Toa ushuhuda wowote ambao unadhani bila Mungu usingetoboa

Toa ushuhuda wowote ambao unadhani bila Mungu usingetoboa

Pale nilipogombana na mkewangu mkewangu akaenda nishitaki mahakamani kwa kosa la kumpiga mke siku ya kwenda mahakaman nikabeba shiling laki mbili kwaajili ya kuwatuliza wasikiliza kesi fika mbele namuona alieshikilia kesi ya wife nikamuita chemba nikamwambia, kiongozi fanya uwezalo nichomoke kwenye hiyi kesi, basi nikazama mfukoni, ile kutoa patupu kumbe hela nimeangusha home wife kachukua kaenda kuhonga kwa wakili asee ile kesi bila mkono wa mungu nisingetoboa, maana nilikaa ndani miez sita, ila wakuu mungu mwenyewe yupo kweli?
Bado upo na hilo limwanamke?
 
Corona ya kwanza ile Kaliiii, daktari anamuogopa mgonjwa, ambulance iko silence , akipatikana mgonjwa tu. Uelekeo Mlonganzila.

Bila mkono wa MUNGU nisingetoboa ILINIPIGA hosp ya kwanza wamepima kila kitu HAKUNA ugonjwa , naulizwa je? Unajisikia kukereketa Kooni , nawajibu HAPANA kumbe hali hiyo NAISIKIA .Anapewa dawa narudi nyumbani hali ile ile.

Hosp nyingine hivyohivyo. Hali yangu vikawa tete!! Hakika NILIMUOMBA MUNGU, maombi ambayo NINA UHAKIKA MWENYEZI MUNGU MUWEZA WA YOTE, aliyasikia na WEMA NA FADHILI ZAKE ZIKANIFUATA.
 
My whole life aisee maisha yangu yana bahati sana asee kuna mambo hata sistahili lakini naona yananitokea tu tena mema sana

Huwaga naishi na huu msemo “tell me there is no God and i will tell you my story”

Acheni Mungu aitwe Mungu 🤲🏾

Ayubu 19:26-27 SRUV​

Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu; Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu!
 
Oya eeh sio pw..
2018 nilikua natumiki kifungo changu katika gereza la ISIS mbarali,tulikua tunafyatua tofali(zile zenye foroma mbili) yaan kwa wakati mmoja unabeba tofali mbili halafu mchakamchaka na nyuma yako kuna kiherehere anakutandika viboko...
kiukweli ile hali ya kupigwa niliichoka(nkakumbuka nimekaa jkt miez 3) nikawaza hapa nisipotumia ukakamavu wangu nitapigwa mpaka mgongo utaoza...

wakat kiherehere ananipiga nikammwagia yale matope usoni halafu nikamkumba mpaka chini tukaanza kugaragazana,wenzie wakaja...

ile wanaanza kunipiga akaja nyapara akaita jina langu,nikaitika chap "NIPO BWANA MKUBWA" akasema unaitwa ubaoni...dah kumbe bro alikua amefanya mpango wa kunitoa...NILIUONA UTUKUFU WA MUNGU SIKU ILE..

Zaburi 124:1 SRUV​

Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa
 
Pale nilipogombana na mkewangu mkewangu akaenda nishitaki mahakamani kwa kosa la kumpiga mke siku ya kwenda mahakaman nikabeba shiling laki mbili kwaajili ya kuwatuliza wasikiliza kesi fika mbele namuona alieshikilia kesi ya wife nikamuita chemba nikamwambia, kiongozi fanya uwezalo nichomoke kwenye hiyi kesi, basi nikazama mfukoni, ile kutoa patupu kumbe hela nimeangusha home wife kachukua kaenda kuhonga kwa wakili asee ile kesi bila mkono wa mungu nisingetoboa, maana nilikaa ndani miez sita, ila wakuu mungu mwenyewe yupo kweli?
Mbona umeweka alama ya kuuliza tena ni swali au???
 
2012 nilikuwa naishi Mbagala naungaunga maisha feri
Huko nnapoishi sikuwa na chochote ni kwa mshkaji nilikuwa nachangia kodi na sometimes nakosa
Siku moja sikuwa na kitu niliishia kula mihogo ya mia tatu asubuhi na sikupata kula chochote tena mpaka usiku niliamua kurudi Mbagala
Lakini mfukoni nilikuwa na jero tu ilibidi kwenda Mbagala na kesho lazima nirudi feri

Nilitega dcm limejaa nikadandia nyuma ndiyo nikaenda Mbagala ili ile jero inifae kesho kurudi feri nauli ilikuwa ni mia tatu kipindi hicho
Nimefika home mshkaji yupo na shemeji mpya
Nikaishiwa pozi inatakiwa nitafute pa kulala huwa narudigi feri kulala kwenye miboti

Nikaskuti kama nusu saa hivi pale ikabidi niage nikaondoka nikapanda gari tena kurudi feri usiku huo
Nilipofika feri huwa sehemu nzuri ya kulala ni upande wa kigamboni nikawa naenda kwenye kivuko kuna namna ya kuingia pale bila kulipa lakini siku hizi sijajua pakoje

