Tido Mhando na Kinana ndani ya TBC1, wasema elimu bure haiwezekani

Jokakuu can you please tell us, when education become free who gona pay for it?
uingereza na ubepari wao elimu ya msingi mpaka sekondari/upili ni bure na kwa msingi watoto wanapewa chakula, elimu ya kulipia ni university na mkopo unatolewa kwa ajili hiyo ukifikisha maksi zinazo takiwa, sasa bado hujenda sweden/norway/denmark/canada nk
 
Kasheshe,
I can tell you. Ukipunguza baraza la mawaziri kutoka arobaini hadi 20. Ukipinguza mishahara ya wabunge na marupurupu yao. Ukipunguza 30% za bajeti inayotumika kwa chai na vikao vya warsha, inawezekana. Yes we can, alisema Obama, and it can be done, alisema Nyerere. Priority, my friend, priority! Na hapo hujaweka 30% ambayo Kikwete alikiri inaishia mifukoni mwa mafisadi kutokana na corruption.


...Na hapo hujapitia upya mikataba ya kipuuzi inayowafanya wawekezaji wachukue aslimia 97 sisi tubakiwe na 3 na katika hizo tatu aslimia 1.7 iende Rombo kupitia kwa akina Stewarts na mwishowe sisi kubaki na asilimia 1.3 inayoshia mifukoni mwa mafisadi ambayo ndio kila siku yanasimama majukwaani kuzomoka kuwa elimu ya bure haiwezekani!!
 
Sasa wao kama wanabisha si wampe Slaa kipindi japo cha robo saa wamuulize elimu bure itawezekana au la, then ndio waconclude.


...Hawathubutu kwa sababu ndani kabisa ya mioyo yao miovu wanajua kuwa INAWEZAKANA!! Everybody has just to play his/her part and the wananchi starts playing theirs on October 31!
 
Elimu bure inawezekana na ni kwa wapumbafu wa aina ya kina Kinana na wenzake ndo elimu bure haiwezekani. CHAGUA DR SLAA MABADILIKO
 
Hivi shilingi bilioni 250 zinaweza kujenga nyumba ngapi za walimu?

Nyumba za walimu kwa kule kwetu vijijini nzuri kabisa the best house unajenga kwa 20,000,000/= Ths. 100mil utajenga nyumba 5, 1 Billion utajenga 50 houses, 250 billioni utajenga 50 x 250 = 12,500 . hizi ni nyumba nyingi sana na zenye hadhi ya maana kwa walimu wetu wa shule za kata karibu zote Tanzania.
 
Na mimi nakuuliza swali, kwanini UFISADI UNAWEZEKANA bali Elimu na afya bure visiwezekane?

Kwa nini wenye dhamana ya uongozi wa nchi hii wanakumbatia, wanaulinda na kuudhamini ufisadi, bali elimu na afya bure wanauona kama ukoma vile?

MICHAWI YA MCHANA kama hiyo kina Kinana na miovu mingine inayofaidi mfumo mchafu usio na dira ya kitaifa ndiyo inayoshabikia wazimu wa CCM.

Sasa nakwambia, CCM na makuwadi wao NDIO KIKWAZO cha maendeleo ya TANZANIA kwa miaka yote hii 50 tangu ukoloni wa mwingereza.

KIAMA CHENU KIMEFIKA NA HAMTAPONYOKA. TANZANIA MPYA INAKUJA KWA KISHINDO!
 
Jokakuu can you please tell us, when education become free who gona pay for it?

Kasheshe that is a good question. Unajua kama mtu una mashaka na kinachosemwa ni afadhari uulize. Tatizo ni kuwa wengine wanafuata mkumbo wa kisiasa tu hawataki kuwa majasiri na kusema, how can it be done?

Although am not jokakuu who you directed this question to, i will try to give my opinion on this. Watu wanaosema hili haliwezekani wanasahau kuwa tayari Tanzania ilikuwa na utaratibu kama huo, na ulifanyika vizuri na kiwango cha elimu kilikuwa bora kuliko sasa. Kwa hiyo utaratibu huo unaweza kurudi na mambo yakawa mazuri.

