The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Zaidi Waziri Membe, ni Wenyekiti wa Tume za Uchaguzi, NEC na ZEK na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Oscar Taranco.
Shughuli imeanza kwa burudani ya Mr.Ebbo na Jhikho Man.
 
Mwanamuziki wa kizazi kipya Witness ametoa testimonial kwa akishuka kwa lingua ya anglo saxon utadhani sio Mbongo.

Mkurugenzi wa UNDP sasa anazungumza akiainisha lengo kuu la fungu hili ni kuliwezesha taifa kufanya uchaguzi mkuu huru na wa haki.

Pia amezungumzia umuhimu wa vyombo huru vya habari katika jukumu kuhabarisha, kuelimisha na kuhamasisha suala zima la uchaguzi mkuu.

Amemalizia kwa neno 'Asante Sana'.

Sasa anazungumza M/Kiti wa NEC jaji Lewis Makame.
 
Mkataba umeshasainiwa, Waziri Membe amezungumza kwa Kiswahili, na kilifuatia kipindi cha maswali na majibu.
Membe alieleza pamoja na mambo mengine, fungu hilo pia litatumika kujenga uwezo kwa waandishi wa habari kuripoti uchaguzi huo kwa uhuru na uwazi bila kuegemea upande wowote.
Viburudisho vinafuatia.
 
Hapo ni pa kuangalia pia kwa uangalifu zaidi
 
Pasco.
Viongozi wa upinzani walikuwepo pia? Hizo pesa mgawo wake ukoje maana isije pesa zote zikaishia mikononi mwa fisadi RA peke yake.
 
heko ccm ,hatimaye ndoto imekamilika yauhakika wa gharama za kampeni maana hali ilikuwa mmmhhh!!!!!!!!!
 
Pamoja na kuwa mimi ni muungaji mkono wa demokrasia, lakini naona hao UNDP kama wangekuwa na nina njema wapeleke hizo hela kwenye maendeleo. Najua ni wazo contoversial lakini ndivyo ninavyoona.
 
Tukio limeisha nitawajulisha wachangiaji wakiongozwa na Uingereza iliyotoa Pauni milioni 10.
Mod rekebisha hii sasa sio breaking news tena.
 
Pamoja na kuwa mimi ni muungaji mkono wa demokrasia, lakini naona hao UNDP kama wangekuwa na nina njema wapeleke hizo hela kwenye maendeleo. Najua ni wazo contoversial lakini ndivyo ninavyoona.

Mkuu, kupata viongozi ni maendeleo pia.
 
Pesa hizi ni mkopo au ni zawadi?

Hizi huwa ni grants na siyo mkopo, chini ya utaratibu wa Basket funding ambapo wafadhili wote isipokuwa US ( sera zao haziruhusu kushiriki kwenye basket funding arrangements) huweka fedha zao za ufadhili wa uchaguzi - kila mfadhili ana interest na uchaguzi hivyo ni muhimu kuchangia.UNDP pamoja na kuwa nao hutoa kiasi, kwa vile ni Shirika la UM/UN wanakuwa na nafasi nzuri zaidi kusikilizwa na kuaminiwa na serikali ( trusted partner) wanaratibu kwa niaba ya wengine.In the process ya kuratibu na management ya pesa hizo nao hupata pesa ( management/admin fee) inayowawezesha kujiendesha na kulipia gharama mbalimbali ikiwa ni pamoja na mishahara ya wafanyakazi.So it is to their interest too that they really negotiate with othe DPs kupata hilo jukumu la kuratibu.
Hata uchaguzi uliopita utaratibu ulikuwa hivi hivi.Fedha hizo zilisaidia kuanzisha daftari la wapiga kura, elimu ya uraia,kujenga uwezo wa vyama vya siasa ( japo hawakuvigawia pesa waliwapa mafunzo mbalimbali ya kuweza kushiriki uchaguzi wa vyama vingi), n.k.
 
Wazungu bwana, kwa uwezo na akili zao zote wanaamini kuwa kuna UCHAGUZI Tanzania wa kugharamia mahela yooote hayo ya walipa kodi wao? Najua wana namna ya kuzirudisha pesa hizi kwa njia mbalimbali ikiwemo mikataba mibovu ya uwekezaji.
 
Pamoja na kuwa mimi ni muungaji mkono wa demokrasia, lakini naona hao UNDP kama wangekuwa na nina njema wapeleke hizo hela kwenye maendeleo. Najua ni wazo contoversial lakini ndivyo ninavyoona.

Bongolander,
Mawazo yako mazuri na hata mimi huwa natamani sana hawa jamaa wafanye hivyo. Lakini nimekuja kugundua kuwa hawa wahisani nao hawana tofauti na watz ambao hupenda kuchangia sherehe zaidi kuliko mambo ya maendeleo. Unajua kwamba kama ulimwengu hasa hizi nchi tajiri wangeamua kufuta umaskini na kuboresha miundombinu duniani kote inawezekana kabisa. Ni matajiri na wana mapesa mengi mno lakini hawana huo mpango. Ukiangalia Marekani misaada yake mingi huwa iko kwenye kupunguza Ukimwi ambako wataalamu wa mambo wanasema wakati mwingine wanachomekea hata virus humohumo ili waafrika wafe zaidi.