Magari yako foleni kusubiri kivuko kije natembea pembeni ya foleni nikaona hela imekunjwa kunjwa elfu 10
kama mita mbili tu mbele kuna mama alikuwa amesimama anaongea na jamaa aliyeko ndani ya gari
Nilivyookota hela aliona kuna kitu nimeokota lakini hakujua ni nini nilivyofika mbele ilikuwa ni elfu 25 nilimshukuru Mungu kwa kila namna siku hiyo na nlibaki na maswali sana kwa kilichotokea

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Dah ALLAH He the GREATEST 🙌🙌👏
 
My whole life aisee maisha yangu yana bahati sana asee kuna mambo hata sistahili lakini naona yananitokea tu tena mema sana

Huwaga naishi na huu msemo “tell me there is no God and i will tell you my story”

Acheni Mungu aitwe Mungu 🤲🏾
Askofu GWAJIMA Huwa ni mtu wa tofaut sana.....

Ingia YouTube Kuna somo alifundisha jumapil ya hii wiki pata muda sikiliza......

KUSUDI LA KUCHAGUA LITASIMAMA

mwenyez MUNGU haangalii matendo yako mazuri au mabaya....yeye hum bariki amtakaye...
Mwenyez MUNGU hum hurumia amtakaye Kwa sabab amemchagua.....
Kuna watu Mungu amewabarik na hawajawai kupiga goti hata hawaja mwomba chochote.....

Watoto Esau na yakobo walishindana tumboni.....
Na MUNGU alimpenda Yakobo........
Kabla hata hawajazaliwa....Mungu alimchagua Yakobo tangu tumboni hajazaliwa... kusema Mungu alimchukia Esau...ina maana Mungu ana upendeleo...Hasha......
Sio Kwa mazuri au mabaya Mwenyezi MUNGU humchagua amtakae Ili kusudi la MUNGU litimie...

Unaweza kusoma mpk PhD na usiweze kumilik hata bajaji.... Mwingine hakusoma Wala nini akawa na maisha Bora kabisa kuliko wewe...
Una weza kua na akili nyingi za darasani lakini sio Kwa kutenda mazuri au mabaya Mwenyezi Mungu humchagua amtakaye...

KUSUDI LA MUNGU KUCHAGUA LITASIMAMA
 
Bado nakumbuka sana mwezi ule niliota ndoto fulani kuwa napiga story kuhusu Ukimwi (HIV) , basi nilipoamka week lote hata nikijisahaulisha basi ile ndoto na mada za Ukimwi zinakuja...

Hata mtandaoni yani nikigusa tu Twitter, na huku jf basi nakutana na mada za HIV tu..

Mwezi mmoja badae, siku moja usiku niliumwa sana usiku, pumzi ilikuwa kama inanata hivi asubuhi yake nilikuwa kitandani hospital nilizima usiku uleule

Nilishtuka nikakuta drip lipo mkononi, na doctor Mzee mmoja wa makamo yupo na ndugu zangu 5..

Nikapigwa vipimo vingi majibu yakaja nina TB nikazimia hahaha.. nilivyoshtuka doctor akanipiga elimu na kuniuliza kama nimewahi pima HIV, nikamwambia hapana,

Honestly I was so loyal kiasi kwamba nilikuwa na mpenzi mmoja tu

Basi akanipa counseling ya kuniandaa kisaikolojia juu ya majibu maana aliona nimeanza panick.

Nikapimwa pale majibu yakawa negative yani imagine familia nzima wazazi, sisters na brothers 2 wote walilia

Hapo kilo zimekata na nikatakiwa kuundergo matibabu miez 6...

Fast foward niliomba Mungu anifunulie nilipata wapi hiyo TB..ndipo Mungu akajifunua mbele zangu kuna siku nilimface tu bae wangu kuwa sina amani nae, tukapime..

She was shocked vibaya mno na nikakazia tunapima ukimwi.... Akagoma na akasema namchukulia cheap sababu ananipenda na anajitoa kwangu...

Nikamshit, sababu sikuwa na uhakika lakini mwezi mzima hatutafutani, mwisho wasiku akanitafuta kuna ktu anataka kuniambia..

Sikuhiyo ndo akafunguka kuwa amezaliwa na HIV na alitamani sana kuniambia lakini alishindwa..

Hapo imagine nimelala nae zaidi ya two years tena mara 20+ kavu....the whole year nilipima nikawa salama

Mungu mwema sana, maana nisingejua hali yake ningeendelea and you never know..

Kitu kingine chaajabu kwayule girl alikuwa mkavu nikawa natumia sana mafuta kumlainisha na hapo sijawahi tumiaga kabla..

I look back na kumuogopa sana Mungu pia naogopa sana kuomba Mungu anifunulie mambo mengine maana anatuepusha na mengi bila ya sisi kuona
Hallelujah, Glory to God
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom