The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Wewe mbona una mtazamo finyu unafikiri kila anayeweka kitu jf ni kwa sababu kina makosa ??
 
CCM waanza kampeni za Kikwete 2010 wamchangia Sh milioni za fomu

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ameanza kupigiwa upatu ili awe mgombea pekee katika uchaguzi mkuu 2010.

Na Lilian Lugakingira, Bukoba

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeanza safari ndefu ya kumnadi Rais Jakaya Kikwete ili awe mgombea pekee katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, na tayari wilaya ya Bukoba Mjini imetoa hundi ya Sh1milioni za kulipia fomu yake ya kuwania nafasi hiyo.

Hundi hiyo ilitolewa jana na Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Bukoba Mjini kwa maelezo kuwa umeridhishwa na uongozi wa Kikwete katika kutekeleza na kutimiza ilani ya CCM, na hivyo kuungana na jumuiya nyingine, vikundi na watu mbalimbali waliojitokeza kuanza kumkapenia Kikwete.

Hata hivyo, katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliiambia Mwananchi jana kuwa hajui kwa nini jumuiya hiyo ya vijana wa chama chake imefanya hivyo na kwamba atawatafuta ili kupata ukweli na sababu za kitendo hicho.

"Niano msimamo wa chama, lakini siwezi kusema kwa sababu sijajua wamefanya nini. Bila shaka wanayo sababu," alisema Makamba baada ya kuuliza maswali mengi kuhusu kitendo hicho cha UVCCM Bukoba.

Katika halfa iliyofanyika mjini hapa, mwenyekiti wa UVCCM wa Bukoba Mjini, Chifu Kalumuna alimkabidhi mwenyekiti wa CCM wilayani Bukoba Mjini, luteni mstaafu Ally Shamte hundi ya fedha za kuchukulia fomu hizo.

Katika hafla hiyo, Kalumuna pia alimkabidhi mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki hundi ya Sh 100,000 kwa ajili ya kuchukulia fomu za kuwania ubunge katika uchaguzi huo.

Akizungumzia sababu za kutoa fedha kwa Kikwete na Kagasheki kwa ajili ya kuchukulia fomu, katibu wa vijana wa Bukoba Mjini, Yusuph Kaliat alisema wamefanya hivyo kutokana na kuridhika na ufanisi katika utekelezaji wa ilani ya CCM.

“Sisi kama vijana na nguzo ya taifa, tumeamua kutoa zawadi hiyo ili viongozi hao waendelee kuongoza, kila mmoja kwa nafasi aliyokuwa nayo,” alisema Kaliat katika hafla hiyo

iliyohudhuriwa na viongozi kadhaa wa CCM na UVCCM, akiwemo Kagasheki.

Chifu Kalumuna alikabidhi hundi zote mbili kwa Balozi Kagasheki ambaye naye alimkabidhi Shamte.

Hakuna maelezo yaliyotolewa kwa nini UVCCM wilaya ya Bukoba imeamua kutoa fedha hizo sasa, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya mchakato wa uteuzi za majina ya wagombea na kuanza kampeni.

Kwa kawaida, CCM ina kipindi chake cha kuanza kampeni za ndani kwa wagombea wa nafasi zote za kuanzia serikali za mitaa, udiwani, ubunge na urais, lakini muda rasmi unaoruhusiwa na Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya kuanza kampeni ni miezi minne kabla ya tarehe ya uchaguzi.

Uchaguzi mkuu utafanyika mwezi Agosti mwaka 2010.

Kitendo cha wilaya hiyo kutoa fedha kwa ajili ya kuchukulia fomu kinaelekea kuwa ni mkakati mpya wa kumnadi Kikwete pamoja na Kagasheki, ambaye hivi karibuni alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema hatawania kiti hicho tena.

Fedha hizo za jumuiya ya vijana ya Bukoba Mjini ni sehemu ya kampeni kadhaa ambazo zimekuwa zikionekana katika miezi ya karibuni kumpigia debe Kikwete, ambaye alipata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa mwaka 2005.

Hivi karibuni Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Manyara ulimpendekeza Kikwete kuwa mgombea pekee wa nafasi ya urais katika chama chao cha CCM.

Umoja huo ulitoa msimamo huo Mei 30 katika mkutano mkuu wa mkoa uliofanyika kata ya Magugu wilayani Babati ambako mgeni rasmi alikuwa katibu mkuu wa UWT, Hasna Sudi Mwilima.

