The SGR War: Wakati Kenya wakisuasua, Uganda wameamua kujenga SGR. Hii ni fursa kwa SGR ya Tanzania. Is it viable? Tuichangamkie?

Mkuu!! Ukiweza kujiaajiri utakuwa na maisha ya Raha Sana aisee
 
Mkuu victor mboro, the best way kupanda Mlima Kilimanjaro inayopendwa sana na watalii ni route ya Marangu, kuanzia Marangu National Park. Kenya walipanga kujenga uwanja Taveta, kutoka Taveta hadi Marangu national park ni 20 KM, just 30 min drive, wakati kutoka KIA to Marangu ni 80km, 2hrs drive, hivyo Kenya wakijenga uwanja Taveta, watalii wa Marangu route watapitia Kenya. Japo route ya Machame ni fupi, kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia Machame ni 7 days wakati Marangu ni 6 days kutokana na vilima vikali kuliko Marangu.
P
 
Aliandika PseudoDar186


Nimepitia takwimu kutoka the National Bureau of Statistics (NBS) na Tanzania Ports Authority (TPA) kuhusu mizigo / shehena yanayopitia bandari za Tanzania kwenda au kutoka nchi za jirani.

Kwa mwaka 2017/18, jumla ya tani 5.6 million zilipitia Tanzania (bandari ya Dar es Salaam pekee) kwenda au kutoka nchi za jirani, ikilinganishwa na tani 4.8 million mwaka 2016/17. Hili ni ongezeko la asilimia 17.1 na ni habari njema kabisa kwa TPA na nchi yetu kwa ujumla.

Ukiangalia mchanganuo wa shehena zinazoenda au kutoka nchi za jirani, asilima 61.1% ni za Zambia (36.6%) na J.D. Kongo (24.4%). Hii ni zaidi ya tani 3.4 million ambazo kwa asilimia kubwa zinawafikia jirani zetu kupitia barabara zetu hapa Tanzania. Ukipitia takwimu za 2017/18, TAZARA imefanikiwa kusafirisha mizigo ya tani 187,558 tu (3.4% ya 5.6 million) kwa njia ya reli.

Shehena za Rwanda ni asilimia 16.5% pekee (au tani 922,134) kwa mwaka wa 2017/18. Ukilinganisha na 2016/17, kuna upungufu wa 9.0% - kitu ambacho kinaashiria kuwa mizigo ya Rwanda inawezekana kuwa inapitia Kenya na Uganda.

Kwa kutumia akili za kawaida (common sense), kuna haja ya kuwekeza reli ya SGR kuunganisha Tanzania na Zambia na J.D. Kongo kwa sababu business case (volume of cargo) ni kubwa mno (kwa mara 3.7) kuliko Rwanda. Pia, tukiweza kuondoa hata tani 2 million barabani, TANROADS watapumua kidogo na matengenezo ya kila mara yanayotokana na uharibifu wa baraba zetu. Hii ni kwa mujibu ya data za NBS na TPA wenyewe.

Naomba mwenye taarifa kuhusu ya haya maamuzi ya kupeleka SGR Rwanda atujulishe
 
Hili kabila limejaa watu wa hovyo sn, Jiwe, Paschal, Mnyeti, Makonda n.k sijui kwanini?
 
Mkuu Paskali,
Mseven anakenga SGR sio kwenda port bell ambapo kuna port toka Mwanza;
Anajenga reli kwenda Malaba ambako ni mpakani na Kenya;

On the other hand labda tujiulize Kenya SGR yao, unawapatia/inaleta nini kwa Kenya.

Ukisoma vyanzo mbalimbali ambavyo ndicho kinaendelea kwenye akili zetu; Kenya wana import zaidi bidhaa toka nje ya nchi kuliko wanavyo export.

Je na sisi SGR ikikamilika itakuwaje, tuta import zaidi au tutaitumia ku-export zaidi; kiuchumi ni faida (trade surplus) kuliko kuwa na hasara (trade deficit).
Nchi hizi zetu ikiwamo Congo, Burundi, Rwanda, Uganda, Malawi na Zambia zina import nini?
Dawa za mswaki
Miswaki
Mopers
Mifagio (soft brooms)
Toothpick
Penseli
Kalamu za kuandikia
Pedi za wanawake
Toilet paper
Cornflakes
Superghet
Nyama za makopo
Samaki za makopo
Vitunguu swaumu
Fanicha zilizotengenezwa kwa unga/vumbi la mbao;

Sasa hata lini tutajivunia kupitisha containers zenye vitu hivi na kupata tozo bandarini/kwenye SGR;

Kuna rocket sayansi kutengeneza chupi za kiume na handkerchief?

