Timu ya Taifa inakosaje kuwa na basi lake?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Wakuu,

Nimekutana na video ikionesha Timu ya Taifa inainga uwanjani kwaajili ya mchezo wake na Morocco, wakitumia basi ya Super Feo. Namnukuu Msigwa kama alivyoandika kwenye ukurasa wake Instagram; " Taifa Stars imeingia kibabe sana leo Uwanja wa Benjamin Mkapa. Kitu cha Marcopolo, sio mchezo!"

Kiongozi unapata wapi nguvu ya kujjivuna kabisa kwa timu ya taifa kuingia na basi la kukodi, tena hakuna bendera ya taifa, hakuna chochote gari lipo uchi utafikiri ni katimu kanakojitafuta!

Wameweza kununua magoli ya timu lakini wakashindwa kununua basi kwa timu ya taifa kweli? Pamoja na kodi zote kwa wananchi mmeshindwa kununua basi la timu ya taifa mpaka mnajigamba na basi la kodi, hii ni aibu kubwa.

Tunaweza hadi kulipa kulipa watu wabebe mabango ya kusifia ila sio kupush kwa mambo ya kuboresha timu hizi?

msigwa.jpg


 
Back
Top Bottom