The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Na Mwandishi Wetu

IKIWA imesalia takriban miezi 18 kabla ya Uchaguzi Mkuu Oktoba mwakani, sasa ni dhahiri kuwa Rais Jakaya Kikwete ana kibarua kigumu cha kukamilisha ahadi lukuki alizotoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Mazingira hayo pia yanawaweka njiapanda wabunge wengi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika kutetea tena nafasi zao.

Baadhi ya wabunge tayari wameliona hilo na miongoni wamelisema bungeni wakiwashutumu mawaziri ambao wamekuwa wakilimbikiza miradi ya maendeleo kwa upendeleo kwenye maeneo yao bila kuzingatia vipaumbele vya taifa, hata baadhi yao walifikia hatua ya kutishia kukwamisha bajeti iliyopitishwa Alhamisi iliyopita.

Kauli kali zaidi ilitoka kwa Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii aliyeomba dua kwa Mungu awalaami mawaziri hao.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, ahadi kadhaa alizozitoa Rais Kikwete bado hazijatekelezwa na kwa kipindi kilichosalia ni vigumu kufanya hivyo.

Miongoni mwa ahadi alizotoa Rais Kikwete na hazijaonekana matunda yake dhahiri ni zile zilizoandamana na kaulimbiu yake ya Ari Mpya, Nguvu Mpya, Kasi Mpya na mpango wa ‘Maisha bora kwa kila Mtanzania’.

Kigogo mmoja ndani ya CCM amelieleza gazeti hili kwamba ahadi hiyo ya maisha bora ndiyo ilimpatia Kikwete kura za kishindo na isipotengenezewa mkakati maalumu inaweza kuwa ndio kitanzi chake na wabunge wengi wa CCM.

Alisema ahadi hiyo imesababisha baadhi ya vigogo wa chama na serikali kubadili kauli, na kusema kwamba maisha bora hayatawafuata wananchi kama hawafanyi kazi kwa bidii.

Kwa mujibu wa watu mbalimbali waliozungumza na Mwananchi Jumapili, na hata kauli za wabunge wanapochangia bungeni, Watanzania walio wengi bado wana hali duni ya kimaisha, jambo ambalo litakuwa gumu kulieleza kwa wapigakura hapo mwakani.

Kutokana na ahadi hiyo serikali ilitoa Sh30 bilioni ambazo zilipewa jina la mabilioni ya Kikwete, lakini hazikufika kwa maskini walio wengi kutokana na masharti yake kuwa magumu, na kuangukia kwenye mikono ya wasio wajasiriamali wadogo, hivyo kukwamisha mpango huo wa rais.

Ahadi nyingine zinazoelekea kushindikana ni ya mwafaka wa kisiasa wa Zanzibar ambao Rais Kikwete aliuweka kwenye kipaumbele, lakini hadi sasa hakuna mafanikio yoyote na tayari Chama cha Wananchi (CUF), kimetangaza kujitoa katika mazungumzo.

Ahadi nyingine ni ujenzi wa madaraja ya Kilombero mkoani Morogoro na Kigamboni, jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa ahadi kubwa alizotoa Kikwete na hadi sasa hakuna dalili zinazoweza kuashiria kuwa ipo nia ya utekelezaji.

Hata hivyo, Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa alipoulizwa alisema kwamba daraja la Kilombero limetengewa fedha katika bajeti ya mwaka 2009/10.

Kuhusu daraja la Kigamboni, alirudia kauli za muda mrefu kuwa hilo limo kwenye mkakati wa kuanza kujengwa wakati wowote chini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kushirikiana na wahisani mbalimbali.

Ahadi nyingine ambazo hazijatekelezwa, zimeelezwa kuwa ni kilio cha mahakama nchini juu ya suala la masilahi ya watumishi na vifaa vya kazi.

Hivi karibuni, Jaji Mkuu, Augustino Ramadhan alisikika akilalamika kuwa kiwango cha mafungu yanayoahidiwa kutengwa kwa mahakama hufika kwao kikiwa pungufu.

Suala jingine limeelezwa kuwa ni uboreshaji wa mashirika ya umma ambayo bado yako mikononi mwa serikali, lakini kila kukicha yamekuwa na matatizo na kuzua malalamiko mengi.

Kwa upande wa barabara ambazo ziliahidiwa kujengwa kwa kiwango cha lami na ambazo bado ni Tabora-Nzega, Bunda-Ukerewe na Marangu-Mkuu Rombo-Tarakea-Kamwanga.

Aliahidi pia kulifanya jimbo la Rorya mkoani Mara kuwa wilaya, lakini utekelezaji wake umekuwa ukisuasua.

Mambo mengine ilikuwa ni kupambana na rushwa, lakini pamoja na hali hiyo kuonekana kuzaa matunda kwa mambo mengi yaliyokuwa yamejificha kuchimbuliwa na kuwekwa hadharani, malalamiko yanayoibuka ni baadhi ya watuhumiwa kutofikishwa mahakamani.

