Thinking aloud: Magufuli ni Chaguo la Mungu

Kaunga

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2010
Posts
12,529
Reaction score
13,502
Kama mmoja wa UKAWA nasema hivyo kwa uhakika nikimlinganisha Yakobo jinsi alivyoupata uzaliwa wa kwanza kwa njia 'zisizo haki' lakini mapenzi na mpango wa Mungu ukaendelea kutimilika kupitia yeye. Lowassa kupokwa ushindi ni kama Essau kutapeliwa uzaliwa wa kwanza.

Njia za Mungu hazichunguziki, na tunashukuru kwa ajili ya Magufuli maana anatekeleza yale ambayo ukawa tumekuwa tukiyapigia kelele.

Na hii inazidi kunikumbusha ile sala ya Bwana.....mapenzi yako yatimie; na pia sala ya Yesu kwa Baba yake....kikombe kiniepushe ila si kwa mapenzi yangu...

Go Magufuli, changamoto bado unazo sana na ushakuwa unpopular kwa chama chako.
 
Taratiiibu mkaanza kukubali muziki wa Magufuli

Anachokifanya ndicho tulichokihubiri all these years. Bado mbele giza, maana ccm ndio mnaisoma number.
Kama wanainchi wa kawaida tunataka things zihappen basi
 
Magufuli ana good intentions
kaipania hii kazi
angependa kukumbukwa kama aliekuja 'kuijenga' nchi

but.......too early kumtangaza 'chaguo la Mungu'

Mobutu na Iddi Amini pia waliwahi kutangazwa 'machaguo ya Mungu huko makwao'
miaka ya mwanzo tu walipochukua madaraka
na kila walipokuwa wanapindisha au kuvunja sheria ili 'kuharakisha maendeleo'
kwa wananchi walipigiwa vigelegele nchi nzima...mpaka pale waliopiga vigelegele walipoanza
'kuisoma namba pia'

Hata kama ana nia nzuri...sheria zifuatwe
watu wasibomolewe nyumba bila taarifa au huku kuna zuio mahakamani
na sisi turukeruke na kusherehekea kisa ni 'ccm wanaisoma namba'

jamani ni siku 20 tu hizi.....kuna miaka 5 mbele......tutamlewesha sifa tutajuta
 
We kweli GT
 
Hivi, hii slogan ya "chaguo la Mungu" mbona inashika kasi hivyo...
Tangu JMK tunaona machaguo ya Mungu tu...
Mihemko inatusumbua sana..JPM is doing well so far...
 
The Boss inategemea nini mtu ana maanisha akisema chaguo la Mungu.
Kikwete ni chaguo la Mungu na viongozi waliopita ni chaguo la Mungu bila kujalisha wamepatikanaje.
Kwangu mimi just because kimamlaka ya kibinadamu ambayo tunaaswa tuyatii ni kiongozi basi Mungu karidhia.

Mungu alifanya moyo wa Farao kuwa mgumu ili asiwaruhusu waisraeli kuondoka mapema. Kikwete amefanya alofanya na Mungu kaachilia ili watu waanze kuwa na mawazo ya kimapinduzi au mabadiliko. Ni mtazamo wangu lkn.
Pombe kwa week 3 kafanya mengi ya kimapinduzi anastahili sifa, ila ana mengi zaidi na vizuizi au vigingi vingi sana baada ya kuanza kufanya haya aliyoyafanya ndani ya week 3 hizi. Hivyo anahitaji kila aina ya support hasa kutoka UKAWA na wananchi wa kawaida coz he is definitely going to need them as CCM elites are surely going to oppose his every move.
 