Risala ya akina mama hao iliyosomwa na katibu wa mkoa, Venosa Mjema ilisema wamenufaika zaidi na uongozi wa Rais Kikwete tangu alipoingia madarakani mwaka 2005.

Pia mkoa wa Rukwa ulionyesha kuridhishwa na uongozi wa Kikwete katika hafla ya kuchangisha pesa kwa ajili ya ujenzi wa shule za mkoa huo.

Katika hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam na ambayo mgeni rasmi alikuwa Kikwete, kiasi cha Sh 1.4bilioni kilichangwa kwa fedha taslimu au ahadi.

Wanachama wengine wa CCM waliowahi kutoa kauli za kutaka Kikwete awe mgombea pekee wa chama hicho ni pamoja na makamu mstaafu wa rais, Samuel Malecela, mwenyekiti wa zamani wa CCM mkoani Dodoma, Pancras Ndejembi na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoani Dar es Salaam, Mzee Hemed Mkali.

Baada ya wazee hao kutoa kauli hiyo mapema mwaka huu, Mbunge wa Sumve, John Shibuda alidai kwamba atachukua fomu kuwania urais mwaka 2010. Shibuda pia alikuwa miongoni mwa wana-CCM 11 waliochukua fomu kuwania urais mwaka 2005.

Wengine ni makamu mwenyekiti wa zamani wa CCM, Malecela, waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof Mark Mwandosya, Balozi Patrick Chokara, Balozi Ali Karume, Dk Abdallah Kigoda, Dk William Shija, Dk Salim Ahmed Salim na Idd Simba.

Akionekana kunogesha kampeni za chini kwa chini hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Shinyanga, Rais Kikwete mwenyewe alisema haoni sababu kwa nini akina mama waliofaidika na mradi huo wamnyime kura mwakani.

“Nasema, kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kupata usingizi… mimi sioni kwa nini akina mama walionufaika na mradi huu waninyime kura,” alisema Kikwete huku akishangiliwa na akina mama waliofika kwenye uzinduzi huo.

samp1.jpg
 
Mi nadhani ingemuondoa kwenye orodha ya wagombea kwa sababu ameanza kampeni kabla ya muda amekiuka sheria ya uchaguzi au tupeleke malalamiko yetu umoja wa mataifa
 
CCM waanza kampeni za Kikwete 2010 wamchangia Sh milioni za fomu

kikwetecapaign.jpg

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ameanza kupigiwa upatu ili awe mgombea pekee katika uchaguzi mkuu 2010.Na Lilian Lugakingira, Bukoba

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeanza safari ndefu ya kumnadi Rais Jakaya Kikwete ili awe mgombea pekee katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, na tayari wilaya ya Bukoba Mjini imetoa hundi ya Sh1milioni za kulipia fomu yake ya kuwania nafasi hiyo.

Hundi hiyo ilitolewa jana na Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Bukoba Mjini kwa maelezo kuwa umeridhishwa na uongozi wa Kikwete katika kutekeleza na kutimiza ilani ya CCM, na hivyo kuungana na jumuiya nyingine, vikundi na watu mbalimbali waliojitokeza kuanza kumkapenia Kikwete.

Hata hivyo, katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliiambia Mwananchi jana kuwa hajui kwa nini jumuiya hiyo ya vijana wa chama chake imefanya hivyo na kwamba atawatafuta ili kupata ukweli na sababu za kitendo hicho.

"Niano msimamo wa chama, lakini siwezi kusema kwa sababu sijajua wamefanya nini. Bila shaka wanayo sababu," alisema Makamba baada ya kuuliza maswali mengi kuhusu kitendo hicho cha UVCCM Bukoba.

Katika halfa iliyofanyika mjini hapa, mwenyekiti wa UVCCM wa Bukoba Mjini, Chifu Kalumuna alimkabidhi mwenyekiti wa CCM wilayani Bukoba Mjini, luteni mstaafu Ally Shamte hundi ya fedha za kuchukulia fomu hizo.

Katika hafla hiyo, Kalumuna pia alimkabidhi mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki hundi ya Sh 100,000 kwa ajili ya kuchukulia fomu za kuwania ubunge katika uchaguzi huo.

Akizungumzia sababu za kutoa fedha kwa Kikwete na Kagasheki kwa ajili ya kuchukulia fomu, katibu wa vijana wa Bukoba Mjini, Yusuph Kaliat alisema wamefanya hivyo kutokana na kuridhika na ufanisi katika utekelezaji wa ilani ya CCM.