Hapa ndipo dhana ya kujenga viwanda inakuja na hata mjerumani alijenga reli ya kwanza yeye Ujerumani a-import raw materials kwa ajili ya viwanda vya Ujerumani na sio vinginevyo.

Reli ni kama mishipa ya damu, uzalishaji wa ndani una tija zaidi ku-cut down imports ya vitu basic kama nyama za kopo au samaki wa kopo?

Tusitumie sana model za World bank, baadhi kama sio nyingi zina tu-mislead.

Tutafute Japanese economic miracle
Malaysian economic miracle
Wote hawa waliona faida ya kukuza uchumi baada ya kuwa na surplus kwenye manufacturing kwa kutumia raw material toka ndani au nje ya kuonegeza export.

Tunapojenga SGR macho yetu yawe focused on prize; lazima tuwe na right model ya PPP; otherwise JPM ataondoka then tutabaki tunashangaa huyo anaekuja nae aje na vipaumbele vyake.
 
Ni jambo jema!

Lakini sidhani kama tuna mashindano na Kenya mkuu Pascal!
Sahihi. Lengo kubwa siyo kushindana ila ushindani hauepukiki. Mimi hupenda kuitazama hii 'vita' ya SGR kwa muktadha wa maendeleo ya viwanda kuliko biashara ya uchukuzi. Na hapa ndipo kwenye manufaa makubwa zaidi ya vile wanavyodhani watu. Mtandao wetu wa reli ya kisasa ukiwafikia majirani wengi kwa ufanisi mkubwa kuliko ule wa Kenya maana yake bidhaa zetu zitakuwa na competitive advantage dhidi ya zile za Kenya.

Tuwatazame hawa majirani kama masoko ya bidhaa zetu kuliko kama wateja wa huduma ya uchukuzi.
 
Kwa hiyo hiyo ndiyo sababu inayoifanya chadema isiwe na angalau kiwanja tu 🤔😅😅
 
mada nzuri , inahitajika time frame ya kukamilisha miradi kama hii yenye tija kubwa. siku SGR ikifika Mwanza na Kigoma ni siku ya kihistoria kwa bongo! penye nia pana njia! wakope kokote kiasi chochote reli iishe pesa itarudi tu! hata wajukuu wakilipa si tatizo! vitu viwili tu hupaisha uchumi wa nchi reli ya umeme na umeme wa bei rahisi na wa kutosha!
 
Tanzania hawapeleki SGR Rwanda, bali Rwanda wanaunganisha SGR yao mpakani mwa Tanzania na Rwanda ambapo wamepata mkopo kutoka AfDB.

AfDB wanafadhili miradi ya kimkakati nchini Tanzania. SGR yetu ni kuwezesha usafiri wa haraka na wa chini zaidi kwa abiria/bidhaa kutoka mikoa ya Mwanza, Kigoma, Geita, Tabora na mikoa yote ambayo inapita nk. Sio lazima upande ndege ili usafiri kwa haraka zaidi, SGR itachangia uchumi wa Tanzania kwa ujumla na kupunguza uharibifu wa barabara pamoja na ajali. In a long run its cheaper to have SGR.

Zambia tayari ipo reli ni swala la kuiimarisha na kuifanya ifanye kazi kwa faida zaidi. Tanzania tulichelewa sana inabidi tukimbie.
 
Wanabodi, Tanzania ni nchi yetu sote, viongozi wetu wana wajibu wa kutusikiliza sisi wananchi wao tunasema nini na kushauri nini, kama ushauri wetu ni mzuri, wauzingatie, kama ni ushauri wa hovyo, wau puuzie.

Ushauri huu ulitolewa miaka 3 iliyopita, ulipuuzwa!. Leo Spika kaenda China, akaonyeshwa na Wachina umuhimu wa bandari ya Bagamoyo, sasa ndio leo, Spika wetu anaongea Bungeni!.

