Usiwaze sana mwanakwetu EDWARD hana kufikiri ila akiamua kusema leo hii jinsi bosi wake alivyo leta richmond na mambo kina 6 na mawembe waliyo mfanyia basi hata wewe utampatia kura yako tusubiri wakati ukuta ata yazungumza yote hayo.
Nachelea kuamini Lowassa kuwa mgombea 2015, na pia kuwa
Rais, okay yawezekana wanaosema haya wanajua zaidi ama wana
data zaidi kuliko, lakini Watanzania ni wepesi kuamini kitu bila
hata kufanyia uchunguzi ama kuumiza kichwa kidogo kisa tu,
labda ameambiwa na mtu kutoka Ikulu au cjui babake ni kigogo huko TISS.
Okay mnataka niamini Lowassa anahodhi hisa 75% huko TISS, kimahesabu
maana yake hyo TISS ni ya kwake, swali langu ni dogo tu..
Kuna mtu amgeamini kama Lowassa angefika mpaka kujiuzulu
kwa ushawishi huo alio kuwa nao huko TISS bila kuzuia hyo
saga???? Ni vigumu kuamini lakini najua wenye data zaidi yangu
watakuwa na jibu la hili kama kawaida yao! Au jamaa alipata hzo hisa
baada ya kujiuzulu?????
Tatizo la nchi hii sio mtu ni mfumo ndio unaotutesa, lakini
mfumo huu umewekwa na watu hao hao, sasa tunahitaji mtu mpya
atakayerekibisha hii mifumo dhalimu na kukaa kwenye mstari.
Nakiri kwamba ni vigumu kumpata huyo mtu katika mazingira haya
lakini ukweli ni kwamba watu makini wapo japo ni wachache.
Taifa letu limekos mustakabali, kuna watu wachache ndio
wanatuchagulia Rais na hii inatokana ya kuwa watu wengi
ni wajinga na walioenda shule wanafanya mambo kwa maslahi
yao, lakini muda unakwenda mambo yanazidi kubadilika.
Sisi ni wanafiki na ndio maana, mabadiliko yanatukimbia...
Kitendo cha kukiri tu kwamba jamaa anaikamata TISS tayari
ni kukubali unyonge, yaani hyo stori imekuwa kama nyimbo
yaani kila sehemu inapigwa watu hatuna reaction nayo bali tunaona
ndio sawa, mabadiliko ya kweli huanzia kwenye nafsi na sio laxima kwenda
barabarani.
Tunapenda changes, lakini fikra zetu bado si changamfu.