Last edited by a moderator:
Kama mmoja wa UKAWA nasema hivyo kwa uhakika nikimlinganisha Yakobo jinsi alivyoupata uzaliwa wa kwanza kwa njia 'zisizo haki' lakini mapenzi na mpango wa Mungu ukaendelea kutimilika kupitia yeye. Lowassa kupokwa ushindi ni kama Essau kutapeliwa uzaliwa wa kwanza. Njia za Mungu hazichunguziki, na tunashukuru kwa ajili ya Magufuli maana anatekeleza yale ambayo ukawa tumekuwa tukiyapigia kelele.
Na hii inazidi kunikumbusha ile sala ya Bwana.....mapenzi yako yatimie; na pia sala ya Yesu kwa Baba yake....kikombe kiniepushe ila si kwa mapenzi yangu...

Go Magufuli, changamoto bado unazo sana na ushakuwa unpopular kwa chama chako.

Nakuunga mkono kabisa kuwa Magufuli ni chaguo la Allah! Ni wana UKAWA wachache wanaweza kusema haya! Hongera sana.
Hapo kwenye red umeharibu kabisa labda ueleze kiundani ni kivipi alipokwa? Mlikuwa wapi? Aliposema nyie mpige kura swala la kuzilinda mmwachie yeye ulimuelewa?
Hakika Magufuli ni chaguo la Allah tumpe ushirikiano..
 
HAKUNA MTAWALA DUNIA HII ATAKAYE KUJA KUWA CHAGUO LA MUNGU !
-huyo unayemshabikia ana mabaya mengi sana ila yananyamaziwa kwakuwa tu kaaamua kuwa DIKTETA.
 
Kama mmoja wa UKAWA nasema hivyo kwa uhakika nikimlinganisha Yakobo jinsi alivyoupata uzaliwa wa kwanza kwa njia 'zisizo haki' lakini mapenzi na mpango wa Mungu ukaendelea kutimilika kupitia yeye. Lowassa kupokwa ushindi ni kama Essau kutapeliwa uzaliwa wa kwanza. Njia za Mungu hazichunguziki, na tunashukuru kwa ajili ya Magufuli maana anatekeleza yale ambayo ukawa tumekuwa tukiyapigia kelele.
Na hii inazidi kunikumbusha ile sala ya Bwana.....mapenzi yako yatimie; na pia sala ya Yesu kwa Baba yake....kikombe kiniepushe ila si kwa mapenzi yangu...

Go Magufuli, changamoto bado unazo sana na ushakuwa unpopular kwa chama chako.

Utakuwa unamuongelea mungu yupi hasa? Wako wengi tu. Be specific usije ukwa unafanya kufuru.. Blasphemy.
 
HAKUNA MTAWALA DUNIA HII ATAKAYE KUJA KUWA CHAGUO LA MUNGU !
-huyo unayemshabikia ana mabaya mengi sana ila yananyamaziwa kwakuwa tu kaaamua kuwa DIKTETA.
Huu ni mtazamo mwingine wa tafsiri ya CHAGUO LA MUNGU.
 
Utakuwa unamuongelea mungu yupi hasa? Wako wengi tu. Be specific usije ukwa unafanya kufuru.. Blasphemy.

Mungu wa Israel, Isaka na Yakobo. Mungu katika nafsi tatu ambazo ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Mungu ninayemuamini mimi Mkristu Mkatoliki
 
Worse ni kwamba JK nae alisemwa ni chaguo la mungu. Huku ni kutotumia akili hata kidogo. Kwa hiyo mungu huyu aliyesemwa ndiye aliyetutesa maiaka 10 akitaka kufaidi nini hasa toka kwetu Watz?. That type of god should not be the same for magufuli otherwise we are worse then we thought.
 
The Boss inategemea nini mtu ana maanisha akisema chaguo la Mungu.
Kikwete ni chaguo la Mungu na viongozi waliopita ni chaguo la Mungu bila kujalisha wamepatikanaje.
Kwangu mimi just because kimamlaka ya kibinadamu ambayo tunaaswa tuyatii ni kiongozi basi Mungu karidhia.

