Tido mhando na ajira yake, jeff koinage na taaluma yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tido mhando na ajira yake, jeff koinage na taaluma yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MWANALUGALI, Dec 4, 2010.

 1. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nyerere na serikali yake walituongoza kwa uadilifu na kutufundisha Elimu ya ujamaa na kujitegemea lakini inaelekea katika masomo yao haya walishindwa kabisa! Kwa nini wana taaluma wetu hawakujifunza kujitegemea?

  Tido Mhando alifanya kazi BBC kwa mafanikio makubwa, lakini alivyorejea hapa Tanzania alirudi mikono mitupu na kuajiriwa kama Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la taifa ambako amejisahau na hajali taaluma yake wala uzoefu aliopata akiwa BBC.

  Mwenzake Jeff Koinage WA Kenya alifanya kazi CNN kwa mafanikio lakini aliporejea kwao akaanzisha kituo cha television cha K24 ambacho kinafanya vizuri sana ( kiko kwenye DSTV channel 413) Hiki ni kituo kinachokuza na kuonyesha Taaluma inavyo thaminiwa na kumjenga mtu!
  Kwa Tido, vijana wa Tanzania wanajifunza kujipendekeza na kutokuthamini taaluma lakini kwa Koinage, vijana wa Kenya wanajifunza umuhimu wa taaluma na taaluma kuwasaidia kujitegemea!
  Nawasilisha kwa mjadala!
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  TIDO yuko kifadhila zaidi
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Angalia smile ya TIDO
  inasema yote wala huna haja ya kumtafiti sana.
  he is primitive dude ktk tasnia ya habari nchini
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Kuna tetesi zisizothibitishwa za ubadhirifu chini ya uongozi wa Tido, ndani ta TBC.Inase,emkana kuna vifaa(spares) hewa zimeagizwa na hazionekani, wakuu wanajikanyaga!
   
 5. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,301
  Trophy Points: 280
  Tofauti ya TIDO na JEFF ni kubwa. Jeff Koinange alirudi na kuanzisha kituo chake. Huyu mwingine kilaza tu
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kufananisha tido na jeff ni matusi kwenye tasnia ya uandishi wa habari
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  tumezoea longolongo na kujipendekeza na kulipana fadhila mwisho tunaua taaluma zetu
   
 8. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo Tido ni mharibifu mkubwa ( janga la Kitaifa) wa akili za vijana ambao walitakiwa kujifunza kutoka kwake namna taaluma inavyosaidia kuendeleza nchi yetu. Sasa kwake wanajifunza ufisadi na faida zake, kujipendekeza na kutokuzingatia wanachojifunza!! Huyu Tido Mhando atakumbukwa kwa mengi kama ukabila, ufisadi, uzandiki, kujipendekeza kwa wakubwa, kuhakikisha BBC inachukua upande wakati wa kampeni, kuharibu kizazi chetu na kuwa mfano mbaya kwa elimu ya kujitegemea!!!!
   
 9. kuberwa

  kuberwa JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 568
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Darasani always kuna wa kwanza na wa mwisho, utachanganya na zako kujua position ya Tido na Jef pia class. Tatizo la wabongo ni ufuasi tu bila kureason. Elimu ya ujasiriamali pia ni tatizo, wabongo ni 'risk averse' sign ya kutokujiamini!
   
 10. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2010
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Policies za Tido zimesababisha wanahabari wote pale tbc wamekuwa waoga na wanafanya kazi kwa kujipendekeza ... mfano mdogo; angalia usomaji wao wa habari za kutoka magazetini, it is pathetic!!
   
 11. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Amerudi mikono mitupu na kichwa kitupu.
   
 12. c

  chelenje JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mbavu zanguuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! :eek2::eek2::eek2::eek2::eek2::eek2::israel::israel::israel:
   
 13. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umenena kabisa! Ngoja nikugongee ka thanks.
  "EEEH Mungu wa Watanzania, mbona umetutupa hivyo? mbona hujatupatia mtu wa kuwa mfano kwetu?"
   
