The beggining of the game!
Akamjibu okay! Chieff akamwambia tu wear something shorter and sexier! Akaguna rohoniiii. Akawa anashuka kurudi kwenye kibox chao, njiani akamkutaaa mkaka wa kawaida tu, akamsalimia, Mambo! Akamjibu poaaaa. The guy was a little chatty,akajitambulisha mi naitwa Ronny, sijui wewe unaitwa nani? Akamjibu Linda, im new here, Finance intern.
Ronny akajiongeza, new huh! Karibuuu, karibu sanaaaa, so uko huku kwa chieff au kwa dada Asha? Akasema kwa dada Asha, Ronny akashusha pumzi. Linda akamuuliza kwani Chieff ana nini akamwambia tu You will find out! Nice to meet you Linda, i will keep in touch.
Kufika kule akaanza kuongea na shosti wake wa asubuhi, akamwambia how is head of marketing? Akastukaaaa! Akawaambia wenzie anamuulizia head of marketing, wakaacha kazi wote na kumsikilizaaa. Akawaambiawa you just came in like TODAY and you already asking for HOM! You my dear are something else.
Akawatoa shaka no, it is just nimegongana nae nikiwa na chieff akanioffer postion in marketing, so i just wanted to know. Wakashangaaa! He offered you that position? I applied it too. Me too, me too. Hadi shosti jirani yake akasema me too. Wale wengine wakanunaaaaa. Shosti amabe akaja kumwambia anaitwa Amina, ila ajiita Mina kimjini mjini akamuomba namba yake akamtex wote wamekaa pale pale, usingesema shostiii, ushanunua uadui. Linda akawa kashangaaa.
Mmoja wao ambae ndo mzuriii, na kiranga aliempa kazi asubuhi Joyceline, akaanza ubuyu, jamani nani anaenda na chief hio jmosi kwenye bankers night? Mmmmmh! Wakawa wanagunaa, mmoja kasema labda Dada Asha, Mkaka Jose akadakia dada Asha ashakuwa mbuzi mzee, hahaaaaaaa! Wakacheka bora hata aniambie mimi Jose nimsindikize mwanaume mwenzie tuongee hata mipira au nimpe mbinu mpya za kupigana miti! Loooh! Wakachekaa.
Danny nae wa hapo hapo akadakia ataenda na hawa hawa warembo wetu wa 3, Joyceline, Mina na Linda. Sasa Mina muke ya ustaandh atampa nani ruhusa so hapo either Joyceline au Linda, kule juu kwa chieff wote mbuzi wazee hawafai kwa kuchoma wala kukaanga wao supu tu, labdaaa! Hahahaaaaa! Wakacheka. Linda akadakia kaniomba mimi nimsindikizeee! Wote wakatoa mijichoo na kinyamaza kimyaaaaa, hamna alietia neno. Joyceline akawa katoka kimya kimya.
Mina akamtumia sms usingesemaa, at the rate you are going utakuwa huna shostiii wala mshkaji humu. Akaona kizungu zungu. Luncha wakaitana wale wa kaka na Joyceline wakawa wanamwambia Joyceline tupeleke Tanzanite Suits, biriani yao ni kibokooo kabisaa afu 6000 tu, hapo mtaa wa libya biriani ya kihindi balaa sanaa. Joyceline akasema kama mnanilipia sawa, wako gari lako tena tusikulipie twende bwana. Linda akawaomba na mimi tuongozane, Joyceline akadakia gari haitoshiiiiii. Wale wakaka wakabakia kimya chezea lift nyie.
Akabakia na Mina, Mina akatoa kiporo chake kaenda kukipasha na kuanza kula. Akawa anamwambia hapa kazini sio watu wote wazuriii. Akatoka dada Asha we ushamtibu Joy kakunyima lift? Hahaaaa! Tungeongozana lakini nina mambo yangu mengiiii. Poleeee. Akamwambia Minaaa viporo vitaota tumboniii, ubahili gani huooo? Ustaadh bado hajata kazi baada ya kuikataa ile ya TBL. Mina akamjibu hajapata dada Asha mfanyie mpangooo. Dada Asha yupo we mtu kakataa kazi ya TBL kisa wanauza bia tu, eti dini haitaki basi akafundishe madrassa. Utakula viporo mdogo wangu mpaka viote tumboni usiwajambie tu wenzio hapo! Hahahaaaaaaa! Akatoka zake.