Mungu alifanya moyo wa Farao kuwa mgumu ili asiwaruhusu waisraeli kuondoka mapema. Kikwete amefanya alofanya na Mungu kaachilia ili watu waanze kuwa na mawazo ya kimapinduzi au mabadiliko. Ni mtazamo wangu lkn.
Pombe kwa week 3 kafanya mengi ya kimapinduzi anastahili sifa, ila ana mengi zaidi na vizuizi au vigingi vingi sana baada ya kuanza kufanya haya aliyoyafanya ndani ya week 3 hizi. Hivyo anahitaji kila aina ya support hasa kutoka UKAWA na wananchi wa kawaida coz he is definitely going to need them as CCM elites are surely going to oppose his every move.

Kuna double standard unaifanya na i am sure hata huioni
First Kikwete unampa lawama yeye as individual zaidi hutaki kutambua kuwa
hata yeye Kikwete pengine 'alidhibitiwa' na CCM if its true kama kuna watu powerfull CCM
wa kumdhibiti Rais.....kama hakuna hao watu ilikuwa uzembe wake Kikwete
basi na huyu wala tusimtafutie 'visababu' akishindwa huko mbele
itakuwa uzembe wake pia.... tusije kuwa tunaanda mazingira ya kumtetea akishindwa huko mbele

Inaweza kuwa nguvu ya soda au mbinu za kuteka akili watu
ili 'ajifanyie' anayoyataka huko mbele bila kubuguzwa
ndo maana nime mention kina Mobutu na Iddi Amin...walipendwa haswa
na mpaka leo kuna watu wanawatetea kuwa 'walishauriwa' vibaya tu
uzalendo wanao na nia zao zilikuwa njema
 
Unaona ugumu gani kusema ukweli wa ulichokuwa unataka kusema? "ILIKUWA NI LAZIMA LOWASSA ACHUKUE FORM CCM ILI TUMPATE MAGUFULI. MUNGU NI MWEMA
 
Kuna double standard unaifanya na i am sure hata huioni
First Kikwete unampa lawama yeye as individual zaidi hutaki kutambua kuwa
hata yeye Kikwete pengine 'alidhibitiwa' na CCM if its true kama kuna watu powerfull CCM
wa kumdhibiti Rais.....kama hakuna hao watu ilikuwa uzembe wake Kikwete
basi na huyu wala tusimtafutie 'visababu' akishindwa huko mbele
itakuwa uzembe wake pia.... tusije kuwa tunaanda mazingira ya kumtetea akishindwa huko mbele

Inaweza kuwa nguvu ya soda au mbinu za kuteka akili watu
ili 'ajifanyie' anayoyataka huko mbele bila kubuguzwa
ndo maana nime mention kina Mobutu na Iddi Amin...walipendwa haswa
na mpaka leo kuna watu wanawatetea kuwa 'walishauriwa' vibaya tu
uzalendo wanao na nia zao zilikuwa njema
Hayo maneno ya kukosa hoja za msingi , mkubalini Magufuli. Mpaka ashindwe ndo tuyaseme hayo. Sasa ni kazitu.
 
vipi alimpigia kura?
kwani nae ni raia wa Tanzania!
 
HAKUNA MTAWALA DUNIA HII ATAKAYE KUJA KUWA CHAGUO LA MUNGU !
-huyo unayemshabikia ana mabaya mengi sana ila yananyamaziwa kwakuwa tu kaaamua kuwa DIKTETA.
Mkuu hebu yaseme! Kwani udikteta wake ni upi? hebu toa mfano...
 
HAKUNA MTAWALA DUNIA HII ATAKAYE KUJA KUWA CHAGUO LA MUNGU !
-huyo unayemshabikia ana mabaya mengi sana ila yananyamaziwa kwakuwa tu kaaamua kuwa DIKTETA.
Hahaaa, Mfa maji kweli haachi kutapatapa. MAGUFULI atawaaibisha sana vimdomo mdomo, udikteta wa kukuzuia kusems mabaya yake ni upi? Ni usafi wake ndiyo unafanya udikteta wake unachukua nafasi na kukubalika.
 
Back
Top Bottom