Kila la heri Timu ya Taifa Karume Boys

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi anaitakia Karume Boys kila la heri timu ya taifa ya kandanda ya Vijana ya Zanzibar chini ya Umri wa miaka 15 katika mchezo wa fainali ya Michuano ya CECAFA (U-15) alhamisi tarehe: 16 Novemba dhidi ya vinara wa Uganda.

Rais Dk. Mwinyi amesema Karume Boys ina uwezo mkubwa wa kurejea na Kombe kutokana na kiwango walichoonesha katika kundi lao walipoibuka washindi.

"Mcheze kwa nidhamu mkielewa Wazanzibari wote wapo pamoja nanyi wakiwaombea dua" amemalizia Rais Dk. Mwinyi.
IMG-20231115-WA0019.jpg
 
Back
Top Bottom