Mwaka ndio huo unasepa, Malengo yako uliyojiwekea umeyatimiza kwa kiasi gani?

Dx and Rx

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
1,303
3,085
Heri ya sikukuu kwa familia nzima ya JamiiForums.

Turejee kichwa cha uzi hapo juu.

Nina imani wengi wetu huwa tunajiwekea Malengo ifikapo mwanzo wa mwaka ili tuweze kuyatekeleza na kufika hatua ya mafanikio tunayoitaka.

Mbali na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika safari ya kutekeleza malengo uliyojiwekea, umeweza kuyatimiza kwa kiasi gani, je umebaini vikwazo vilivyokukwamisha na kuwa tayari kubadili mbinu ya kukabiliana navyo au umebuni njia nyingine ya kupita?

Najua ndugu zangu wa kwenda kuhesabiwa kule lazima wakanadi hatua walizopiga ndani ya mwaka husika na kupeana moyo na mbinu mpya za kukabiliana na mwaka unaofuata.

Hapa JF pia tunaweza kushirikishana mbinu, changamoto na vikwazo vilivyotukuta ili tuweze kuingia vyema kwenye mapambano ya mwaka unaokuja.

Karibuni!
 
Nashukuru zimebak siku chache mwaka uishe na malengo yangu yatimie kwa asilimia mia! Lengo langu kubwa kwa mwaka huu lilikuwa ni kuuacha huu mwaka upite free kama ulivyo, nisifanye chochote! Na naelekea kufanikiwa
 
Heri ya sikukuu kwa familia nzima ya JamiiForums.

Turejee kichwa cha uzi hapo juu.

Nina imani wengi wetu huwa tunajiwekea Malengo ifikapo mwanzo wa mwaka ili tuweze kuyatekeleza na kufika hatua ya mafanikio tunayoitaka.

Mbali na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika safari ya kutekeleza malengo uliyojiwekea, umeweza kuyatimiza kwa kiasi gani, je umebaini vikwazo vilivyokukwamisha na kuwa tayari kubadili mbinu ya kukabiliana navyo au umebuni njia nyingine ya kupita?

Najua ndugu zangu wa kwenda kuhesabiwa kule lazima wakanadi hatua walizopiga ndani ya mwaka husika na kupeana moyo na mbinu mpya za kukabiliana na mwaka unaofuata.

Hapa JF pia tunaweza kushirikishana mbinu, changamoto na vikwazo vilivyotukuta ili tuweze kuingia vyema kwenye mapambano ya mwaka unaokuja.

Karibuni!
Mwaka mmoja ni muda ambao binadamu wamejiwekea hivyo usitishwe sana wala kuhesabu mfanikio kwa kigezo cha mwaka kwa mwaka.
 
Si jambo jepesi kuumaliza mwaka ukiwa umelipa madeni yote. Ni jambo ambalo nilikuwa nalipambania miaka kwa miaka, hatimaye mwaka huu limetimia.

Kila mtu ana malengo yake, mimi langu hilo linetimia.

Kheri ya Christmass na Mwaka mpya
Pongezi kwako mkuu
 
Hongera sana mkuu kwa kumaliza madeni nina imani mwaka huu utaepukana nayo au kuyakwepa kwa kiasi kikubwa.
 
Back
Top Bottom