The Working Class, Savages in Suits

The Working Class, Savages in Suits

Kaniangusha hajaonesha resistance yoyote kama mtoto wa kisure

Kwa hio mtoto Wa kisure hana nyege au? Hujui Wa kisure kuna levels nako? Kilichokuuma Ronny tu kupokonywa tonge mdomoni. Hahaaaa! Mwenye kisu kikali ndo anakula nyama
 
Duuhh HOM mshenzi tuu, kanichosha hatari. Nimemmaind balaa mxiiiiiiuuu
 
Akawa anajoa ana mkosi tuu. Akapelekwa hospital, wakampima, dr akasema hana tatizo maybe ni uchovu tu. Akamuandikia dawa. Akawa anshinda home, kama mgonjwaaa, ila mgonjwa wa mawazo, akawa anawaza tu WHY? HOM kamfanyia vileee? WHY Bae Moro alimfanyia vileee? All she ever wanted was to be a good girl! Kwanini mikosi hamuishii? Why does she keep making more and more mistakes? Akawa analiaaa, analala. Na kazi ikawa ashaamua kuacha jumlaaaa! Ila ikawa badohajamwambia mama yake maana, akimwambia anaweza kuchanganya madawa afu ikaonekana kuna sinto fahamu.

Wa kwanza kuja alikuwa Mina na Joy, wakamwambia poleee, ungetuuliza,yule shetani binadamu hafai hata mbolea. Wewe sio wa kwanza aliwapost watu kibao ndo tabia yakee, he kiss and tells. Alishampost mpak Dada Asha, oraaaaa! Hawakuongea mwaka mzimaaa. Sema Ash mtu mzima kaamua tu kumpotezeaaa na kusahau. Ashawapost watu production, watu wa chemistry lab, wadada wa law, sales ndo balaa, Na victims wake wengi wanaachaga kazi, basi huo ndo ubabe wake. We rudi bwna achana nae, angalia maisha yako. Akawaambia mimi kurudi haiwezekani ila nawatakia kazi njemaaa. Mina akaaga aksema mimi Ustaadh atanipa talaka, ngoja nikawahi kupikaaa. Wakaondokaaa.

Hakwenda kazini siku 3, ya 4, chiffu akampigia kamjulia hali, akaanza kujielezea, " Niwie radhi mimi ndo nimesababisha yote haya, siku il ya kwanza kabisa tulivogogana nae kwnye corridor akaniita kando aliniambia amekubali ombi langu kwa mashari, ombi lenyewe ni kuwa nikikuchukua wewe kwenda kwenye bankers night, basi atasoma speech ya kampuni kwa niaba yangu. Nisipokuchukua wewe nikae mwenyewe nisomee speech yote, sasa mimi tamaa tamaa zangu i knew you could handle him, you looked bright and rich, and you had class nikajua hatokuzoa. Too bad it is what it is. Lakini rudi kazini, hizi skiu 3 nitazi over look, take it as compensation for my responsibility in everything. And do me one favor share zile picha, as hard as it can be please share zile pichaaa. My wife is sick really sick, na usipo share picha zile hali yake itakuwa sio nzuri. I am really sorry" Akamwambia picha nitashea, mpe pole mkeo, ila kazini mimi kurudi hapanaaa"

Akampigia Mina akamuuliza kwani mke wa chief anaumwa nini? Mina akamwambia figisu figisu zinadai ana shikwaga uchiziii! Khahaaaaaaaaa! Ndio ni mntal case, kama psychological issues kuna mda zinafyatukaga kabisaaa, anafungwa kambaaa na kufungiwa chumbani, wanazunguka kwa waganga weee, kuhangaika hospitali za vichaa hizi anapata nafuuu. Hivo hivo afya yake tia maji tia maji, na hio imepelekea chieff kuwa very anti social. Hataki watu wajue mambo yake, ila watu tunajua either way. Na mbaya zaidi wana watoto 2, mmoja tayari ashaonesha dalili zote na mental case, anahangaika kumtibia ulaya, India, kwa wataalamu hawa wakienyeji, could be family ya mkewe ina hio history ya mental problems, manake hata mama yake mkubwa wanavodai watu nae alikuwa chizi kabisaaa wa kuokota makopo mpaka alipofariki.

