Toa ushuhuda wowote ambao unadhani bila Mungu usingetoboa

Toa ushuhuda wowote ambao unadhani bila Mungu usingetoboa

Mungu hakuna alilowahi kunisaidia, kikubwa anakula pesa zangu kila siku,

Mimi ndo namsaidia maana nampa pesa.

Nilikuwa na shida akanitupa halafu saivi eti nimtolee, kweli?

Kila nilichonacho nimekipata kwa jasho langu.

Kwanza hayupo na kama yupo hana nguvu yoyote, kiufupi mimi namzidi uwezo.
Tubu uongeayo.Mungu kasema ni mwenye uwivu.
 
Aahaaaaaaah!?

Mkuu kumbe ndiyo Mungu wako alivyo

Ila kama hautajali


Mungu yupi huyo!?
...Umeishajibiwa mara nyingi....'Unayemjua Wewe !' lakini Husikii TU!

Ina maana wewe ni Kibuyu Wazi mno huna Mungu unayemfahamu ????...
 
Mimi nilipata shida kazini...
Nikasimamishwa kazi...

Kumbe boss wangu kanitengenezea kesi ya wizi... Ameshaenda kuripoti polisi... Kamwaga hela huko mi sina taarifa...
Akamtafuta afisa flani wa polisi kwamba nikiripoti kituoni yeye awe ndiye mwenye faili.. Kiufupi huyo awe mpelelezi wa kesi...

Niko nyumbani napigiwa simu njoo ofisini... Kufika polisi hawa hapa.. Nikaenda central... Kufika yule polisi aliyekuwa amepangwa akanidaka..
Nikachukuliwa maelezo kinguvu nguvu... Nafikiri mnajua polisi kukoje...

Sasa imefika jioni kuna mama mmoja mtu mzima akawa anakagua mahabusu... Akanikuta nimepiga magoti nasali..
Nafikiri mama huyo alishangaa kidogo.. Nikasikia officer flan flan mlete huyu ofisini kwangu.. Naomba file lake nilipitie....

Hapo ndipo nilipo pona... Nilimweleza kila kitu na kumwambia makosa ninayotuhumiwa sijawahi kufanya...

Akabadili mpelelezi.. Akafanya upelelezi nikiwa nimepewa dhamana nikakutwa sina hatia...

Baadae bosi alishushwa cheo...

Ila niliponea kubambikwa kesi... Mungu mkubwa
Mungu aendelee kukupigania

Zab 27:3 SUV​

Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini.
 
Kwa kweli ukimtegemea Mungu 100% nakuhakikishia utatoboa,Mimi nilikuwa na biashara ilikuwa inachechemea sana kwa muda ,Ila nilipoamua kuikabidhi kwa Mungu nimeona mabadiliko makubwa sana.
Kikubwa uwe mwaminifu, utoe sadaka pamoja na kikumi ,usali na uwe unasoma neno la Mungu na kuomba ( kufunga), nakuhakikishia utatoboa.Sasa hivi mauzo yameongezeka zaidi ya marambili ya Yale ya zamani.
Glory to God.
🤝🏻🤝🏻🤝🏻
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom