Salaam wana MMU,
kuna kale kamsemo kwamba mpenzi wako wa sasa ni mpenzi wa zamani wa mtu mwingine, kana kaukweli fulani. An ex is like a dormant volcano kwamba haierupt lakini ipo one day inaweza kuja kuerupt tena. Point of reference;ni majuzi tu nimekutana na ex-mpenzi wangu ambaye tulidate like 2 years ago ila baada ya kuhama physical location ukawa ndio mwisho wetu. Hiyo majuzi katika pita pita zangu za kwenda kushangaa ulaya a.k.a mlimani city (ndugu zangu wa chit-chat wananipata swadakta) nikakutana na mpenzi wangu huyo wa zamani. Kiukweli kwa sasa ameng'ara sana na kunawairi na kupendeza mpaka mwenyewe nikakiri kimoyomoyo. Alikua na jamaa mmoja ambae judging from the looks, their positions and posture it doesnt need an elite person kujua huyo jamaa ndio mmiliki halali wa binti huyu na jamaa ndio aanahudumia kila kitu. Nilitaka kukausha nimpite kamasimjui ila binti akanikumbuka akaniita, alifurahi sana akanihug pale, akanitambulisha kama rafiki yake wa zamani kwa huyo mpenzi wake. Basi tukapiga story dakika mbili tatu nikamzuga nina haraka so she gave me her dials. Tumeanza kuchat, akaanza kukumbushia mambo ya zamani, mara anipigie late night calls, vi clip vya kijinga whatsapp n all those stuffs. Nilimbana kwenye angle flan katika kuchat kwetu mwisho akakiri she still got some sort of feelings for me and she wont mind vile tukihave a friendly match kujikumbushia back in days.
Hii kitu nimewaza nikaona kumbe sometimes tunaweza kua na wapenzi wetu wenyewe tunaona tumefika tunapeeendwa kumbe kuna watu ambao walikonga nyoyo zamani ambao always watakua wana special place kwenye nyoyo zao. Sasa kama mambo yenyewe ndio haya, si mtu unaweza ukaoa/kuolewa na mtu halafu kumbe kuna ex wake ambae alikua anamkuna kweli kweli ambaye akichombeza kidogo tu anapewa mzigo kama kawaida? Au ndio mambo anayosema Rich mavoko kwamba kuchapiwa ni siri ya ndani? (personally i hate this line in the song).
Anyways, wafaransa wenyewe wanasema :C'est la vie....
Jumapili njema wapendwa!