Juzi nimeendesha kutoka Dar kwenda Mbinga, hii ni safari ndefu ya kilomita zaidi ya 1,000
Kipande cha Mlandizi hadi Morogoro kimekua na usumbufu sana, kutoka kwa baadhi ya hawa ndugu zetu.
Hivi ni kwa nini mtu anajificha kichakani na tochi? Uko na km zaidi ya 900 kufika mtu anakupiga tochi eti kwa nini unaenda 57km saa wakati kuna kibao kimeandikwa 50 max
Ina maana niwe naendesha huku macho yako katika speed meter na si barabarani? Ni kweli tofauti ya 7 ni hatari kiasi cha kustahili kulipishana?
Ninafahamu Askari wengi na waaminifu na wanafanya kazi vizuri, lakini wapo wanaoharibu kazi nzuri na sifa nzuri ya jeshi letu la polisi, hawa wachache wasifumbiwe macho, ninaomba Uongozi wa Jeshi la Polisi wwachunguze na kuwachukulia hatua stahiki wale watu walioko MDAULA, wanatumia vibaya zile tochi zilizonunuliwa kwa pesa za walipa kodi kwa faida yao.