 14. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280
  Tido na Jeff ni sawasawa na Barclays Premier League na Kinesi Cup. Jeff aliondoka CNN kwa kufukuzwa baada ya kufanya broadcasting ya wazungu wakitekwa na waasi wa MEND kule Niger Delta. Tido hakufukuzwa BBC ila alitongozwa na mkwere ili aje aongoze TUT into TBC. Kwaiyo unaweza kuona jinsi hao wawili walivyorudi kwao. Jeff alirudi na hasira za kuonesha kua CNN walikosea kumfukuza,ivyo akaanzisha TV network yake iliyo critical na objective. Tido alirudi kumridhisha mkwere kua hakukosea kumchagua yeye. The result ndo tofauti inayoonekana kati yao.
   
 15. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #15
  Dec 4, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tido aliiacha taaluma yake huko huko Uingereza akaja na suruali yake tu, lakini Jeff alirudi na kila kitu chake na anaviendeleza whether kwa hasira kumuonyesha nani au vyovyote vile, lakini kwa faida ya Kenya na Kizazi cha nchi hiyo. He is an inspirational material lakini Tido mmmh!
   
 16. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Acheni majungu wakubwa, kwani mafanikio ni lazima aanzishe media? huwezi jua ame invest kwenye sector gani. Hayo ni mambo binafsi acheni umbeaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Tido piga kazi yako uki staafu anza kufanya vitu vyako. Kama utarudi Tanga kuanzisha kilabu cha pombe ya denge au utabaki Dar ufungue genge uwanja wa fisi yote maisha.
   
 17. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Tatizo la wabongo kama Tido akishapewa kaulaji na kauboss basi ana sahau kila kitu hata taaluma anaiona haina mana kwake nlitegemea angekuwa mstari wa mbele ktk kufuatilia habari na hata kuanzisha kipindi chake cha kuwahoji viongozi wa serikali kuhusu utendaji wao na wananchi wawe wanapiga simu live kuhoji madudu na mazuri matokeo yake nae kamezwa na chama na kuchakachuliwa kabisa uzoefu wake ktk tasnia ha yahabri.jeff ni mpiganaji hodari na si mnafiki anajua anachokitenda.wabongo sijui tutaacha lini unafiki na woga hata pale penye ukweli tunaficha.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Dec 4, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,326
  Trophy Points: 280
  Je kuna yeyete humu anaweza ilinganisha TBC kabla ya ujio wa Tido na TBC baada ya ujio wa Tido?.
   
 19. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TBC kabla ya Tido ilikuwa TVT, Tido alipokuja akaikarabati kwa kuigiza KBC, BBC ikawa TBC. Hope umenipata mzee Pasco. Vinginevyo alianzisha ushindani wa chuki dhidi ya ITV na kukumbatia mafisadi!
   
 20. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kutoka wikipedia, Jamani JF tuwe tunasema ukweli. Story ya Jeff si hivyo kama wengi tunalazimisha iwe. Kwanza yeye si mmliki wa hiyo Channel, pia alifukuzwa kwa scandal ya ngono. Tuwe wakweli. Hivi credibility yetu iko wapi?
  Background
  Koinange was born in Kenya and worked with Kenya's first independent television channel KTN Kenya Television Network. He attended Kingsborough Community College in Brooklyn, NY between 1987–1989 and graduated with an Associate's degree. He also received a Bachelor of Arts degree in broadcast journalism from New York University. Prior to joining CNN, Koinange worked for Reuters Television from 1995 to 2001, covering Africa and serving as their chief producer from 1999 to 2001. He also worked as a producer at NBC News in 1994 and also worked for ABC News earlier in his career from 1991 to 1992. Seven months after leaving CNN, Jeff was hired as a News anchor by a new Kenyan TV station, K24, which started doing test runs in Nairobi in December 2007.He is the host of Capital Talk Show a replica of the CNN Larry King Live
  [edit] CNN career

  Included among the more significant stories Koinange has covered for CNN in Africa were the crisis in Darfur, the civil wars in Liberia and Sierra Leone and the famine in Niger, for which Koinange won an Emmy award.
  Most recently, in early 2007, Koinange was reprimanded by the government of Nigeria for his coverage[1] of the Movement for the Emanicipation of the Niger Delta (MEND). In his report, Koinange accompanied masked MEND guerillas to a camp where they were holding a number of Filipino hostages. The Nigerian government said that the report was "staged", a charge CNN denies.[2]
  Koinange has also covered news outside of Africa, including extensive reporting on the aftermath of the Hurricane Katrina crisis as well as the Iraq War.[3]
  On May 29, 2007, CNN announced that Koinange was no longer employed by the network. He had apparently been caught up with some sex scandal that CNN did not want to become associated with.[4]
   
Loading...