The World is a flat plane and not a globe

The World is a flat plane and not a globe

Unashangaa watu kwenda mwezini na wakaonyesha video na picha ila haushangai Mtu aliweza kuupasua mwezi vipande viwili na ukarudi katika hali yake!majini kufanya ibada na kutumika kutengeneza utajiri! Haushangai hadithi za bawa moja la nzi lina dawa hivyo akidumbukia kwenye maziwa kwa bawa moja umzamishe kabisa ndio unywe maziwa yako!
Hushangai hayo ambayo hayana ushahidi wowote! Kalaghabao.
Haya mambo ya Sayansi huwa yana uongo mwingi sana, tatizo watu wengi wanapenda story za Sayansi basi hata muda wa kuhoji hawaupati.

Nilishawahi kuwauliza humu wajinga fulani kwamba, kuna jafribio gani la Kisayansi liliwahi kufanywa likathibitisha ya kuwa Dunia inazunguka ? Auwatuthibitshie tu ya kuwa Dunia inazunguka, majibu yao ni vituko.

Sayansi ya maumbile na hasa ya anga niliachaga kuamini, pale niliposikia habari za mtu kwenda mwezini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The pot calling the kettle black
Hapana nakataa issue sio upeo wa macho issue ni humidity,vumbi,fog na vitu kama snow n.k zinapoteza sight .

Au tafuta camera au telescope ya P9 mkuu nenda baharini fungua app ya weather angalia mda huu kuna humidity kiasi gani kama ni ndogo anza kuvuta umbali kama kulikuwa na meli ambayo hata kwa darubini hukuiona ukijua curvature halafu ukaiona usione ni miujiza.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafikiri hawa watu wanaotengeza p9 camera watakuwa wanaufahamu ukweli huo unaoufahamu wewe kupitia camera yao?
Nani kaenda mwezini ,mwezi ni kama illuminary object ukiwa na p9 camera unauona kama kioo flani hivi au gololi ya transparent yenye rangi ya pale light grey...ngoja nikupe picha ya hawa jamaa wanavyotuactia

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatakaa akuelewe kwa sababu anaamini hadithi zilizotungwa huko uarabuni zaidi ya miaka 1000 iliyopita wakati dunia ikiwa bado katika lindi la ujinga.
Kuwa reasonable mbona nilichokuuliza kinaeleweka kabisa!

-Kama straight line inagusa a point katika cycle then imagine you are 100× smaller than that point. Unafikifi in your perspective utaweza tofautisha straight line from a cycle.?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hadithi maarufu ya vipofu na Tembo.
Kipofu mmoja aliyegusa sehemu za tumbo la tembo yule alielezea furaha yake na kusema jamani, “tembo kweli mkubwa, ni kama kichuguu pale alipolala”. Kwake kipofu huyu tembo alikuwa mkubwa kweli kama kichuguu.
Kipofu wa pili aligusa miguu ya tembo, akaipapasa na kuinyanyua. Huyu naye maelezo yake juu ya tembo alisema, “He he he, kumbe tembo mwenyewe ni kama kinu cha kutwangia”. Kipofu wa tatu yeye alifikia kupapasa sikio na kwa mshangao mkubwa akasema, “Masikini, hivi tembo tunayemsikia kumbe ni kama ungo wa kupepetea tu!” Vipofu wale wote hakuna aliyemwona tembo, bali kila mmoja alifanikiwa kumtambua kwa kupapasa au kushika sehemu fulani ya tembo na sehemu ile kwake kipofu yule ikawa ni picha na tafsiri yake ya tembo!

Sent using Jamii Forums mobile app
Poa.
 
Unashangaa watu kwenda mwezini na wakaonyesha video na picha

Sishangai watu kwenda mwezini sababu najua hakuna mwenye uwezo na wala hatokuwa na uwezo huo yoyote mpaka Kiyama kinasimama, ila nashangaa kwanini watu wanawadanganya watu.
ila haushangai Mtu aliweza kuupasua mwezi vipande viwili na ukarudi katika hali yake!