“Sisi kama vijana na nguzo ya taifa, tumeamua kutoa zawadi hiyo ili viongozi hao waendelee kuongoza, kila mmoja kwa nafasi aliyokuwa nayo,” alisema Kaliat katika hafla hiyo
iliyohudhuriwa na viongozi kadhaa wa CCM na UVCCM, akiwemo Kagasheki.
Chifu Kalumuna alikabidhi hundi zote mbili kwa Balozi Kagasheki ambaye naye alimkabidhi Shamte.

Hakuna maelezo yaliyotolewa kwa nini UVCCM wilaya ya Bukoba imeamua kutoa fedha hizo sasa, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya mchakato wa uteuzi za majina ya wagombea na kuanza kampeni.

Kwa kawaida, CCM ina kipindi chake cha kuanza kampeni za ndani kwa wagombea wa nafasi zote za kuanzia serikali za mitaa, udiwani, ubunge na urais, lakini muda rasmi unaoruhusiwa na Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya kuanza kampeni ni miezi minne kabla ya tarehe ya uchaguzi.
Uchaguzi mkuu utafanyika mwezi Agosti mwaka 2010.

Kitendo cha wilaya hiyo kutoa fedha kwa ajili ya kuchukulia fomu kinaelekea kuwa ni mkakati mpya wa kumnadi Kikwete pamoja na Kagasheki, ambaye hivi karibuni alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema hatawania kiti hicho tena.

Fedha hizo za jumuiya ya vijana ya Bukoba Mjini ni sehemu ya kampeni kadhaa ambazo zimekuwa zikionekana katika miezi ya karibuni kumpigia debe Kikwete, ambaye alipata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa mwaka 2005.

Hivi karibuni Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Manyara ulimpendekeza Kikwete kuwa mgombea pekee wa nafasi ya urais katika chama chao cha CCM.

Umoja huo ulitoa msimamo huo Mei 30 katika mkutano mkuu wa mkoa uliofanyika kata ya Magugu wilayani Babati ambako mgeni rasmi alikuwa katibu mkuu wa UWT, Hasna Sudi Mwilima.

Risala ya akina mama hao iliyosomwa na katibu wa mkoa, Venosa Mjema ilisema wamenufaika zaidi na uongozi wa Rais Kikwete tangu alipoingia madarakani mwaka 2005.

Pia mkoa wa Rukwa ulionyesha kuridhishwa na uongozi wa Kikwete katika hafla ya kuchangisha pesa kwa ajili ya ujenzi wa shule za mkoa huo.

Katika hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam na ambayo mgeni rasmi alikuwa Kikwete, kiasi cha Sh 1.4bilioni kilichangwa kwa fedha taslimu au ahadi.

Wanachama wengine wa CCM waliowahi kutoa kauli za kutaka Kikwete awe mgombea pekee wa chama hicho ni pamoja na makamu mstaafu wa rais, Samuel Malecela, mwenyekiti wa zamani wa CCM mkoani Dodoma, Pancras Ndejembi na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoani Dar es Salaam, Mzee Hemed Mkali.

Baada ya wazee hao kutoa kauli hiyo mapema mwaka huu, Mbunge wa Sumve, John Shibuda alidai kwamba atachukua fomu kuwania urais mwaka 2010. Shibuda pia alikuwa miongoni mwa wana-CCM 11 waliochukua fomu kuwania urais mwaka 2005.

Wengine ni makamu mwenyekiti wa zamani wa CCM, Malecela, waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof Mark Mwandosya, Balozi Patrick Chokara, Balozi Ali Karume, Dk Abdallah Kigoda, Dk William Shija, Dk Salim Ahmed Salim na Idd Simba.

Akionekana kunogesha kampeni za chini kwa chini hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Shinyanga, Rais Kikwete mwenyewe alisema haoni sababu kwa nini akina mama waliofaidika na mradi huo wamnyime kura mwakani. “Nasema, kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kupata usingizi… mimi sioni kwa nini akina mama walionufaika na mradi huu waninyime kura alisema Kikwete huku akishangiliwa na akina mama waliofika kwenye uzinduzi huo.
 
Last edited:
Wanajipendekeza hao!!! Si unajua tena kazi ya wapambe na jumuiya za chama!!! Kuna issues muhimu ambazo ziko pending, hazisogei lakini mambo ya bendera fuata upepo ndiyo yanakuwa priority!!! Huko ndiko kutojiamini. Nakuhakikishia kama nataka kazi fulani au uongozi sihitaji wapambe, najiamini kwa sababu sifa ninazo. Na always not otherwise!!! Kila wakati ma-cheap popularity tuuuu weeee, ni lini tutabadilika???
 
Mtu mwingine akianza kupigiwa debe itakuwaje? Watamfanyia kama wanavyomwandama Mengi? Mlango umefunguliwa sasa tuanze kuwapigia debe watakaotufaa.
 
Wanabodi ebu tujikumbushe na CCM na hizi chaguzi ilikotoka..Tusiwe wepesi wa kulaumu na kusikiliza hizi kampeni chafu wakati tunajua fika kwamba CCM siku zote hujiandaa mwaka mzima kabla ya uchaguzi na hata kubadilisha sheria...
nawaomba someni hii makala ya Jenerali Ulimwengu, pamoja na kwamba ni ndefu sana lakini inatukumbusha kwamba hakuna ksichowezekana chini ya CCM wakitaka..
 
MABADILIKO YA KATIBA KAMA NYENZO YA UFISADI

Na jenerali Ulimwengu.

MWAKA 2000, kabla ya uchaguzi mkuu, Bunge la Jamhuri ya Muungano lilifanya mabadiliko ya kikatiba ambayo, miongoni mwa mambo mengine, yalibainisha kwamba mgombea urais anaweza kuchaguliwa na akakabidhiwa madaraka ya rais bila kulazimika kupata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa.
Kwa wale waliojua kilichokuwa kikifanyika hii ilikuwa ni hatua muhimu sana, ingawaje haikupokelewa kwa kelele ambazo zilikuwa zinastahili. Umuhimu wake unatokana na kwamba mabadiliko hayo yalikuwa yanaingiza mbegu za utata mkubwa unaoweza kuikumba nchi hii huko tuendako, hata kama hivi sasa hatujui kwamba bomu limetegwa ila sisi hatujui.
Nitaeleza. Kukubali kikatiba na kisheria kwamba mgombea anaweza kuwa rais bila kulazimika kupata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa ni kukubali kwamba mtu anaweza kuwa rais bila kuwa na ridhaa, angalau, ya nusu ya wapiga kura wake. Ina maana kwamba, hata kama asilimia sitini, au sabini, au hata themanini wakimkataa, tena wakasema hivyo kwa kishindo, mtu huyo atakuwa rais alimradi ndiye aliyepata kura nyingi kuliko mgombea ye yote mwingine.
Tuchukue sura tuliyo nayo ya vyama vya siasa nchini Tanzania hivi leo. Tuseme kwamba vyama vinane vimewaweka wagombea wa nafasi ya urais, na vyama hivyo ni CCM, CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi, TLP, Democrasia Makini, DP na TPP.
Iwapo miongoni mwa wagombea wa vyama hivyo wagombea wa vyama saba, (tuseme CCM, CUF, NCCR-Mageuzi, TLP, Demokrasia Makini, DP na TPP), watapata jumla ya asilimia 70 ya kura zilizopigwa, kisha mgombea wa CHADEMA akapata asilimia 30, mgombea wa CHADEMA atakuwa rais.
Mantiki ya uamuzi huo bado haijanielea, na wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa, kisheria na kikatiba wanasema haijawaelea. Ilikuwa vigumu zaidi (labda kuliko ilivyo leo) kuielewa wakati huo ikipitishwa kwa sababu ya tukio moja kuu la miaka mitano tu kabla ya uamuzi huu wa kushangaza. Nitalisimulia.
Mwaka 1995, mwishoni kabisa mwa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM pale Chimwaga, wagombea watatu wa mwisho waliopigiwa kura walikuwa Jakaya Kikwete, Benjamin Mkapa na Cleopa Msuya.
Kura zilipohesabiwa ikadhihirika kwamba hakuna mmoja aliyeweza kupata zaidi ya nusu ya kura, na kwa hiyo ikabidi wawili wa juu warudiane katika kile kinachoitwa run-off. Msuya alipata kura za chini zaidi, kwa hiyo run-off ikawa kati ya Kikwete na Mkapa, na Mkapa akashinda.
Najua wapo watu wanaodai kwamba ulikuwa uamuzi wa mzengwe; kwamba Kikwete alikuwa kashinda; kwamba Mwalimu Nyerere aliingilia kati "kumnusuru Mkapa" ; eti Mwalimu alimwambia Kikwete: Wewe bado kijana, mwachie mwenzako, zamu yako itakuja.
Hadithi hii nitaijadili mbele ya safari, lakini kwa sasa niseme tu kwamba si kweli. Katika majukumu ya mkutano mkuu wa CCM katika mwaka wa uchaguzi mkuu wa Taifa, mojawapo ni "kumchagua" mwanachama atakayegombea urais wa Jamhuri, na kwa mujibu wa katiba ya CCM uchaguzi katika nafasi ya aina hiyo hauna budi uheshimu kanuni mbili kuu, miongoni mwa nyingine: moja, uchaguzi uwe kwa kura ya siri; pili mshindi apatikane kwa zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa.
Iwapo hivyo ndivyo ilivyo na ndivyo ilivyokuwa huko Chimwaga wakati huo; na iwapo matakwa hayo ya katiba ya CCM yalijengeka juu ya msingi wa mantiki fulani; na iwapo mantiki hiyo ndiyo iliyomfanya Mkapa awe mgombea wa CCM na siyo Kikwete; na iwapo mantiki hiyo ndiyo iliyotaka kwamba uchaguzi wa Taifa umpate rais kutokana na mgombea aliyepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa, sasa ni kwa nini mgombea aliyepitishwa kwa kanuni ya "zaidi ya nusu ya kura" katika chama chake aifutilie mbali kanuni hiyo kwenye ngazi ya Taifa kabla ya kugombea muhula wa pili?
Jibu rahisi ni kwamba washauri wa Benjamin Mkapa, wakati huo akiwa rais, hawakuamini, au yeye mwenyewe hakuamini kwamba angeweza kupata zaidi ya nusu ya kura ambazo zingepigwa katika uchaguzi wa 2000. Kwa hiyo, kama kawaida ya watawala wetu wanapotaka kukidhi maslahi yao bila ya kujali maslahi ya Taifa, ikaamuliwa kuiondoa ‘kero' hiyo kutoka katiba ya Jamhuri.
Labda tungekumbushana kwamba wakati mabadiliko haya yanafanyika Mwalimu Nyerere alikwisha kuaga dunia, na tunajua sasa kwamba mambo mengi ya kifisadi yalifanyika wazi wazi pale watawala walipojua kwamba hakuna mtu mwenye kauli nzito angeweza kuwakemea hata wangefanya nini.
Kwa maneno mengine, kifo cha Mwalimu kilikuja kama fursa kwa kila aina ya ufisadi kuchanua bila kuchelea kusutwa. Sote tunajua kwamba Mwalimu katika miaka yake ya ustaafu alikuwa amejenga utamaduni wa kushiriki, kama raia ye yote anayejali, katika mijadala kuhusu mustakabali wa Taifa, na ni vigumu kuamini kwamba angekaa kimya kuhusu suala hili, kama ambavyo najua asingenyamaa kuhusu ule ufisadi mwingine unaohusu mali.
Kwamba Mkapa na watu wake walikuwa wametishika katika uchaguzi wa mwaka 1995 ni dhahiri, nami naweza kulirudia hili mara nyingi. Augustine Mrema alikuwa amechota akili za watu wengi kiasi cha kuifanya kampeni ya Mkapa iegemee zaidi nguvu ya ushawishi aliokuwa nao Mwalimu kwa watu wake walio wengi. Bila Mwalimu ilikuwa vigumu kuona ni jinsi gani Mkapa angeshinda.
Hata hivyo, mwaka 2000 mambo yalikuwa yamekwisha kubadilika sana. Kweli, Mwalimu alikwisha kuondoka, lakini Mkapa alikuwa amefanya kazi nzuri (kwa ujumla) katika miaka mitano ya uongozi wake, na wala hakuwa na sababu ya kuichezeachezea katiba ili kujihakikishia ushindi kwa njia yo yote ile, kitendo ambacho bila shaka kilizidisha nguvu ya uvumi kwamba hata Chimwaga 1995 utaratibu ulipindwa ili kumlinda Mkapa.
Hapa tunakumbana na suala kubwa, zito na la msingi. Kwa kubadili katiba kama ilivyoelezwa hapo juu, Mkapa na watu wake, hususan washauri wake wakuu akiwamo Mwanasheria Mkuu, waliitendea nchi hii haki?
Je, maslahi ya Mkapa na watu wake ya kurejea madarakani mwaka 2000 yalikuwa na ushawishi wenye uzani wa kutosha kuiingiza nchi katika utaratibu ambao hapo baadaye unaweza kuifanya nchi ikatawaliwa na mtu ambaye hatakiwi?
Je, kitendo cha kubadili katiba jinsi kilivyofanywa hakikuwa na maana ya kwamba Mkapa na washauri wake walikuwa radhi kubakia madarakani kwa njia yo yote ile, hata kama wananchi wangekuwa hawamtaki? Au siyo maana yake?
Hapa sitaki kuingia katika uchunguzi wa kazi hiyo muhimu waliyotaka kuifanya (Mkapa na watu wake katika muhula wa pili) hadi wakaichezea katiba (nitaijadili katika sura zijazo), bali tu nataka niseme kwamba kilikuwa kitendo cha hovyo, kitendo cha uhuni na kilichodhihirisha udhaifu mkubwa wa imani, yote ambayo leo hii hayashangazi.
Mwanademokrasia (dhahiri, Mkapa na washauri wake sio) hawezi kubadilisha kanuni za ushindani kwa sababu tu ameona kwamba zitamnyima ushindi. Atazibadili pale tu anaposhawishika kwamba kwa kuzirekebisha atatoa uhuru mkubwa zaidi kwa raia zake, ili sauti yao katika uendeshaji wa nchi isikike zaidi.
Katika awamu ya tatu tulizoea sana kusikia maneno "uvivu wa kufikiri" ambao, mimi nakiri, umejaa tele nchini mwetu, hususan miongoni mwa watawala wasiotaka kusumbua vichwa vyao kudurusu mifumo mbadala ya kuendeshea shughuli za utawala na maendeleo ya watu wao. Uvivu huo wa kufikiri unatokana na kwamba muda wao ulio mwingi wanashughulika na mambo mengine, ambayo hawakuyasema katika ilani zao.
Isingekuwa hivyo wangetumia muda mwingi zaidi kujadili nini kifanyike iwapo hakuna mgombe mmoja aliyepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa. Njia moja ni kufanya kama ilivyotokea Chimwaga 1995 Kikwete na Mkapa waliporudiana baada ya kumtoa Msuya. Njia nyingine ni ushirikiano, katika serikali, baina ya vyama vinavyokaribiana katika falsafa na mwelekeo. Kwa vyo vyote vile, mwaka 2000 hatukufika huko, kwani Mkapa, pamoja na woga wake wote, pamoja na kutojiamini, alishinda.
 
Rais - Edward Lowasa
Makamu wa rais - Y.Makamba
Waziri mkuu - Rostam Azizi
Baraza la mawaziri (bila kujali wizara zao)
Sofia Simba, Mramba, Mkuchika, Jeetu patel, Subash Patel, Tanil Somaiya, Kinana, Mzee wetu Kingunge, Salva Rweyemamu, John Mwakipesile, James nsekela, Mzee wa Vijisenti chenge, Tambwe Hiza, Rita mlaki, E.Nchimbi, L. Masha, Anna Mkapa, Mdhihiri Mdhihiri, Mahita, Mehgji, Ridhiwani kikwete, Ngereja, Daniel Yona, Yusuf Manji,
 
loooh...pangekuwa patamu!!! hakuna wa kuiba maana wote wajanja. mwizi mpe mwanao akulindie
 
Rais - Edward Lowasa
Makamu wa rais - Y.Makamba
Waziri mkuu - Rostam Azizi
Baraza la mawaziri (bila kujali wizara zao)
Sofia Simba, Mramba, Mkuchika, Jeetu patel, Subash Patel, Tanil Somaiya, Kinana, Mzee wetu Kingunge, Salva Rweyemamu, John Mwakipesile, James nsekela, Mzee wa Vijisenti chenge, Tambwe Hiza, Rita mlaki, E.Nchimbi, L. Masha, Anna Mkapa, Mdhihiri Mdhihiri, Mahita, Mehgji, Ridhiwani kikwete, Ngereja, Daniel Yona, Yusuf Manji,

Liyumba, Kweka na Peter Noni wanastahili nafasi pia!
 
I was a little bit busy thus i was not available but now i am back.
i think that government will not be effective and committed since all the people are not competent enough to run the government which is need to bring this important nation to path of brighter future which its children deserve.
Also Tanzania do not need experience leader any more since they have proving as wrong by showing that they are not capable of being the true sons of Tanzania.
 
I was a little bit busy thus i was not available but now i am back.
i think that government will not be effective and committed since all the people are not competent enough to run the government which is needed to bring this important nation to path of brighter future which its children deserve.
Also Tanzania do not need experience leaders any more since they have proving us wrong by showing that they are not capable of being the true sons of Tanzania.
 
Bado wapo wengi hujawapa nafasi zao za manaibu waziri kama Karamagi, msabaha, malima n.k
 
Back
Top Bottom