MWANALUGALI
JF-Expert Member
- Feb 1, 2010
- 601
- 34
Nyerere na serikali yake walituongoza kwa uadilifu na kutufundisha Elimu ya ujamaa na kujitegemea lakini inaelekea katika masomo yao haya walishindwa kabisa! Kwa nini wana taaluma wetu hawakujifunza kujitegemea?
Tido Mhando alifanya kazi BBC kwa mafanikio makubwa, lakini alivyorejea hapa Tanzania alirudi mikono mitupu na kuajiriwa kama Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la taifa ambako amejisahau na hajali taaluma yake wala uzoefu aliopata akiwa BBC.
Mwenzake Jeff Koinage WA Kenya alifanya kazi CNN kwa mafanikio lakini aliporejea kwao akaanzisha kituo cha television cha K24 ambacho kinafanya vizuri sana ( kiko kwenye DSTV channel 413) Hiki ni kituo kinachokuza na kuonyesha Taaluma inavyo thaminiwa na kumjenga mtu!
Kwa Tido, vijana wa Tanzania wanajifunza kujipendekeza na kutokuthamini taaluma lakini kwa Koinage, vijana wa Kenya wanajifunza umuhimu wa taaluma na taaluma kuwasaidia kujitegemea!
Nawasilisha kwa mjadala!