Nacheka sana, husemwa ukijua sababu ajabu huondoka. Tukio la kushuka kwa mwezi na kupasuka vipande viwili, ule ni muujiza na liliwezekana lile kwa uwezo wa Allah, baada ya wale walio kuwa wanampinga mtume,kumtaka awafanyie muujiza ili wapate kumuamini. Na mwezi ukashuka na ukapasuka na ukarudi katika hali yake ya kawaida.
Haushangai hadithi za bawa moja la nzi lina dawa hivyo akidumbukia kwenye maziwa kwa bawa moja umzamishe kabisa ndio unywe maziwa yako!

Sishangai sababu ile ni haki. Sio jambo la kinadharia na kubahatisha.
Hushangai hayo ambayo hayana ushahidi wowote! Kalaghabao.
Ushahidi wa jambo lililo pita unaupataje ? Au ushahidi kwako unatakiwa ukidhi vigezo gani ?

Wewe unaupataje ushahidi wa kuwa Isaac Newton alipata kuishi duniani au kina Aristoto, au Plato na wengine ?

Vipi au ulitaka na sisi tushuhudie nini hilo tukio? Sasa kufikiri kwa namna hii ni kufikiri kivivu na kiupofu bali ni kufikiri kitoto.

Sasa jifunze kujenga hoja kielimu sio kimhemko hemko.

Nipo ....
 
Hata ukipanda juu ya mlima kilimanjaro bado spherical horizon ipo acha ubishi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ok
images (26).jpeg
images (25).jpeg
images (24).jpeg
images (23).jpeg
images (22).jpeg
images (21).jpeg
images (20).jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndg yangu sisi tule tulale tufe, basi.

Ukitaka kujua faida ya huo uongo ni sisi kuufundishwa na kuuamini. hivyo yani.

Hivi kwenye maisha yetu ya kila siku, umbo la dunia linafaida au hasara gani hata kama tusingelijua lilivyo?

Tunaishi katika vita ya Nature na Sayansi ili tuione Nature si lolote na Mwanasayansi ndio mgu wa muhimu, na kadri tunavyozidi kuusapoti uongo wake ndivyo tunavyomrahisishia safari ya sisi kuwa watumwa wake.
Tuendapo itafikia mwanasayansi akitaka tusile kuku hakuna wakumbishia maana wote atakua anawatengeneza yeye. Leo hii kila msimu wa kilimo mbegu zakununua basi za asili zikiisha kabisa akitaka tufe njaa nani atampinga na mbegu zake hazizaliani.?

Kwahiyo kupitia uongo wa wanasayansi ni faida kwao katika kututawala wewe na mimi, jaribu kutafakari vingapi vinaendesha maisha yetu ya kila siku ambavyo vinatoka viwandani, vp siku wasipovizalisha tuna kipi cha asili kinachoweza kureplace.

Tunadanganywa tuamini kila kitu kinaweza kufanywa na mwanadamu lakini sio mimi na wewe ili watakaoweza wawe ndio watawala.

Na ngoja siku ifike itakua mwanasayansi akitaka kuja bongo ila pachafu, anazima internet hadi mpige deki barabara na mitaa, hapo utapata picha tulikua tunafundishwa kutawaliwa au kuishi kwa furaha.

ukitulia nakutafakari vizuri, utazijua faida za wanaotufundisha hizi elimu ambazo wana imani na uhakika asilimia zote mtu wa kuzi prove hatotokea..

Nihitimishe hivi....
Mimi katika hili la shape ya dunia nipo upande wa wanaoamini ni flat kwa sababu Naiona hivyo, jua na mwezi likipita juu katika zafari zake. Nadhafia ya mviringo inapingana na hisia za mwili wangu mimi kama mimi kupitia milango ya fahamu niliyonayo.

Na katika mengi niliyofundishwa kuhusiana na umbo la dunia mviringo nimeshindwa ku prove tofauti na ya dunia flat.




Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe kukiona kitu kiko hivyo haimaanishi kuwa ndiyo kilivyo wala kitendo cha wewe kushindwa kuthibitisha kuwa kitu kiko hivyo haimaanishi kuwa hakiko hivyo.

Wewe kupata hisia ya jambo fulani haimaanishi kuwa jambo hilo lipo ama ni la kweli. Pia, wewe kutopata hisia ya jambo fulani haimaanishi kuwa jambo hilo halipo ama ni uongo.

Unasema wanasayansi ni waongo, pengine naweza kukubaliana na hilo kwa namna fulani lakini wewe hujaweza kuthibitisha hilo katika hiki tunachokijadili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom