Is your Ex lasts for the rest of your life?

Jack HD

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
851
1,166
Hope All is well!!!

Kuna utatanishi mkubwa sana juu ya nadharia ya kuendeleza mawasiliano yasiyo ya kimapenzi na watu tuliopita nao kwenye mahusiano hayo (Ex wife/ Ex girlfriend). Kuna wanaokubaliana na nadharia hii kwamba si vibaya kuendeleza hayo mawasiliano lakini si kuendeleza mapenzi yetu ya zamani. Kuna kundi la pili la watu ambao wao hupinga kabisa juu ya kuendeleza mawasiliano na ex wa zamani kwa njia yoyote ile. Tuacahane na wale wenye kutaka kuendeleza vyoote yaani mawasiliano na mapenzi.

Latest Experience
Jana mida ya jioni nilipata kupokea message kwenye simu yangu ya kiganjani. She was my 2011 ex gal. She is currently married and blessed with a very good kid. She missed me but si kimapenzi (i'm not sure but lets think that way coz tunaheshimiana). Huyu dada kuna kipindi nilimchunia na alikuwa anapenda sana kuendeleza mawasiliano na ni kweli kuwa anaheshimu sana ndoa yake na hataki kufanya ujinga wowote (Through her words na nilivyomsoma).

After kama three months za kumchunia, jana akawa kama anatoa darasa kwangu kuwa si vibaya kuendeleza mawasiliano kama heshima na hekima ikiendelea kuwepo. Namnukuu, "kwanza hata mume wangu hakujui, kwa hiyo hata kama ukija nyumbani atajua ni rafiki wa kawaida kama walivyowengine" Kwa kufupisha maneno jana ikawa kama ni mtu ambaye alikuwa amenikumbuka kama mtu ambaye tulishawahi date kipindi cha nyuma. Chatting haikumtosha baadae Akahitaji kusikia sauti yangu yaani anipigie simu, nikamrusha nikamwambia tutaongea jioni muda huu nimebanwa na kazi. Lengo langu hasaa ilikuwa asahau, siku ipite maisha yasonge. Karibu na jioni akaniomba namba ya mtandao ambao unafanana na ule ambao yeye anatumia ili aweze kunipigia kwa muda mrefu. Niliipotezea hiyo text but ziliingia text kama hzo mbili baadaye, nikashindwa kupotezea ikabidi nitume tu ile namba.

Kweli jioni hiyo alipiga simu na tukaongea mengi, The past and the present. Simsemehi vibaya but ni kweli alinikumbuka na i admit she truly loves her husband. She loves her marriage too. Simdhanii kuwa atakuja kutaka kuendeleza our old times. Alifurahi na mpaka alipokata simu bado chatting za hapa na pale zikawa zinaendelea.

Morning
Asubuhi naamka, The first text was from her, "Asante sana kwa muda wako jana, nimefurahi kusikia sauti yako, najua utakuwa salama" Si, vibaya kujibu text ya namna hiyo na hautakiwi kuwaza vibaya kwa text ya dizaini hiyo tu

Few chats asubuhi hii zikaendelea mara akajiongelesha, "Ila nimemiss kukuona hadi aibu"
SITOWEZA KUONANA NAYE na story inaishia hapo.

Back to the topic
Hivi wadau, ni vema kuendeleza mawasiliano yasiyo ya kimapenzi na aliyekuwa ex wako ambaye kwa sasa yupo kwa marriage? Mawasiliano tunayoongelea hapa sio text za kusalimiana tu za salamu maybe kila baada ya mwezi. Mawasiliano ya kumpa kampani ya kirafiki close friendship ndio tunayoiongelea hapa.

Kusherehesha uzi huu naomba niquote japo kidogo kuhusu hawa maex wetu.

"Going back to your ex is like taking your spit from the ground" (M.F. Moonzajer)

“Unbeknown to us, some of the people who we hope are missing us wherever they are do miss us; some miss someone else; and some are dead.” (Mokokoma Mokhonoana)

“I know we are miles and miles away from one another, but I always believed that as long as our souls are connected to each other, the flame of our love will burn forever. Only souls can resist death, our physical connection is meaningless... you always stayed in me and me in you, I never lose my hug I admit sweetie . I appreciate and admire my hug.” (Abdul'Rauf Hashmi)

"All my life there has been ex wife or a girl friend" (Roonie wood)

“Having a date with someone other than your ex-wife after being a married man for more than twenty five years was an important occasion alright, but wearing a tie she bought with such strong emotional value attached to it was a form of cowardice, a subconscious reluctance to let go.” ( Vann Chow, The White Man and the Pachinko Girl )
 
Hamna ubaya wowote kama ni mahusiano ya kawaida tu ila ya kimapenzi hatari
 
Mie Sina Uadui Na Gal Friends Zangu Wote Tena Ndo Tumekuwa Marafiki Wakutupwa Kama Dada Na Kaka
 
kama hamkugombana hakuna shida bali upendo utawale daima, na kama mligombana ni vizuri kusamehe na kuendelea na maisha kukumbukana sio vibaya.
 
KAMA MAPENZI YENU YALIAMBATANA NA URAFIKI KATI YENU,BAEI HATA MKIACHANA MAPENZI YATAKWISHA ILA URAFIKI UTADUMU
 
i
KAMA MAPENZI YENU YALIAMBATANA NA URAFIKI KATI YENU,BAEI HATA MKIACHANA MAPENZI YATAKWISHA ILA URAFIKI UTADUMU
its sound. nakubaliana na wewe. lakini huoni hatare kuwa mnaweza siku moja mnaweza kukumbushia
 
Ujumbe wako umenisononesha sana.
Kuna ex girl wangu (2006/11) huwa anakaaa hata miaka miwili, lakini iko siku atanipigia na kunijulia hali.
Kitu cha ajabu ni kwamba; Hakuwahi kuihifadhi (save) namba yangu kwenye simu yake na vivyo hivyo kwangu, lakini kila mtu hata akiamshwa usiku wa manane anaikumbuka namba ya mwenzake.
Huwa napata wakati mgumu kila akinipigia kwani tukianza kuzungumza basi tutazungumzia mengi.
Nimeshindwa kumsahau na yeye pia kashindwa kunisahau japokuwa kila mtu yuko na familia yake.

Kuwasiliana naye si vibaya ila kutokana na namna alivyosema kwamba; 'Nimemis kukuona hadi aibu' ni dhahiri kwamba anahitaji akuone ili afahamu status ya maisha uliyonayo na nakuahidi kuwa ukionana naye kama una maisha mazuri, basi tambua kuwa mahusiano yatarudi upya na hata ukigoma hatoacha kukusumbua
 
i

its sound. nakubaliana na wewe. lakini huoni hatare kuwa mnaweza siku moja mnaweza kukumbushia
Ulivyoongea inaonekana ulimuacha wewe wakati yeye bado alikuwa anakupenda! Ni hatari mwanaume kumuacha mwanamke wakati mwanamke bado anampenda. Atafanya chini juu mtaanza kulana kubali au kataa. Huyo wako ana uhanga anataka mliendeleze libeneke. Mara nyingi mwanamke akikutaka huponyoki kuponyoka ni kukata mawasiliano. Endelea na kuchati naye utaleta mrejesho wa kutatuliwa marinda (mumewe atakukamata hata baada ya miaka 10 na rinda lako utakuwa umeliweka rehani). Tuna uzoefu na haya majambo ndugu yangu
 
Ujumbe wako umenisononesha sana.
Kuna ex girl wangu (2006/11) huwa anakaaa hata miaka miwili, lakini iko siku atanipigia na kunijulia hali.
Kitu cha ajabu ni kwamba; Hakuwahi kuihifadhi (save) namba yangu kwenye simu yake na vivyo hivyo kwangu, lakini kila mtu hata akiamshwa usiku wa manane anaikumbuka namba ya mwenzake.
Huwa napata wakati mgumu kila akinipigia kwani tukianza kuzungumza basi tutazungumzia mengi.
Nimeshindwa kumsahau na yeye pia kashindwa kunisahau japokuwa kila mtu yuko na familia yake.

Kuwasiliana naye si vibaya ila kutokana na namna alivyosema kwamba; 'Nimemis kukuona hadi aibu' ni dhahiri kwamba anahitaji akuone ili afahamu status ya maisha uliyonayo na nakuahidi kuwa ukionana naye kama una maisha mazuri, basi tambua kuwa mahusiano yatarudi upya na hata ukigoma hatoacha kukusumbua
Mkuu binafsi nimeshafunga vioo, lakini huyo wa kwako mmmmhh mmefika pazuri;);)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom