Nimesoma kwa masikitiko katika gazeti la Mwananchi la leo kuwa Tido Mhando hataendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC baada ya mkataba wake kuisha tarehe 15 Desemba 2010.
Tido mwenyewe anakili kuwa mkataba umeisha, lakini hakuridhika na jinsi ujumbe ulivyoletwa kwake.
Watu wengi, wakiwemo wafanyakazi wa TBC, wanalihusisha tukio hili na ushujaa wa Tido kuhakikisha TBC haina upendeleo kwa vyama vyote vya upinzani wakati wa uchaguzi mkuu ulioisha 31 Oktoba 2010.
Kama CCM, nikiwa na maana serikali yake, imefanya hivi, basi anguko lake ni baya. Ni yale ya mfa maji asivyoacha kutapatapa.
Tuliombee taifa letu amani.
Pole Tido, Mungu atakuilipa.