2012 nilikuwa naishi Mbagala naungaunga maisha feri
Huko nnapoishi sikuwa na chochote ni kwa mshkaji nilikuwa nachangia kodi na sometimes nakosa
Siku moja sikuwa na kitu niliishia kula mihogo ya mia tatu asubuhi na sikupata kula chochote tena mpaka usiku niliamua kurudi Mbagala
Lakini mfukoni nilikuwa na jero tu ilibidi kwenda Mbagala na kesho lazima nirudi feri
Nilitega dcm limejaa nikadandia nyuma ndiyo nikaenda Mbagala ili ile jero inifae kesho kurudi feri nauli ilikuwa ni mia tatu kipindi hicho
Nimefika home mshkaji yupo na shemeji mpya
Nikaishiwa pozi inatakiwa nitafute pa kulala huwa narudigi feri kulala kwenye miboti
Nikaskuti kama nusu saa hivi pale ikabidi niage nikaondoka nikapanda gari tena kurudi feri usiku huo
Nilipofika feri huwa sehemu nzuri ya kulala ni upande wa kigamboni nikawa naenda kwenye kivuko kuna namna ya kuingia pale bila kulipa lakini siku hizi sijajua pakoje
Magari yako foleni kusubiri kivuko kije natembea pembeni ya foleni nikaona hela imekunjwa kunjwa elfu 10
kama mita mbili tu mbele kuna mama alikuwa amesimama anaongea na jamaa aliyeko ndani ya gari
Nilivyookota hela aliona kuna kitu nimeokota lakini hakujua ni nini nilivyofika mbele ilikuwa ni elfu 25 nilimshukuru Mungu kwa kila namna siku hiyo na nlibaki na maswali sana kwa kilichotokea
Sent from my TECNO KC8 using
JamiiForums mobile app