Is There Such a Thing as Agro-Imperialism? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Is There Such a Thing as Agro-Imperialism?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Dec 4, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Companero na Zakumi,

  Nyie ni wazee wa Kilimo Kwanza, what is your take on this?

   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Ukoloni unarudi kwa mlango wa nyuma Ngambo Ngali [​IMG] 15th September 2009, 06:03 PM

  Sasa imeaminika pasi kuacha shaka lolote kuwa kilimo kwanza ilikuwa ni pathway ya kukaribisha wageni toka nje kuchukua ardhi yetu. Hivi kweli Watanzania tumeshindwa kulima hiyo ardhi jamani. Sokoine University iko katika orodha ya vyuo bora 100 vya Afrika ina miaka zadi ya 30 je products wa miaka yote hiyo wako wapi na wanfanya nini mpaka tuite investors.
  Tuna vyuo vya kilimo vya tokea enzi za mkoloni mlingano, ukiriguru, mati ilonga , mpwapwa, tumbi just to mention a few jee products zote hizo haziwezi kulima hayo mashamba. Hela za EPA zilizorudishwa zimeenda TIB kwa ajili ya kilimo kwa nini Watanzania wasipwe hizo hela kuendeleza mashamba hayo ambayo wafungwa wameshindwa na au hawataku kuyalima.
  Wafungwa na vijana wa JKT walikuwa ni labour power tosha ya kudevelop landbank hiyo kitu gani kimewashinda wafungwa manafanya nini gerezani cha maana kama sio kula kodi zetu bila kuwa productive. Reli, shule, hospitali, ofisi za serikali wakati wa mkoloni zilijengwa na wafungwa sasa leo wafungwa wana ardhi, watalaamu wa kilima na pesa iko TIB lakini tunatafuta mwekezaji aje alime.

  JKT sasa hivi kazi yao kwenda kuzuia wapiga debe ubungo zamani ( sio zamani sana) zilikuwa kambi za uzalishaji wa hali ya juu. Oljoro, masange, mafinga, bulombora, makatupora, ruvu etc ona sasa JKT ni magofu tu wataalamu wapo hakuna kinachoendelela

  50 years after independence we are still looking for investors, why then did we fight for our independence if that is the position. hii mentality itatutoka lini cant we do things on our own? it seems the only thing we can do on our own is stealing EPA Funds, i can tell you in that we dont need investors, donors or expatriates.

  What kind of people are we?

  Now i sart to believe that kilimo kwanza is not for wakulima waliotusomesha kwa jembe la mkono, waliolima kahawa na korosho mpaka tukawa kwenye ramani ya dunia kwa ajili ya mazao hayo bali , bali ni kaulimmbiu ya kukaribisha matajiri wa jangwani walio na ardhi isyo rutuba walime kwetu kwenye rutuba, ardhi ichoke sie tusipate kitu na halafu wao hao waondoke sisi tuambulie land rent ambayo itaishia kufurnish ofisi za wizara ya kilimo na Halmashauri na kumwacha mwananchi hoi kama mwanakijiji na jembe lake begani akiwa hajui mwelekeo wake.
  BABU ZETU WALIKUWA NGUMBARU NDIO MAANA WALIDANGANYWA KWA SHANGA, VIOO NA RISASI SISI TUMESOMESHWA NA HAO WAKULIMA TUNAOWADHULUMU PAMOJA NA ELIMU YETU USHAWISHI GANI UNAOTUFANYA TUDANGANYIKE, NI NINI HASA??????

  REV CHAMA CHETU KI WAPI ? TUNACHELEWA, TURUDISHE KWENYE NCHI YA AHADI
   
 3. Bambo

  Bambo JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 237
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  kilimo kwanza ni wazo nzuri tusilaumu bila kuchunguza!!tuchangie namna ya utekelezaji wake,nilikuwa kijijini hivi karibuni mipango ya kilimo kwanza imenusa huko watu wanashauriana namna bora ya kugawa mbolea ya ruzuku ya kilimo kwanza.hakuna namna ya kufanya maendeleo bila kuwarudisha kundini wakulima ambao wamekata tamaa ya kilimo vijijini kwa sababu mbalimbali ikwa ni pamoja na kukosa pembejeo!!...ambalo ni matokeo ya kukatika kwa ruzuku kulikosababishwa na maamuzi ya kimataifa na sio serikali zetu kama wengi wanavyodhani. Matatizo mengi ya nchi zetu ni kuwa na uzalishaji mdogo unaotokana na kuwa na wazalishaji wachache wengi ni walevi huko vijijini!..na mjini ndo hivyo mtu mmoja analisha watu 20 pamoja na extended family.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Well the answer lies between these lines....
  - They've found that impoverished governments are often only too welcoming, offering land at giveaway prices. A few transactions have received significant publicity, like Kenya's deal to lease nearly 100,000 acres to the Qatari government in return for financing a new port, or South Korea's agreement to develop almost 400 square miles in Tanzania. But many other land deals, of near-unprecedented size, have been sealed with little fanfare.
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ujinga wa Mwafrika!
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  sikio la kufa halisikii dawa
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mchungaji nakuomba tena nakusihi sana usinihusishe na sera mufilisi!
   
 8. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Rev:

  Samahani sikuona hii posti yako. Nipe muda niisome kwanza na baadaye nitarudi.
   
 9. bona

  bona JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  kilimo kwanza ndio hatua ya mwisho ya unyonyaji baada ya apo itafuata kupunguzwa cjui kwa carbon monoxide au cyanide gas only God knows, kilimo kwanza ni sera tuliyobandikwa toka nje haijabuniwa na serikali yetu kama wanasiasa wetu wanavyotaka tuamini, tukishawapa ardhi hakuna amabacho tutakua tumebakiwa nacho.
  imebuniwa ili kutusahaulisha strategy ya vision 2025 ambayo inaelekea kushindwa, ngoja nitaje strategy tulizobuniwa na hazijaweza leta maendeleo
  1.structural adjacement programme
  2. azimio la zanzibar
  3.millenium development goal
  4.vision 2025
  5.mkukuta
  6.mkurabita
  7.azimio la arusha
  je katika yote hayo si azimio la arusha tu ndio lililotuletea maendeleo? mengine yaliyobaki yaliyobuniwa nje yametufilisi zaidi, sasa inakuja kilimo kwanza eti wameamua kuibadili jina kutoka green revolution ili ionekana ya kitanzania zaidi maana ingekuja kwa jina la green revolution ingegundulika kirahisi kua ni ya nje!
   
 10. Companero

  Companero Platinum Member

  #10
  Dec 11, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  WB: Foreigners buying African farms a good thing
  KIGALI
  The Outsourcing of food production in Africa by some Asian and Middle-
  Eastern countries may boost global stock and may help stave off of
  future food crises, the WB says.
  In the aftermath of the last year's food crisis, capital-rich nations
  who lack sufficient arable land to feed growing populations started
  buying or leasing large portions of cheap, fertile African soil to
  grow staple crops.
  WB director of Sustainable development Hartwig Schafer. Adding that
  the much needed investment in infrastructure, processing and
  agricultural technology could improve yields and mitigate the impact
  of volatility in world food markets.
  Opponents say the schemes will not improve food security in Africa
  because the capital, technology and expertise are unlikely to trickle
  down to the poor farmers.
  Smallholders may be pushed off land which they have tilled for
  generation but have no legal rights over, critics say...

  Chanzo: Mtandao
   
 11. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Rev:

  Nimepitia article na itabidi niiweke kwenye makarabashi yangu ya kazi. Kwa kifupi tu: If Tanzanians play their cards nicely, I believe the whole thing could be a blessing or at least a blessing in disguise.

  Sina misamihati ya kuelezea thesis yangu. Lakini kuna vitu muhimu vya kuangalia hapa.

  Kitu cha kwanza ni thamani ya capital. Capital iliyopo Saudi Arabi kwenye reserve ikisubiri nchi hiyo ipate matatizo ya kifedha ndio itumike na hile itakayokuja Tanzania zinaweza kuwa na thamani sawa. Lakini itakayokuja Tanzania na kuwa invested in Agriculture itakuwa na manufaa mengi kwa humanity kwani itaweza kutoa ajira, kuboresha miundo mbinu na mambo mengine.

  kitu cha pili. Investment katika kilimo ni renewable resource. Kwa mfano, vipande vilevile vya ardhi vilivyotumika Marekani, bado vinaendelea kwa zaidi ya miaka 200. Lakini hiyo ardhi hiyo ingetumika kwa uchimbaji wa madini kama dhahabu, basi dhahabu yote ingekuwa imeondoka. Hivyo sioni sababu ya watu wanaotoa sehemu za ardhi kwa ajiri ya machimbo ya madini, walete ubishi usio wa kiuchumi kwenye kilimo.

  Kitu cha tatu.Uzalishaji katika sekta yetu ya kilimo is utterly pathetic. Kwa sababu tunatumia masaa mengi kwenye matumizi ya primitive tools. These primitive tools are poverty traps that have entangled African societies for so many years (MIAFRIKA NDIVYO ILIVYO). I belive foreign capital could help to buy expertise and equpments as well.

  Kwa mfano kwenye articale kama Saudi Arabi ambao hawakuwai kulima kwa millennia waliweza kutumia capital yao kuweza kuzalisha ngano jangwani na ku-export. Kwanini capital isiweze kubadilisha the way Tanzania approaches agriculture industrial.

  Nne, the global has reached 6 billion. Hivyo baadhi ya mazao yatakuwa na demand kubwa na kufanya shughuli za kilimo kuwa sexy again. Kuwanyeshwa chai au kahawa watu wa China, India, Ulaya na Marekani kutahitaji wakulima wa Afrika.

  Tano, mabadiliko ya hali ya hewa yanabadilisha sana mbinu zinazotumika kwa kilimo kwa watanzania. Hivyo capital na machinely ni lazima zitumike.

  Wako

  Free Marketeer and Kabaila

  Z10 Mwanamavungi.
   
 12. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kaka,

  Miye nimekuchokoza tu, najua haufanani na Kilimo Kwanza!
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  Dec 12, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Z10, ukiweka kilimo pembeni, je ni sekta gani nyingine imepokea misaada na fdi kubwa kuliko kilimo na kuonesha mafanikio makubwa?! Je, hili likifanyika kwenye kilimo kutakuwa na utofauti wowote na kile kilichotokea kwenye madini hapa Bongo?!
   
 14. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #14
  Dec 12, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Steve D:

  Nilianza na condition kuwa If Tanzanians play their cards nicely....... Tukirudi kwenye swali lako la msingi. Watanzania kushindwa katika miaka 50 toka uhuru ni kitu kilichoandikwa ukutani au kwenye jiwe. Na sababu moja kubwa ambayo wengi wanaigopa kuitaja ni backwardness.

  Hapa watu wanasema standard yetu imeshuka, lakini Ngabu akiwauliza je kabla ya hapo ni nini mlichokuwa nacho, hakuna anayetoa jibu la maana. Hivyo backwardness ni kikwazo kikubwa.

  Pamoja na kuwa ni kikwazo, watu wakaichukua kama strength ya kujenga taifa au kufanya industrialization wakati hakuna experince, excelleny, expertise na mambo mengine yanayohitaji katika mafanikio.

  South Korea, Saudi Arabia na nchi nyingine zilizochipuka kwenye uchumi zimechukua zaidi ya miaka 50 kuweza ku-manage resources zao.

  Kuhusu madini na kilimo kuna tofauti kubwa sana katika jinsi ya ku-invest. Kilimo ni renewable resource. Katika kipande kimoja unaweza kulima kwa zaidi ya miaka 1000. Kwenye madini, once you take out the metal, the real deal is gone.
   
Loading...