Rais Kikwete pia aliahidi kuondoa kero nyingi za Muungano lakini licha ya kuunda kamati ya kuzijadili na kuzishughulikia chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, zipo dalili za baadhi ya wananchi kutoridhika.

Tatizo kubwa linalojitokeza ni baadhi ya Wazanzibari, wakiwamo viongozi wa SMZ kutoa kauli zinazoonyesha dalili za waziwazi kwamba wanadhulumiwa ndani ya Muungano.

Pamoja na hali hiyo, Rais Kikwete atajivunia kwa kutekeleza ahadi yake ya kulifanya Bunge kuwa huru kwani limeonyesha dhahiri kuwa na meno kwa kufichua udhaifu wa baadhi ya vigogo serikali bila kuwa na woga.

Ameonyesha mafanikio pia katika ahadi yake ya kuendesha dola kwa misingi ya utawala bora na uwajibikaji; utawala wa sheria unaoheshimu na kulinda haki za binadamu.

Hata hivyo, katika kipengele hicho kuna manung’uniko kadhaa kama vile baadhi ya viongozi wanaotuhumiwa kuendelea na nyadhifa zao wakati taratibu za utumishi wa umma ziko wazi kwamba wangepaswa kusimamishwa au kupewa likizo ama kuhamishiwa sehemu nyingine, ili uchunguzi huru ufanyike.

Mafanikio mengine ni kutekeleza ahadi ya kuongeza nafasi za elimu ya juu baada ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Ahadi nyingine ambayo Rais Kikwete ameonekana wazi kuivalia njuga ni kuboresha kilimo; na tayari mikakati kadhaa ikiwepo ya pembejeo za kilimo imewekwa, ingawa kuna malalamiko ya pembejeo kutofika kwa wakulima na wakulima wa karafuu na kahawa kutokuwa huru kutafuta masoko yao nje ya nchi.

Nguvu kubwa ya serikali yake kuielekeza kwenye kilimo imechagizwa na mtikisiko wa uchumi duniani ambao umetishia uchumi wa nchi nyingi hasa maskini ambazo zinategemea chakula kutoka nje.

Licha ya mafanikio hayo, serikali ya Kikwete inakabiliwa na changamoto kadhaa hasa za wananchi kutoridhika na mambo mbalimbali yanayotendwa na serikali yake.

Lingine ni wananchi kuona kuwa bado serikali ina matumizi makubwa ya fedha na wakati huo huo inawabidi kufunga mkanda ili kuihudumia huku wakikabiliwa na mazingira magumu ya kipato.

Malalamiko mengine ni baadhi ya watendaji serikalini kuendelea kutumia magari ya kifahari na kutenga Sh19 bilioni kwa ajili ya chai maofisini.


Source:
Mwananchi
 
Ahadi za kikwete ni kwa miaka kumi mzee..

Heshima mbele mkuu. Raisi utawekaje ahadi za miaka kumi tu? Lazima kuwa na long term goals na short term goals. Muda wa uraisi ni miaka mitano kwa hiyo hatakiwi kuassume kwamba ni lazima atimize miaka kumi madarakani hata kama ndiyo hivyo CCM kina nguvu. Na kama ahadi zilikuwa na miaka kumi alibidi a specify ahadi hizi ni za muda huu na hizi hapa ni za muda huu na siyo kugeneralize mambo. Na sababu kubwa ya viongozi wetu kugeneralize mambo sana ni ili wakishindwa wapate sababu za kusema. Our leaders only have implied promises na specifics wana ziacha mpaka hapo watakapo ona hizo ahadi zinaelekea wapi.
 
Wabunge wanataka kushusha mzigo kwa Rais lakini ukweli wa mambo wale ambao hawajafanya lolote katika majimbo yao ndio wanaolalamika.Na ukiwachunguza ni wale ambao ni wajumbe wa bodi katika taasisi mbalimbali ambao pamoja na kuwa katika kamati za bunge.Muda wao wa kukaa majimboni mwao ni mdogo.hivyo hawakufuatilia utendaji wa halmashauri zao.Fedha nyingi za miradi mbalimbali zimepelekwa katika halmashauri za wilaya katika kipindi hiki cha awamu ya nne.wabunge walitakiwa kuwabana madiwani kuhakikisha fedha hizo zinawaendea walengwa.
 
Nakumbuka baada JK kuchaguliwa kuwa mkuu wa nchi alifanya mahojiano na idhaa ya kiswahili ya BBC na Tido Mhando alimuuliza kuhusu mlima wa ahadi alizowaahidi watanzania katika kampeni zake na JK, akajibu namnukuu:

"....si maneno matupu...ni ahadi ambazo tutazitekeleza...naogopoa kuja kusutwa baadae...."

Labada tusioona utekelezaji huo hatuna macho lakini ndo mwaka unaishia huo na maisha bora yamekuwa bora kuishi tu...
 
Ahadi zingine zitamkaanga,kawahaidi wananchi wa Kyela rami kwenda Matema beach kabla ya Uchaguzi,sijui itakuwaje yangu macho!
 
Kwa kifupi ni kwamba ametulostisha, hakuna aliloweza kulikamilisha. Hata hili swala la ufisadi anashindwa kuwafunga wahusika wakati wanajulikana.

Tatizo watanzania ni waoga sana, tunaogopa mabadiliko si jambo la kushangaza kuona anapata kura nyingi tu 2010
 
Keshaanza kuchaguliwa tayari. Labda kama baadhi yetu hatufuatilii taarifa za vyombo vya habari. Kazi ipo kwa Wabunge kama upinzani utapata watu kama tulionao humu JF.
 
Watanzania tuna haja ya kufanya mabadiliko, kukaa na chama kimoja madarakani kwa miaka zaidi ya 40 ni tatizo. Tunachotakiwa ni kuhakikisha SISIEMU inakosa nguvu nani ya Bunge. Ukiangalia wabunge wengi walikuwa wakiga kelele kuhusu Budget lakini hao hao ndio walio ipitisha, sasa hii ni akili au matope???
 
kpleo.jpg


MWANANCHI.

wadau JF,
Wakati huu tunasikia kelele nyiiiiiingi bungeni kutoka kwa Waheshimiwa wabunge,mnadhani wanapwaga kwa ajili ya njaa za walala hoi????
think again.
 
Ha!ha!ha!....jana orodha ya wabunge walikuwa wanataka kuchangia bajeti ya PM ilikuwa haifiti kny muda ulioopo.....!now naona hawajamaa hawataki kabisa kucheka na kima!
 
Wamechelewa sana,watawajibika tuu kwa wapiga kura hata kama hawatabadiishwa lakini angalau adhabu ya kuzomewa wataipata
 
Wamechelewa sana,watawajibika tuu kwa wapiga kura hata kama hawatabadiishwa lakini angalau adhabu ya kuzomewa wataipata
Kwa hivyo unawahakikishia wasiwe na wasiwasi just kuzomewa tu lakini bunge lijalo hataliona kwenye tiviii?
 
Kwa hivyo unawahakikishia wasiwe na wasiwasi just kuzomewa tu lakini bunge lijalo hataliona kwenye tiviii?

Sasa mkuu Juni, umesahu kwamba uchaguzi wa Tanzania anaye amua nani mshindi ni NEC si kura yako?

Kura utapiga kwa unaye mtaka, lakini atatangazwa wanaye mtaka ama waliye ambiwa wamtangaze! Hujasikia Mgosi Makamba kaisha acha maagizo B'mlo nako watangaze tu?
 
Sasa mkuu Juni, umesahu kwamba uchaguzi wa Tanzania anaye amua nani mshindi ni NEC si kura yako?

Kura utapiga kwa unaye mtaka, lakini atatangazwa wanaye mtaka ama waliye ambiwa wamtangaze! Hujasikia Mgosi Makamba kaisha acha maagizo B'mlo nako watangaze tu?
Yakhe mm sina habari,nilipitikiwa kabisaaaa kama nchi inaongozwa kijeshi sasa, yaani Lt. Col.Rtd. Yussuf Makamba ameshatoa agizo...!!!!
 
JF, nimeamua kuuliza hili swali baada ya kuona threads kadhaa za siasa hapa zikuzungumzia habari ya Uchaguzi 2015, au Membe anataka Urais 2015. Ni vizuri kuanza kuzungumzia mambo ya namna hiyo mapema ili tuweze kujua kama wenye nchi ni nani tunayemtaka kuwa Kiongozi wetu, kura si ni yetu bwana!
Lakini kinachonishangaza ni kwamba tunaongelea 2015 kama vile tumemaliza kupiga kura 2010 na Rais tunaye tayari. Hili swala sijui mnalionaje wenzangu lakini isije ikafika 2010 hapa halafu tukaanza kujiuliza kama wenzetu wa Iran "WHERE IS MY VOTE?". Je tunaye Rais tayari kwa 2010-2015? Tuna uhakika kiongozi wetu huyu ambaye tumemchagua anafanya yale tuliyomtuma afanye?
Kazi kwetu!
 
watu wamezungumzia hiyo ya membe 2015 kwa sababu ndiye pekee aliyejitokeza mpaka sasa[angalau].kuhusu ile ya 2010 uchaguzi upo na na mwananchi yeyote mwenye sifa na wachama chochote[ikiwamo ccm]anaweza kugombea,mkuu mbona hapa JF watu wameshajadili suala hili sana tu[mfano kulikuwa na thread ya kuhusu EL kujiandaa 2010 kurudi madarakani]
 
Back
Top Bottom