Thread maalum kwa ajili ya kutakiana heri ya mwaka mpya na sikukuu ya X-mass, pia kuorodhesha matukio yote yatakayotokea kwenye X-Mass na mwaka mpya

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Leo nimeona bora nije na thread ya pamoja kwa ajili ya kutakiana heri ya mwaka mpya na sikukuu ya X-mass.

Lakini pia kila mtu atakuwa huru ku share picha za jinsi watu walivyo celebrity, na kusherehekea mkesha wa mwaka mpya huko atapokuwa, au kuandika matukio yote yatakayotokea katika siku hizo mbili.

Binafsi napenda kutumia nafasi hii kuwatakia heri ya mwaka mpya na sikukuu ya X-mass wanaJF wote waliopo humu, haswa wale ambao wapo tayari kwa ajili ya kusherehekea sikuu hizo.

Najua kwa baadhi ya nchi (ikiwemo hii niliyopo mimi), hiki ni kipindi kigumu kwetu kuumaliza mwaka salama, lkn kwa uwezo wa Mungu wetu alie mwema, mwenye upendo na huruma ya kweli kwetu, basi tutaumaliza salama salmin.. Ameen.

Update 👇

Wakuu kama thread ilivyojieleza hapo juu, kwamba mbali na kutakiana heri ya mwaka mpya na sikuu ya Christmas, lkn pia tutakuwa tukileta picha, video au masimulizi mbali mbali yanayohusiana na sikuu hizi, pamoja na matukio mbali mbali ya mwisho wa mwaka yanayotokea katika nchi, au maeneo mbali mbali hapa duniani.

Mchana huu nilipokuwa nikipita maeneo ya kitongoji cha Bertram jijini Johannesburg, nilikumbana na mkasa fulan wa kutisha na kushtua, ambao umefanyika saa chache tu kabla ya mimi kupita eneo husika.

Inasemekana wazee wa "tupe chetu ubaki na roho yako" walivamia katika ofisi ya betting na kuchukua kila kitu, kisha kutokomea kusikujulikana. Ila kabla ya kufanya operation walimuomba meneja wa ofisi hiyo (muethiopia) awape chao mapema wasepe, yeye akajifanya kuleta ngonjera, ndo wazee wa "tupe chetu ubaki na roho yako" wakampa njugu kadhaa mwilini mwake (sina uhakika kama alikufa au hakufa) kisha wakachukua kwa nguvu kilichowaleta na kupotea.

Kwa mbali, ni picha ikionesha askari kadhaa na gari yao wakiwa katika eneo la tukio. Hakuna gari iliyokuwa inaruhusiwa kusogelea au kupita eneo la tukio (ukizoom utauona utepe wa askari) hivyo nlichukua hiyo 4to kwa mbali na kuendelea na mishe zangu zilizonifanya nipite eneo hilo.

Pliz msikose kuwa mnatupia picha na matukio yote yanayotokea na kufanyika sehem mbali mbali za dunia.

Asanteni
 

Attachments

  • 20231215_113935.jpg
    20231215_113935.jpg
    1 MB · Views: 4
Back
Top Bottom