The royal tour kupaisha utalii na uchumi wetu wa Tanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,895
940
THE ROYAL TOUR KUPAISHA UTALII NA UCHUMI WETU WA TANZANIA

Heko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuongoza na kurekodi kipindi Maalum cha The Royal Tour kuonyesha vivutio vyetu vya utalii,utamaduni wetu pamoja na vivutio vya Uchumi katika Taifa letu.

Kipindi hiki kinayo manufaa makubwa sana kwa Nchi yetu na Wananchi kwa ujumla na yafuatayo ni baadhi ya Manufaa au Faida ya ziara hii;

(1)Kuitangaza Nchi yetu pamoja na Vivutio vyake ,Filamu hii inayorekodiwa na Mhe Rais akiwa kama Muongoza watalii Mkuu itazinduliwa Marekani na kuonyeshwa kwenye mabara yote ya Dunia ikiwemo Ulaya ,Asia ,America na Afrika lakini pia kitaonyeshwa kwenye Safari zote za Ndege kwa mashirika ya Ndege Duniani kwa hakika italeta Watalii wengi na Nchi Kufahamika na kunufaika .

(2) Kuvutia uwekezaji Nchini , The Royal Tour itavutia makampuni Mbalimbali yanayohusika na Utalii na yenye wateja wengi kuja kuwekeza Nchini lakini pia uwekezaji kwenye sekta nyengine za Uchumi Kama Madini ,Uvuvi pamoja na Kilimo hii ni kutokana na Tour hii inalenga kutangaza Vivutio vya Uchumi pia hii itaongeza mapato na Ajira kwetu Watanzania .

(3) The Royal Tour inaenda Kulinda Rasilimali zetu, kama mnavyofahamu kumekuwa na propaganda kwa baadhi ya Majirani zetu kujimilikisha vivutio vyetu na kujitangaza kuwa ni vyakwao suluhisho la propaganda hizo ni The Royal Tour ya Mama Samia ,Filamu hii inaenda kufuta uongo wote na kuonyesha uhalisia wa Mambo kwamba Mlima Kilimanjaro upo Tanzania lakini pia kulinda Rasilimali zetu ikiwemo Madini hasa ya Tanzanite na hivyo kunufaika na vyakwetu .

(4) Kipindi hiki Maalum kinalenga kutangaza Utamaduni wetu watanzania katika Mabara na Mataifa mbalimbali Duniani na hii itaongeza utalii hasa wa kitamaduni kwani Utamaduni ni moja ya Vivutio vya Utalii .

Haya ni machache na baadhi ya mafanikio makubwa tutakayoyapata Muda sio mrefu kwani Mhe Rais anataka kufungua fursa kwa watanzania lakini pia adhma yake ni kuona kuwa Watanzania wananufaika na Rasilimali zao, na ikumbukwe Tanzania ni ya pili Duniani kwa kuwa na vivutio vingi tena vya asili sasa ni muda wa kuvitumia kwa manufaa ya Watanzania na hiki ndicho anachofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan .

Kwa Hakika kipindi hiki cha The Royal Tour ni moja ya uwekezaji Mkubwa sana kwenye sekta ya Utalii kwani Filamu hii itatazamwa vizazi na vizazi na kuitambulisha Tanzania Duniani .

#TwendePamoja
#KwaMatokeoYaHaraka
#KaziIendelee

IMG-20210906-WA0043.jpg
 
Ni wazo zuri,Watafute watu walobobea Ili ivutie na wasije kua wamekurupuka.

Pia bajeti yake iwekwe wazi Zaid maana hapo kuna msafara wa Rais hivyo cost yake tu ukiachana na filamu ni kubwaa
 
Heko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuongoza na kurekodi kipindi Maalum cha The Royal Tour kuonyesha vivutio vyetu vya utalii,utamaduni wetu pamoja na vivutio vya Uchumi katika Taifa letu.

Kipindi hiki kinayo manufaa makubwa sana kwa Nchi yetu na Wananchi kwa ujumla na yafuatayo ni baadhi ya Manufaa au Faida ya ziara hii ,

(1)Kuitangaza Nchi yetu pamoja na Vivutio vyake ,Filamu hii inayorekodiwa na Mhe Rais akiwa kama Muongoza watalii Mkuu itazinduliwa Marekani na kuonyeshwa kwenye mabara yote ya Dunia ikiwemo Ulaya ,Asia ,America na Afrika lakini pia kitaonyeshwa kwenye Safari zote za Ndege kwa mashirika ya Ndege Duniani kwa hakika italeta Watalii wengi na Nchi Kufahamika na kunufaika .

(2) Kuvutia uwekezaji Nchini , The Royal Tour itavutia makampuni Mbalimbali yanayohusika na Utalii na yenye wateja wengi kuja kuwekeza Nchini lakini pia uwekezaji kwenye sekta nyengine za Uchumi Kama Madini ,Uvuvi pamoja na Kilimo hii ni kutokana na Tour hii inalenga kutangaza Vivutio vya Uchumi pia hii itaongeza mapato na Ajira kwetu Watanzania .

(3) The Royal Tour inaenda Kulinda Rasilimali zetu, kama mnavyofahamu kumekuwa na propaganda kwa baadhi ya Majirani zetu kujimilikisha vivutio vyetu na kujitangaza kuwa ni vyakwao suluhisho la propaganda hizo ni The Royal Tour ya Mama Samia ,Filamu hii inaenda kufuta uongo wote na kuonyesha uhalisia wa Mambo kwamba Mlima Kilimanjaro upo Tanzania lakini pia kulinda Rasilimali zetu ikiwemo Madini hasa ya Tanzanite na hivyo kunufaika na vyakwetu .

(4) Kipindi hiki Maalum kinalenga kutangaza Utamaduni wetu watanzania katika Mabara na Mataifa mbalimbali Duniani na hii itaongeza utalii hasa wa kitamaduni kwani Utamaduni ni moja ya Vivutio vya Utalii .

Haya ni machache na baadhi ya mafanikio makubwa tutakayoyapata Muda sio mrefu kwani Mhe Rais anataka kufungua fursa kwa watanzania lakini pia adhma yake ni kuona kuwa Watanzania wananufaika na Rasilimali zao , na ikumbukwe Tanzania ni ya pili Duniani kwa kuwa na vivutio vingi tena vya asili sasa ni muda wa kuvitumia kwa manufaa ya Watanzania na hiki ndicho anachofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan .

Kwa Hakika kipindi hiki cha The Royal Tour ni moja ya uwekezaji Mkubwa sana kwenye sekta ya Utalii kwani Filamu hii itatazamwa vizazi na vizazi na kuitambulisha Tanzania Duniani .

#TwendePamoja
#KwaMatokeoYaHaraka
#KaziIendelee
20210906_181126.jpg
 
Back
Top Bottom