Tido Mhando atemwa TBC

Ni majina ya kibondei tu hayo,je kukiwa na akina Mushi au Tarimo kibao kwenye shirika utalalamika kuwa wote ni ukoo mmoja,otherwise kama una hakika kama hao wote ni ndugu ndio ulalamike

Ni kweli maana wapo akina SULTANI, MAKAME, PANDU, MWINYICHANDE...wazanzibari
akina MAGANGA, MASANJA, SHIJA, NYANG'IJA, NG'WANANGWA...wasukuma/wanyamwezi
akina SHIRIMA, MACHA, KINABO, LYIMO...wachagga

Nadhani tusiangalie wanakotoka bali VIWANGO ila mmh!!
 
Si walifuzu vigezo vya ajira? Wasingeajiriwa kwa sababu tu ya majina yao, ingekuwa ubaguzi pia
 
aFADHALI ! JAMAA AMEKUWA TOOTHLEESS BIG DOG ILE MBAYA !KUMBE KWELI WAKATI MWAINNE MFUMO UNAUA AKLI ZA WATU !
 
Tukiwakuta ndugu au ukoo mmoja kwenye fani nyingine hatulalamiki! kosa ikiwa kwenye ajira hapo ndo utasikia mambo! Mbona kwenye soka hatujalalamika ukoo wa akina Manara, Kihwelu n.k. Hebu tuwaache wachape kazi! Inawezekana ukoo wao walipomwona ndugu yao Tido anafanya vizuri na wengine wakavutiwa wakaamua kusomea taaluma ya utangazaji au haujui kama utangazaji unasomewa?

Wabondei wangu hebu chapeni mzigo hata kama mnatoka familia moja nani anajali? CV zenu ziliruhusu kuajiriwa TBC bwana!
 
JK anataka mlipa fadhila 2 times sasa
Inawezekana maana washkaji wanafahamiana tangu enzi zile pale Gerezani railway club ilipokuwa yanafanyika mashindano ya mchezo wa netiboli,mmoja akiwa ni mtangazaji wa kipindi cha mbili kasorobo pale RTD na mwingine akiwa mgeni wa heshima ktk michezo hiyo mara kwa mara.
 
Hoja iwe ni je hao akina mhando wanaweza kazi??? Kama hawawezi, tutajua kuwa ajira zao zilitolewa kwa upendeleo. Kama wanadunda kazi basi hakuna tatizo.
 
WADAU KWANI KUNATATIZO GANI, JE WE UMEENDA TBC kuomba kazi na ukawa na VIGEZO UKATOSWA?, WAACHE WABONDEI WAPIGE MZIGO
 
Hili ni suala la kuchunguzwa kwani kijuujuu unaweza kusema kuna mchezo mchafu na si tu ni ukabila bali ni ukoo. Kwa makabila mengine watu huwa hawajali vigezo lakini wakiwa Wahaya au Wachaga kila mtu anasahau sifa na kudai ukabila kwa hiyo hapo kuna kuwa na viwango tofauti. Hoja yangu ni kuwa kulifanya kabila moja kuwa na sifa ya ukabila ni uongo mtu kwani viongozi wengi katika mashirika ya umma pale walipopata mianya waliajiri watu wengi kutoka maeneo yao. Lakini ambao walibakia na sifa ya ukabila ni Wahaya na siku hizi tunasikia Wachaga wanatuhumiwa wakati ukweli ni kuwa watu wenye nyadhifa katika taasisi za umma na binafsi siku hizi wamekuwa wanaajiri watu wa makabila yao na hatari zaidi ukoo au undugu wa karibu.

Ni lazima tupiganie kuona kuwa ajira za watu katika taasisi za umma zinatokana na mchakato wa wazi unaojali uwezo wa kitaaluma na kikazi na si undugu na unasaba na kiongozi wa taasisi hizo.
 
GrEaTthinKers
Hivi hakuna watanzania wengine wanaoweza kutangaza?
Kwa nini TBC imejaa ukoo mmoja?

Tido kwangu ni KicheFf Cheff:A S-smoking:

Think.
Tatizo sio ukabila bali ni asili:
Wachaga biashara - TRA& Banks
Wahaya Sheria - Advocates
Wakuria ngangari - Vyombo vya usalama
Wasukuma - maafisa ugani
Wagogo - NGOs
WABONDEI MDOMO- RADIO/TV
 
Back
Top Bottom