Ila second version inasema chieff ana mwanamke wa nje, ambae kamroga chiffu ni balaa, na anamroga mkewe leo kesho kutwaaa. Chieff akipunguza mapenzi tu bi mdogo anakoleza dawa huyu bi mkubwa vinapandaaa huku. Na ndo kamchezea mtoto mkubwa wa chieff sababu wakiume, kamuachia huyo wa kike. Kama kweli anamnyanyasa mwenzieee, mkewe mtu mzuri kweliii, nilimuona mara moja mstaarabu dada wa watu maisha haya nyieeee. Sasa chief maisha yakendo anashinda hospital, kwa waganga, inabidi awahi nyumbani kila sikuuu, maana mkewe anahitaji attention sanaaa, na ndugu yake anae muhudumia anachokaaa, so sometimes anakuwa mkali kwa mgonjwaaa, so chieff napenda kama mda unamruhusu akae nae mwenyewe maana ndo anaweza kumvumiliaaaa, afu ashamzoea maana kitambo anaumwa. Na vile yule mtoto mmoja ana matatizoo nae, ndo kabisaaa inabidi awepo nyumbani mnooo." Mmm Linda akachokaaa. Akapost zile picha za Bankers night akamtag chieff.

Ikawa wiki imepita hajaenda kazini wala hana nia ya kwenda, akaja dada Asha, akmwambia Mina alinielekezaaa, na Chieff kaniambia nijkuna kiruhusa nimemwomba, kunikubalia itategemea kama wewe utarudi kazini au vipi hahaaaa! Anyway na mwenyewe nilitaka nije nikupe vipande vyako. Sikia Linda, rudi kazini mdogo wangu, yule boya HOM unavojificha huku na kufa kimya kimya humkomoi chochoteeee. Ndo anazidi kupata sifaaa. Wewe rudi tumshughulike. Watu watasema watachokaaa, ila we angalia maisha yako. Kumkoa yule unarudi pale, unavaaa dress to kill, unakuwa juu hatariii, unamkomeshaaa kwenye kambi yake mwenyeweee. Isitoshe kawafanyia hivo watu wengi, wengi wamekufa kimyaa, it is about time someone should do something about it. Ndoaisha sawa, mimi alinipost nikamchunia mwaka mzima,baadae nikamjua mjingaa tu so nikampotezeaaa, sahivi nalichoraaa tu. We rudi jumatatu, tunakupendaa idara yetu lile pumbavu achana nalo, ngese lile.

Dada Asha akamwambia mimi nafeli ACCA kila siku, wananichekaaa, mimi yangu yananiendea, iko siku nitapata na mimi, sikati tamaa, wala simuogopi mtu. We rudi hana lolote la kukufanyaa. Ilakawa kamuelewa dada Asha uzuri tu. Akaamua jtatu anarudi kazini. Na harudi kama mnyongee, anarudi kama kubwa la wachawiii. Akaenda kusuka, nywele ndogo ndogo penseli, mikia mpaka makalioni. Akaenda kunyoa nyusi tenaaa, akanunua na make up, heels za maana. Akawa anaingoja jtatu kwa hamu. Jmosi hio usiku akaunganishwa group jipya la whats up, lina namba zote za watu wa ofisini kasoro mabosi na HOM wala Da Asha, Wala Chieff hawakuwepooo. Alieunda hilo group akapost pichaaa.

Mtu kibamiaaaa, ana kudud kidogo kweli na juu akai caption neno moja tu HOM! Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Watu wakawa wanaguna tuuu, na kuweka viemojiii vya mbioo. Mara wakaona H.O.M, COF, Dada Asha wame adiwa kwenye hio group. Wakaona H.O.M left this group. Hahahaaaa! Chezea kuwa exposed. Basi watu wako Linda mkomesheeeeee, tukomesheee shubhamit shenzi wahediii huooo! Watu anajiunga na namba zingine afu wana comment, namba za ofisni kimyaaa. Watu wakaanza kuchamba sasa na namba anonymous. COF aka comment alieanzisha hii group aifute mara mojaaa. Haikufutwaaa. Akakaaa, akasema Namba ya mtu nitayoikuta kwenye hii goup kazi hana keshooo. Wakaanza kutoa namba za ofisini zotee zikabaki anonymous zinaendelea kuchamba kama kawaida. Hahahaaaa! Linda akawa anajiuliza nani kaamua kumtetea akawa hana uhakika, akahisi atakuwa Dada Asha ndo ana balls zile.

Jumatatu kava kile kigauni kifupiii, na chupii tu, hills zake ndefuuu, katinga mjengoni. Kangoja saa 3 kila mtu anakuwa kakaa mezani kwake akanona ndo mda wa kuingia ili waongee vizuri sasa. Mlinzi mwenyewe akstukaaa, akamwambia za nyumbani, watoto hawajambo? Wakati hasalimiagi. Mlinzi yuko eeeh nzuri tu, hawajambo anashangaa mengi, kwanza hio gauni, pili alivopendezaa, tatu hio salamu, nne confidence alizokuja nazo. Mmmmmh akasema kazi ipo.

Akapita reception, akawa anapita taratibuuu, akaenda mpaka kwa HOM kwa secretary wake, akamwambia Mambo? Watoto hawajambo! Akabakia kabutwaaa! Bosi wako yupo? Akajibu yupo kwa kigugumizi, Linda akamwambia msalimie sanaaa. Watu wananyoosha shingo kutka kujua kama, zitapigwa au laaa. More than ever wakawa conviced alieanzisha ile group ni Linda.

Akapita mpaka kwenye kibox, akawaambia nimerudiii. Joy na Lina wakafurahi wakaita Daa Ashaaa! Akatoka akamuona, dada Asha yupo kaeleteni keki, tena Joy nenda marketing kaazime camera, wakamkaribishaa welcome back. Watu wengine wanashangaa, juzi group leo karudi, mara party sio mnyonge wakasema kweli huyu ni kiboko ya HOM. Mtu akapost kwenye group, HOM aingia chini ya meza baada ya kumsikia Linda mlangoni kwake! Hahahahaa! Watu wakwa wana comment Kibamia kimepata mlenda safari hii kwisha habari yakeeeee.


Akipita mule ndani, watu wote mambo Linda, za kwako, sasa akawa popular ofisi nzima inamjuaaa. HOM akachukua leave kwanza si kwa kashfa ile ya kibamiaa, akajipange upyaaa. Ila Ronny akawa anamkwepaa flani hivi. Na yeye given she is guilty as charged akawa muelewa tu, japo roho ilimuuma ki design. Siku hio kama siku 4 zimepita tangu arudi, Ronny akaja akamwambia huendi lunch! Akabaki anamtazama tu, si kwa mambo yote yaliopitaa. Akmwambia twende lunch, wakaenda kwa ukimya mkubwaaa, hamna anaeongeaa. Mara Ronny akaanzisha tu story zingine kabisa. Linda akaona this is bullshit it is better aombe tu msamaha you know huenda akaelewekaa.

Aaanza najua uliniambia nisiende, akamwambia shhhhhhhhhhhhhhhhh! For me you are still the Linda imet in the corridors, the other things i dont know, i dont want to kno, i just convince myself it never happened and i like it to remain that way. Tuongee tu mambo mengineee. Every body have their own ghosts. Let us pick up where we left! Linda akawa kashangaaa tu, hana la kusemaa ukizingatia na yeye mkosefuuu akasema poa. Basi wakawa mpaka wanachekaaa kabisaaa. Akapata amani ya roho.

Siku hio Joyceline akamwambia nina maongezi na wewe, wakawa wamekaa sehemu akamwambia mimi nataka unisindikiz nikapime ngomaa! Tobaaaaaaaaaaaaaaaa! We mwana wewe? Akamuuliza siko linakuuma unahisi ngoma ya sikio ina tatizo Akamwambia nataka nikapime UKIMWI. Mmmmh! Akasema why? Kwanini unajitabiria mambo mabayaaa? Joy akamwambia mimi pia nina tukio langu, lilinikuta hapa hapa ofisniii! Ngoja nikwambie unishauriii.

Akasema alivoanza kazi hapo, akakutana na mkaka, waka click instantly, wakaanza kudate, yaani walishibana hatariiii. Basi wakawa wana date mda tuu wanapigana mechi kavu kavuuu, yaani walipendanaa. Mda wote kama kumbi kumbiii. Akamtambulisha mpaka kwa ndugu zake huyo kaka, akawa anawajua na wao wanamjuaaa kabisaaa.

Sasa siku moja alienda mitaa ya kwao akawa kaenda saloon ya jirani akitaka aoshe ndo arudi kwao, maana mda ulikuwa umeenda angekuta huku saloon zimefungwa. Akaingia kuoshaa. Yule mdada wa saluni akamwambia nakuonaga unapitaga na Walter, ni nani yako? Akaamua tu kumdanganya rafiki yangu, family frinds kwani vipi? Akamwambia uwe nae makini, yule ni muathirika wa HIV. Roho ikafanya paaaaaaahhhhh! Dada wa saluni anamwambia alizaliwa nao huo UKIMWI, anasihi kwa dawa,masikini tulijua kitakufa kidogo bt Mungu mkubwa kakua mashallah! Wazazi wake wote tulisha wazika na huo huo UKIMWI, baba yake alikuwa mjedaa, mama yake ticha, mjeda ndo alimuua mkewe. Wlater anakunywa dawaaa

Wlikuwa hawajamwambia mpaka mkubwa form 6 ndo wamemwambia ukweli. Anajua pale alipo kama anakunywa dawa, uwe makinimdogo wangu. Akaona yatoshaa, akamwambia dada kwani shingi ngapi, na maji yake kichwanii. Yule dada akamwambia nenda tuu mwaya nimekusamehe. Akabaikia anatikisa kichwa, na kusema Walter knyoko keshamuambukiza mtoto wa watu. Akakaa siki 3 anawazaa tu, kazini hakujaaa. Siku ya 4 Wlater akaenda kumuona, akamuuliz, nasikia unamwa UKIMWI. Wlaeakajibu NDIO KWELI NAUMWA. Tobaaaaaaaaaaaa! Nilizaliwa nao, so sio kosa langu. Akamuuliza mbona hukuniambia?Akamjibu tu ningekwambia usingenikubaliaaa, na mimi nakupendaa, think about me, nimezaliwa hiviii, and it is my life, sorry lakini i dont know. Akamwambia Wlater tokaaa.

Basi ikawa kamuchaa, baadae akaanza kuumwa na kazi kaacha hajui alipo. Ila yeye kama yeye kajikusanya kaona sasa yupo tayari akapime UKIMWI huenda ikawa hanaaa, ila kwa jinsi walivopiga mechi kavu hajuiii, Mungu atie mkono wake. Ndo anamuomba amsindikizee hana nguvu za kwenda mwenyewe. Linda akasema nitakupeleka, mwnyewe nataka kupima HOM sio mtu mzuri na kuna sehemu nilipita sio nzuri pia basi tungoje 3 months tukapime woteee.

Ronny huku akaongeza kasi sasa anataka relationship hata kesi yake haijapoaaa. Ikawa anashikwa na kigugumizi.

ITAENDELEA KESHO SAA 7 MCHANA
 
so sawa kabisa toka moyoni mpaka kesho sa 7 mchana dah sa ntafanyaje sa kama ndo umeamua na haki miliki zote unazo wewe

kubwaaaaaa la maaaaduiiiiii we ni shiiiiidaaaaah
 
so sawa kabisa toka moyoni mpaka kesho sa 7 mchana dah sa ntafanyaje sa kama ndo umeamua na haki miliki zote unazo wewe

kubwaaaaaa la maaaaduiiiiii we ni shiiiiidaaaaah

Si unajua mwenzio nauguzaa, mgonjwa mwenyewe wa kuogeshaa, kulishaaa, kuandaa chakulaa. Ukubwa jalala. Nikiweza mapema ya hapo nitawaletea muendelezo.
 
Haya mambo ya kuvamia watu, unaweza kujipima na tapemesha mpk unakata kamba, ooohhh
 
hiyo ofisi hiyo.... mpaka sasa nimesikia Linda kaingiza voucher tu..,
 
Huyo HOM naye, wanaume wengine sijui wakoje, bora wamemkomesha na kinanii chake. So immature and inhuman, mtu mwenye roho ndogo si ndo kazi angeacha kama sio na kujinyonga juu. Mungu atusaidie tusije dondokea mikononi mwa predators kama HOM.
 
Back
Top Bottom