Mina ndo akawa anamwambia Linda ujue mimi mume wangu hana kazi, afu nina katoto ka 4 years, afu bado niko tempo, nisipoishi kwa akili tutarudi kijijini. Hii hela ndo itutoshe woote hivooo. Ndo maana nakija na kiporo changu napasha naokoa gharama. Linda akamuuliza jamani katoto kako kakike au ka kiume, akamwambia cha kiume, alhamdulillah. Akawa kakaa pale njaa inamuuma si kidogo.
Akaja Ronny, twende lunch! Ikabidi tu akubali, akajua Ronny ana gari, kufika nje akaita bajaji, ikawa ashamshusha maxiii, Ila wakaenda kula akamlipia hiko chakula. !da wa kutoka akawa anaenda kwenye hiace akakutana na Ronny njiani wakaongozana kufika kituoni story story kila mtu akapanda daldala yake.
Akawa kaenda kwa mama yake mdogo ndo anapofikiaga huku Dar. Basi akawapigia simu kwao wamletee vitu vyake. Basi akamsimulia mama yake jinsi alivoachwa lunch, mama yake akasema kiruuuuu, ya nini uteseke, chukua Nissan Extrail yanguu, mi nitapanda Hyundi ya mzee wetu hapa, nitampa mambo mpaka akununulie hata Corolla. Hahahaaa! Akamwambia kesho nitamtuma Deo akuletee hivo vitu na gari kabisaaa.
Kafika kazini, asubuhi, dada Asha akampangia kazi, wakawa wamekaa kwenye vibox vyao, mchana Deo akampigia gari iko chini pale akachukue funguo. Akafurahiii. Mda wa lunch saa 6, akamwambia Mina twendee tukale, nakupa ofa. Mina kamjibu shoga sehemu za kula hapa mbaliii. Linda akamjibu usiwe na wasiwasi nina gari. Joyceline akastukaaa. Mina akasema haya ngoja nije mie.
Wakawa wameenda akmuuliza Ronny yupo ofisi gani akamwambia yupo customer service, akmwambia tumpitie, basi Ronny hakuwa ready ila akakubali tu, kufika chini Ronny anataka kuita bajaji, akamwambia Noooo nina gari njooni. Kufika Zilikuwa zimebakia gari 2, mwisho wa parking Carina zee na Nissan. Ronny kujitia kidumee akawa kaenda kusimama kwenye Carina, akamwambia noo ni hii huku. Wakaingia kimya kimya. Wanayoka huku wanamuona Joyceline kwenye vitz yake anatoa sijui kitu gani wakampita haooo.
Mina akasema hana lolote yulee kaja tu kuchungulia umekuja na gari gani! Loooh! Na limemshukaaa. Ronny anacheka tu, manake huwezi kuchangia mambo ya wanawake. Kufika kule, wakala Ronny akalipaaa tenaa. Wakawa wamerudi ofisiniik.
Basi Joyceline kabadilikaaa si kidogooo. Anaongea kwa mbwembwe zoote, Utadhani si yeye aliemchunia juzi. Kila kitu Linda, there is this party you wanna come, kuna sehemu wananyoa nyusi vizurii nitakupeleka this weekend. Mina anamkanyaga huku chini. Linda akamwambia sawaaa. Akaja dada Asha nasikia kuna intern ana Nissan XTrail, Mbona mtatuchana misambaaa wazee wa humuuu na gari zenu za wazazi wenuuu! Looohhhh! Mchukuage vi corolla jamani. Huyo bosi wa huyo intern analo! Akaingia ndani.
Mina akamtex Linda joy sasa hivu ataenda kumwambia dada Asha, alivo na wivu sasa, balaa. Ila joy hakwenda instead akaanza kumponda dada Asha, wivu utamuua, ndo maana anafeli kila siku. Mbuzi mzee. Wakachelaa. Wanaume hawakielewa huu muungano wa tz na zanzibar wa ghafla ghafla umetokana na nini.
Jinoni dada Asha akatoka nje akamwambia Linda njoo, akamwambia unaitwa na head of marketing. Fanya ukamsikize. Akasema sawa boss.
Kufika kule akawa anasikia kuna mtu anafokewa balaa, kama mtoto mdogo. Baadae akatoka Ronny, wakaangalina, na HOM alikuwa nyuma, Ronny akapitiliza akaingia Linda.
ITAENDELEA SAA 1 USIKU AFTER SIMBA NA YANGU, yolooooooooo!