Yaani kuna vitu wakishauri kina yakhe, vina puuziwa, lakini akishauri mchina, ndio Spika anaelewa!.
P
 
Kiukweli kabisa, huyu mtu aliyeifanya kazi hii, akitokea kuja kuchaguliwa kuwa Mwakilishi wa Tanzania ndani ya EALA, you can just imagine atafanya nini!. Kama amaweza kufanya yote haya akiwa just a journalist, akitokea akawa mbumbe wa kitu kama EALA, si Tanzania itapaa?. Au mnasemaje wanabodi?.
P
 
Kwenye mambo ya SGR, Watanzania tunapaswa kuambiwa ukweli wa kila kitu!, serikali yetu lazima iwe very transparent see through kwenye kila kitu including mikataba na financial maters kufuatia kuwahi kupigwa huko nyuma kwenye rada, kwenye ndege, kwenye meli na sasa kwenye reli
Maswali haya yajibiwe kikamilifu
Maswali haya yanahitaji majibu ya kina na sio blah blah!.
Kama mtu kuuliza maswali kama haya, kutapelekea kuhojiwa uzalendo wake, mimi naomba kutumia kinga ya kihabari na kanuni ya kwanza ya mwandishi wa habari no seek the truth, and write nothing but the truth!, kuna kitu ninadhamiria sio tuu kuandika bali kukitengenezea a video documentary ya safari ya SGR ya Tanzania, tulipotoka, tulipo na tunapokwenda, ili huko mbele, likija kujitokeza liji white elephant fulani hivi ambalo sijui kama ni mimi tuu naliona, angalau dhamira yangu isinisute, niliona kabla, nikasema kabla, nikaandaa documentary kabla, nikaonyesha kabla, ili angalau jamii ya Watanzania wajue kuna watu waliona kabla na walisema kabla!.

Na labda kuwasaidia Watanzania wenzangu wasio jua, kwenye ile kashfa ya rada, BAE walikiri kutoa mlungula wa kickbacks, lakini sheria yao inawaruhusu non disclosure ya waliowapa mlungula, ilo usipoteze wateja wapya wapenda mlungula, kibiashara mlungula wa 10% ni halali!, ila ikijulikana kuwa umetoa mlungula, unapaswa ama uwataje uliowapa mlungungula, wakamuliwe wautapike huo mlingula, ama uwahifadhi usiwataje, na badala yake utozwe faini kwa uliowapa mlungula, na kuurejesha ule mlungula, na hicho ndicho kilichofanywa na BAE, kuwahifadhi waliowapa mlungula, na badala yake ikakubali kulipa faini na ndipo tukarejeshewa ile chenji ya rada.

Hii maana yake, kuna viongozi wetu walikula mlungula BAE akawakingia kifua kuwahifadhi kwa kulipia faini na ule mlungula ukarudishwa nchini kama chenji ya rada, endapo BAE wasinge wakingia kifua kuwahifadhi na kuwalinda, amini usiamini, hayo majina ya waliopokea mlungula na kuzihifadhi fedha zao kule Credit Suisse, yangetoka, Watanzania msinge amini macho na masikio yenu!.

Kashfa hii iliobuka kwasababu tuu kulitokea lijinga limoja, mgao wake yeye ukauhifadhi visiwa fulani ambavyo viko chini ya milki ya Uingereza, ndipo Muingereza akabaini, lakini kama wote wange bank Swiss banks, kule fedha zao ni very secure, hata bank manager, hajui majina ya customers na clients ni secret codes tuu zinatembea, hivyo wala kashfa ya rada isinge ibuka!.

Hivyo watu tunaoulizia kuhusu haya mabenewa, naomba mtuelewe ni wazalendo wa kweli wa nchi hii!.

Paskali
 
Mambo mengi Magufuli alifanya lakini alitanguliza masilahi yake kwanza. Imagine ule mkataba wa SGR ya Mwanza - Isaka kupitia Chato aliosaini Desemba 2020 ulikuwa na maana gani?

Kumbuka kipande cha Makutopora- Tabora kilikuwa bado by then.

There is no way SGR ikawa na tija. Itbakia white elephant forever
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…