Royal Tour Yaendelea Kulipa: Cartier Ponant Nayo Yatua Tanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942

Royal Tour Yaendelea Kulipa: Cartier Ponant Nayo Yatua Tanzania

Filamu ya Royal Tour aliyofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kulipa baada ya meli nyingine ya kifahari kutia nanga leo fukwe za Kilwa ikiwa na abiria 125 kutokea nchini Ufaransa.

Hii inakuja ikiwa ni siku mbili tu tangu meli nyingine ya kifahari, Coral Geographer, kutoka Australia, itie nanga Kilwa na kisha Zanzibar ikiwa na watalii 120.

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) leo Machi 9, 2023, imepokea meli nyingine ya kimataifa iliyobeba watalii kutoka nchini Ufaransa.

Ikiwa ni toleo la sita sasa la meli za kifahari za kampuni ya Ponant, Le Jacques, ikibeba jina la mgunduzi mashuhuri wa Kifaransa inaelezwa kwa maneno matamu kama ifuatavyo kuhusu mambo mengi matamu na ya kiburudani uwapo ndani ya meli hii:

“Top-notch sound and lighting technology, including an LED wall, makes the 184-guest Theater a popular gathering space. Guests can enjoy a variety of performances, including educational lectures, jazz and dance performances, karaoke and piano recitals.”

Ujio wa meli hii umeratibiwa na Serikali ya Tanzania, Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya Wanyamapori (Tawa) kwa upande mmoja na kampuni kubwa duniani ya Abercrombie and Kent.

Ujio huu ni juhudi kubwa za Rais Dkt. Samia kwani akiwa nchini Marekani Aprili mwaka jana, wakati wa ziara ya kuzindua filamu ya Royal Tour nchini humo, Mhe Rais wa JMT Dkt. Samia Suluhu Hassan , alikutana pia na Mwenyekiti Mwenza wa Abercrombie and Kent, Manfredi Lefebvre d’Ovidio,na kumshawishi kuongeza ushirikiano na sekta ya utalii nchini Tanzania.

Kuhusu Abercrombie and Kent:

Abercrombie & Kent is one of the world’s leading luxury travel companies. The emphasis is very much on luxury here -- whether it’s small-group travel (limit of 18 per group), tailor-made journeys, expedition cruises, train travel, African safaris, European barge cruises, or any of its many other offerings, just about everything A&K arranges is top of the line (Source: Travelstride.com)​

 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-03-10 at 15.34.40.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-10 at 15.34.40.jpeg
    38.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-03-10 at 15.34.41(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-10 at 15.34.41(1).jpeg
    68.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-03-10 at 15.34.41.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-10 at 15.34.41.jpeg
    67.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-03-10 at 15.34.40(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-10 at 15.34.40(2).jpeg
    64.5 KB · Views: 3
Back
Top Bottom