Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 2,209
- 4,769
Kwanza ifahamike kuwa, shule bure imeongeza ujinga mkubwa miongoni mwa wanafunzi tangu tu huduma hii ilipoanzishwa na serikali
Lengo na maksudi ya Serikali na nia yake, ilikuwa ni njema na nzuri mno, ni kuwasaidia watu wote bila kujali umasikini wao, wasome na wawe na elimu kwa kila mtu
Hata hivyo, mimi naona ni kama Serikali imechelewa sana kuyapitia maazimio haya tangu kuanzishwa kwa elimu bure
Kinachoshangaza ni kwamba, kuna watoto eti wanafaulu ili hali hawajui kusoma wala kuandika majina yao, hii ni tofauti kabisa na ilivyokuwa elimu ya kulipia, wazazi walikuwa serious kufuatilia watoto wao ili kuepuka kutupa pesa zao kugharamikia kisichoelewa
Jambo hilo ndilo limenifanya kuja na hoja hii ya kubadili matumizi hayo, fedha zote zinazoelekezwa kusomesha watoto, sasa zielekezwe kwenye matibabu bure kwa kila mwananchi wa nchi hii na wazazi waendelee kugharamia elimu za watoto wao!