa baadhi ya hawa ndugu zetu.

Hivi ni kwa nini mtu anajificha kichakani na tochi? Uko na km zaidi ya 900 kufika mtu anakupiga tochi eti kwa nini unaenda 57km saa wakati kuna kibao kimeandikwa 50 max

Ina maana niwe naendesha huku macho yako katika speed meter na si barabarani? Ni kweli tofauti ya 7 ni hatari kiasi cha kustahili kulipishana?

Ninafahamu Askari wengi na waaminifu na wanafanya kazi vizuri, lakini wapo wanaoharibu kazi nzuri na sifa nzuri ya jeshi letu la polisi, hawa wachache wasifumbiwe macho, ninaomba Uongozi wa Jeshi la Polisi wwachunguze na kuwachukulia hatua stahiki wale watu walioko MDAULA, wanatumia vibaya zile tochi zilizonunuliwa kwa pesa za walipa kodi kwa faida yao.
Mkuu 50 inapaswa kuwa 50 au chini ya hapo lakini ukizidisha hata moja umekihuka sheria za kuzingatia alama za bara barabarani.

Kuhusu kujificha wameagizwa hivyo hata Mpinga aliwahi kusema kwenye vyombo vya habari kwamba hiyo ni mbinu wameibuni ili kukamata makosa mengi.
 
Km kuna kipande kina mgogoro kwenye central highway basi ni Dar- Moro. Wale jamaa ni balaa. Dawa yao ndogo tu, ukikaribia kibao ukaona uko speed, tupia neutral au mwaga maji kwenye kioo na upige wiper au weka wire au mnyororo kwa mbele na uuning'inize uguse lami njia nzima. Kila wakipiga uko 120 tochi zao zitakuwa zinasoma 0km. Labda kama wameboresha matochi yao!!!!
Wameboresha siku hizi zinasoma. Zamani ukitembea umewasha taa zilikuwa haziwezi kusoma lakini siku hizi sio aise!
 
Aaaaah hao jamaa ni noma halafu siku hizi wanatumia magari binafsi na tochi pia wananunua zao binafsi za kukusanyia hela

Maisha magumu jombaa wanachangamkia fursa.. kama huwezi kutii sheria tembea na buku mbili mbili za kutosha.. nchi yenyewe ishauzwa hii
Siku hizi minimum ni ki ten mkuu huna unacopiwa kwenye efd yao ili upunguziwe maksi kwenye leseni!
 
Hv mnasimamaga???kwakweli huwa wanasoma tu namba spidi 150 nasimamaje????
Wanawapigia simu walio mbele ya unakokwenda unakuta wameku block na gari zao kabisa, hukatizi mkuu!
 
Halafu ukiona wanavyotoka speed kuzuia gari kama limekwenda zaidi ya mwendo unashangaa kabisa...kitu kingine nisichoelewa ni hizo speed limit kuwa na mkanganyiko...kuna sehemu haziko clear especially between kibaha na mlandizi.
Ni hao hao wanang'oa hizo alama maksudi ukipita kibao hakuna lakini mbele wanakwambia ume over speed!
 
wewe una matatizo na haujui sheria za barabara, hapo walipokupiga tochi ni lazima kulikuwa na Kibao ambacho kinaonyesha 50km/saa yaani usiendeshe zaidi ya hapo na ni lazima kulikuwa na kijiji au shule au Wanyama kwa kawaida kuna kuzidisha kunakokubaliwa nako ni mpaka 55 km/saa kuanzia 56 k/saa hakukubaliwi...

Hivyo acha kulalama angalia na zingatia alama za barabarani...

Hata ukiwa 51 unapigwa bao mkuu wewe kama umefikisha 55 ukapita hapo atakuwa alikuwepo mjomba wako lazima!
 
Nimeilewa sana post yako, ila sisemi mengi. Nakuomba tufanye uje na gari yako uelekeo wangu wakati mvua inanyesha au ufanye hivyo unavyojua wewe afu mimi nikupimie ushuhudie mwenyewe. Ni PM kama uko siriaz.
Namimi namhakikishia kwamba usemayo ni kweli kwani hata mimi ulikula ki ten changu sijakusahau mkuu!
 
Mm nilipigwa faini kwa 51kph. Nilijitetea hakuna aliye kubali utetezi wangu na ndani ya gari nilikuwa na mgonjwa. Hawa askari nafikiri matatizo hayaji kuwapata maana wao ni Mungu.
Hiki hata mimi huwa nawaonya sana kwamba si kila kosa lazima adhabu wp mmoja niliwahi kumuuliza kama ndivyo anavyolea watoto wake nyumbani wanajifunza nini ikiwa kila kosa ni viboko? Alicheka na kunijibu kuwa eti hapa ni barabarani sio nyumbani kwake!
 
Kuna siku traffic walinionea sana na sitasahau.nilikuwa natoka Dar kuelekea Ars. Kufika michungwani karibia na Segera wakanisimamisha eti nimefika speed 95..hivi kweli utakuwa mwehu kuendesha gari kwa speed yote hiyo wakati Michungwani ni lile gate pale Segera ni umbali mdooogo.. Mi nadhani wakati mwingine huwa wanategesha ili watoze faini. Hivi ntajuaje kama hiyo spees inayosoma katika kamera ni ya gari iliyopita!!! Au ntajuaje kuwa wameitega wenyewe. Wanatia hasira sana hawa jamaa
Kamera inapiga picha gari lako pia.
 
Nimependa dedication ya trafiki kazini - kabla ya saa kumi na mbili alfajiri wapo kazini wanakagua. Jua linatua kuelekea saa moja usiku wapo njiani wanakagua.
 
kuna kifaa jamaa yangu anacho kinafungwa mbele kwenye dashbodi kinagusa kioo kikubwa yaani kinamulika unako elekea kazi yake kubwa ni kukamata aina yoyote ya rada hata kama ni ya jeshi . wakati unaendesha tochi ikiwa mbele yako umbali wa km 1 hadi 2 kuna haramu inalia hivyo unapunguza mwendo
Haramu inalia=????????.
 
Back
Top Bottom