Filamu ya Royal Tour ya Rais Samia, Yapewa Kongole Kuhamasisha Utalii Kulikopelekea Kuongezeka Watalii Wanaotembelea Tanzania

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,614
Wanabodi,

Filamu ya Royal Tour ya Rais Samia, imepongezwa kwa kuchangia kuhamasisha utalii nchini kulikopelekea kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania, kutoka watalii 1,454,000 mpaka watalii 1,806,000, kati ya Desemba 2022 na Desemba 2023, ongezeko ambalo limechangiwa, Pamoja na mambo mengine,ni filamu ya Royal Tour ya Rais Samia, hivyo kufuatia ongezeko hili, umetolewa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa za ajira katika sekta ya utalii kwa kujipatia mafunzo katika huduma za utalii (tourism) ukarimu (hospitality) na uratibu wa matukio (events management), zinazotolewa na Chuo cha Taifa cha Utalli kufuatia chuo hicho kutoa mafunzo ya hali ya juu ya viwango vya kitaifa na kimataifa ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira kwa kuendana na kasi ya ukuaji wa sekta hii.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasisili na Utalii, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki, alipotembelea Makao Makuu ya Chuo hicho yaliyopo kampasi ya Bustani, jijini Dar es Salaam na kukipongeza chuo hicho kwa kutoa mafunzo ya hali ya juu ya viwango vya kitaifa na kimataifa kufuatia kuwa na walimu wabobezi na serikali ya awamu ya 6 kukiwezesha kwa rasilimali fedha, vifaa na miundombinu, hivyo wahitimu kuweza kupata ajira mahali popote duniani.
NCT Photo 2.jpg

Waziri Kairuki aliwashukuru wazazi na walezi na wadau wanaokitumia chuo hicho na kutoa wito kwa Watanzania, kuchangamkia fursa za mafunzo ya utalii zinazotolewa na chuo hicho ili kujipatia ajira kufuatia kukua kwa kasi kwa sekta hiyo kunakochangiwa na mambo mengi ikiwemo ile filamu ya Royal Tour ya Rais Samia ambayo imehamasisha sana na kuisisimua sekta hiyo.

NCT Photo 1.jpg

Kwa upande wake, Mkuu wa chuo hicho cha Taifa cha Utalii, Dr. Florian Mtey amewakaribisha Watanzania kuchangamkia fursa za mafunzo katika huduma za utalii (tourism) ukarimu (hospitality) na uratibu wa matukio (events management), zinazotolewa na Chuo cha Taifa cha Utalli kwa kusisitiza mafunzo yao ni ya hali ya juu ya viwango vya kimataifa ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira kwa kuendana na kasi ya ukuaji wa sekta hii.

NCT Photo 4.jpg

Dr Mtey amesema cguo chake hakijaishia kwenye kutoa mafunzo tuu,, wamejiongeza kwa kwa kuanzisha kampuni ya NCT Utalii and Ukarimu Company Limited inayotoa huduma za catering kwa matukio yanaweza kufanyika hapo hapo katika kumbi zake, au mahali popote, na kutoa wito kwa serikali, taasisi za umma, taasisi binafsi n ahata katika matukio ya kijamii ya watu binafsi, sherehe, misiba au matukio yoyote.

NCT Photo 5.jpg

Dr. Mtey pia amewakaribisha Watanzania kutumia huduma za hoteli ya chuo hivyo kwa vyumba vya kulala, chakula, malazi na hata laundry, chuo kinatoa huduma za mapambo na uratibu wa matukio..

NCT Photo 3.jpg

NCT Photo 7.jpg

Meneja Mafunzo wa Chuo hicho, Mary Maduhu amesema kuna uhusiano mkubwa kati ya huduma za ukarimu na ongezeko la watalii, watalii wanapokuwepo nchini, wakahudumiwa vizuri, wakala chakula kizuri kitamu kilichoanfaliwa kwa mapenzi, watalii hao sio tuu watawamasisha wengine, bali wao wenyewe pia watarejea kutembelea vivutio vilivyobakia, hivyo Chuo cha Taifa cha Utalii, NCT, kinasisitiza zaidi mafunzo kwa vitendo.

Nae Mkufunzi Mbobezi wa mambo ya hoteli, Chef Calist Gabriel Tesha, amesema siri ya chef wazuri wote, ni kuipenda kazi yako kwa moyo wako wote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote, utajikuta unapika chakula kizuri na kitamu, mtu akila, lazima atarudi tena.

NCT Photo 8.jpg
NCT Photo 9.jpg

Kwa upande wao, wanafunzi, Lilian Godifrey Mushi na Patricia Zenus ambao ni wanafunzi wa mwaka wa 3 za Sanaa ya mapishi, , culinary arts, wanawashauri vijana kujiunga na chuo hicho, kwani baada ya kuhitimu sio tuu unaweza kupata kazi popote nan chi yoyote, pia unaweza kujiajiri mwenyewe moja kwa moja, hivyo kupunguzi nakisi ya ukosefu wa ajira kwa vijana.
NCT Photo 6.jpg
NCT Photo 10.jpg

Chuo cha Taifa cha Utalii, NCT ni chuo cha serikali kinachotoa mafunzo katika huduma za utalii (tourism) ukarimu (hospitality) na uratibu wa matukio (events management), na kina kampasi 4, kampasi ya Bustani, iliyopo jijini Dar es Salaam ambapo pia ndio makao makuu ya chuo hicho, kampasi ya Temeke, kuna tawi la Arusha na Tawi la Mwanza.

Paskali
 
Ndugu "njaa" nikwambie kitu, mimi kampuni yangu ya uwakala wa utalii na usafiri imepata wageni 326 kwa mwaka jana.
Kati yao, walioona au kusikia kuhusu "Royal Tour" filamu ni 22 tuu.

Mimi nadeal sana na wastaafu huko Ujeremani, Ujapani, Marekani, Uswizi, Uholanzi, Norway na Finland.

Inawezekana Royal Tour imetia hamasa katika kuongeza watalii, lakini TTB na wizara lazima waje na takwimu za kweli na sahihi ili tujue wapi tunafaidika zaidi.

Katika watalii 326, watalii 208 walisema Covid 19 ilisababisha waje mwaka jana(2023), badala ya miaka ya 2019 - 2022.

Tatizo kubwa la nchii hii ni tafiti na takwimu.

Makampuni mengi ya utalii na safari hapa Tz yanafanya utafutaji masoko yenyewe.
TTB hawana habari ya masoko wala hata kuchukua takwimu.
 
Back
Top Bottom