Nilihudhuria semina mahali fulani Dar, mtoa mada akatudokezea kuwa kuna kitu kinaitwa New York-Brussels Consensus ambayo inasemekana ni makubaliano ya Ulaya na Marekani kuwa makosa yaliyofanyika Asia yasirudiwe tena Afrika. Maana yake ni kwamba misaada ya kimaendeleo iliyotolewa Asia isitolewe kwa Afrika. Sina data zaidi kuhusu hili jambo labda kama kuna mtu mwenye data zaidi atupe.
 
Tukio limeisha nitawajulisha wachangiaji wakiongozwa na Uingereza iliyotoa Pauni milioni 10.
Mod rekebisha hii sasa sio breaking news tena.

Bado kuna watu itaendelea kuwa Breaking News, kwa kuwa kuna wengi bado hawajaingia ktk mtandao.
 
Well, jukumu kubwa la UNDP ni shughuli kama hizi infact siku hizi wanaiita "deepening democracy" whatever that means. Kwa hiyo nadhani ni katika majukumu yake ya kila siku kuhakikisha kwamba resources zinapatikana kwa nyakati za uchaguzi. Sema watanzania wenzangu hatusomi majukumu ya haya mashirika..kwa hiyo tunaona kama tunasaidiwa..lakini reality ni kwamba jukumu la UNDP ndo hili among others. Na hizi hela sio mgao wa bure...kwani na sisi si tunachanga pesa kila mwaka kwenye UN (ofcourse kulingana na uwezo wetu)

Tatizo kubwa nilionalo mimi ni kwamba hizi pesa they hardly help democratize third world countries. I have had a privelege of witnessing kazi za UNDP sehemu mbali mbali..I have to admit ni shirika zuri lenye vision nzuri lakini like other UN agencies..its marred by bureacracy na umangimeza sana.

Well, as said by my compatriot above..UN ni kama watanzania..tunaopenda kuchangia harusi na sherehe. Ukiomba pesa za kujenga barabara..watakwambia kopa..ukiomba pesa za kununua tshirt na kofia/warsha za kuhamasisha watakupa..duh...kazi tunayo.
 
Dondoo 10 muhimu za Mkataba huo.
1. Kuundwa kwa bodi za kusimamia Chakuzi, bara na visiwani
2. Elimu kwa wapiga kura. Uhamasishaji wa ziada kwa wanawake na vikundi tengwa.
3. Vyama vya siasa kushiriki kikamilifu katika hatua zote
4. Wagombea wanawake kujengewa uwezo.
5. Vyombo vya habari kujengewa uwezo kuripoti uchaguzi.
6. Mitandao na asasi za kiraia kujengewa uwezo kuhamasisha ushiriki.
7. Vyombo vya usimamizi kujengewa uwezo na rasilimali kusimamia chaguzi.
8. Vyombo vidau vya uchaguzi zikiwemo taasisi za kiraia kujengewa uwezo kushiriki.
9. NEC na ZEK kutambuliwa rasmi kama wadau muhimu.
10. UNDP kuratibu zoezi zima la Uchaguzi 2010.

5.vyombo vya habari vya
 
big mistake

uchaguzi tungeughaamia kwa pesa zetu wenyewe kama walivyofanya zimbabwe

hiii ya kupewa pesa za uchaguzi akishinda mtu ambaye wao hawamtaki itakuwaje?

na hasa kule visiwani?

otherwise wajiandae kuwapokea wakimbizi zaidi wa kisiasa from Zanzibar by December 2010
 
Uchaguzi ni suala linalowahusu watu wenyewe. Kama hawawezi kucahguana mpaka wapate msaada pia hawawezi kutawalana mpaka waelekezwe jinsi ya kutawlana au watawaliwe moja kwa moja au kisirisiri. Tutakuwa tumefanya hatua muhimu tukiacha na misaada ya namna hii. Hata ikimaanisha kuweka utaratibu wa watemi/wafalme yaani wasiohitaji kuchagua mara kwa mara. Aibu gani kuhitaji msaada wa kuchaguana nani atuongoze!
 
big mistake

uchaguzi tungeughaamia kwa pesa zetu wenyewe kama walivyofanya zimbabwe

hiii ya kupewa pesa za uchaguzi akishinda mtu ambaye wao hawamtaki itakuwaje?

na hasa kule visiwani?

otherwise wajiandae kuwapokea wakimbizi zaidi wa kisiasa from Zanzibar by December 2010

hawa hawatoi tuu mihela hiyo kama hawana faida zao za kifisi humo
 
Mkataba umeshasainiwa, Waziri Membe amezungumza kwa Kiswahili, na kilifuatia kipindi cha maswali na majibu.
Membe alieleza pamoja na mambo mengine, fungu hilo pia litatumika kujenga uwezo kwa waandishi wa habari kuripoti uchaguzi huo kwa uhuru na uwazi bila kuegemea upande wowote.
Viburudisho vinafuatia.

Will they enter into JF zone? There should be opportunities for JF to enter mainstream and connect to the grassroots. Invisible, plans in place yet?
 
Back
Top Bottom