Kwanza tujiulize elimu bure maana yake ni nini? Kama maana yake ni mwanafunzi kutolipa ada, FOR SURE hilo linawezekana. Kama tafsiri ya huduma bure za afya maana yake ni kuwa na hospitali inefficient kama muhimbili, for sure inawezekana kabisa.

Ukiuangalia moja ya malengo ya kuleta uchangiaji wa elimu ilikuwa ni kuboresha elimu, lakini ukiangalia matokeo ni kwamba utaratibu huo umedunisha elimu. Tumeleta mambo mengi ambayo yamefanya elimu isiwe na thamani, unaweza kushangaa watoto wa vigogo vilaza tu wanakuwa wafanyakazi BOT, watu vihiyo wanakuwa mawaziri, mpaka sasa rais wetu amepewa Phd hewa kitu ambacho naona ni dhihaka kwetu, unaona wazi kabisa kuwa elimu sio msingi tena. Kama serikali ikiona finacial value ya elimu kwa kuulipia inawezekana hata umuhimu wake ukaongezeka.

Ukiangalia quality ya huduma za Afya, hospitali chafu zinanuka, kina mama wanaojifungua wanajipanga mawodini, ukienda hospitali wanakwambia wazi kabisa nenda kanunue dawa kwa mtu fulani, au daktari anakwambia njoo kesho kwenye hospitali yangu, hakika unaweza kuona kuwa serikali ikiwa serious inaweza kulipia. Hata elimu ya msingi na ya sekondari, ikiwezekana hata chuo kikuu ukiangalia unaweza kuchoka. Nenda mlimani ukaone palivyo ovyo, vyoo canteen na madarasa yako worse kuliko ilivyokuwa miaka ya 70 na 80, uwezo wa maprof ndio usime kabisa wengine ujaiuliza kama kweli wao ni maprof au nao ni vihiyo. Na watoto wanaokwenda shule za msingi wengi hawana vitabu darasa zima linatumia kitabu kimoja, madarasa mabaya na machafu, kuna wakati darasa lina wanafunzi 50 au hata 60, watoto wengine wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika. Uwezo wa walimu wa sasa wa kufundisha na kuwa-mould watoto uko chini sana ikilinganishwa na uwezo wa walimu seniors. Kama walimu wa siku hizi ni wa namna hiyo serikali inaweza kusupply walimu wengi zaidi kwa shule nyingi zaidi.

Even better, kama serikali ikiwa more serious na more scientific kwenye kukusanya kodi, kufuta unnecessary spending, na kuongeza vyanzo vya mapato uwezo wa kulipia gharama za elimu upo kabisa, hakuna shaka hata kidogo, we (the government) can pay for it.

Ukisikia mtu anasema haiwezekani basi anasema kutokana na umbumbumbu au kutokujua, Kama anajua basi anasema kwa sababu za kisiasa, and not being realistic. Kama mahali pa kuanzia ni hali ya sasa, for sure elimu bure na afya bure vinawezekana.
 
kwa vile wao hawawezi, wakae pembeni mwanaume anayeweza (Dr. - PhD Slaa) aingie madarakani. kama hawawezi, kwani wanalazimishwa? Watz wanataka
Tz hatudanganyiki.JPG
Pia Watz ambao ni maskini wanahitaji
Dr. Slaa anasema inawezekana
Jk anasema haiwezekani.

Basi mchagueni anayeweza. Dr. Slaa
 
Ingekuwa raha wangemuita na muwakilishi wa CHADEMA aziponde hizo data, midahalo wanaikimbia wanataka kuzungumza bila kupingwa na mpinzani na hii ni dalili ya kutokuwa na hoja za nguvu.
 
uingereza na ubepari wao elimu ya msingi mpaka sekondari/upili ni bure na kwa msingi watoto wanapewa chakula, elimu ya kulipia ni university na mkopo unatolewa kwa ajili hiyo ukifikisha maksi zinazo takiwa, sasa bado hujenda sweden/norway/denmark/canada nk

Botswana, mpaka University
 
Back
Top Bottom