The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Mi naona safu hiyo ibaki hivyo hivyo, ila rais abaki huyu wa sasa, lowasa apewe wizara ya maliasili na madini ili amalize kazi (ufisadi) aliyoianza miaka ya mwanzoni mwa 90 na alipokuwa waziri mkuu. Pia wabunge wote wa CCM kasoro wale waliokuwa kwenye kamati ya Dr. Mwakyembe wawe mabalozi wa TZ nchi za nje!!
 
CCM waanza kampeni za Kikwete 2010 wamchangia Sh milioni za fomu

kikwetecapaign.jpg

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ameanza kupigiwa upatu ili awe mgombea pekee katika uchaguzi mkuu 2010.Na Lilian Lugakingira, Bukoba

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeanza safari ndefu ya kumnadi Rais Jakaya Kikwete ili awe mgombea pekee katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, na tayari wilaya ya Bukoba Mjini imetoa hundi ya Sh1milioni za kulipia fomu yake ya kuwania nafasi hiyo.

Hundi hiyo ilitolewa jana na Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Bukoba Mjini kwa maelezo kuwa umeridhishwa na uongozi wa Kikwete katika kutekeleza na kutimiza ilani ya CCM, na hivyo kuungana na jumuiya nyingine, vikundi na watu mbalimbali waliojitokeza kuanza kumkapenia Kikwete.

Hata hivyo, katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliiambia Mwananchi jana kuwa hajui kwa nini jumuiya hiyo ya vijana wa chama chake imefanya hivyo na kwamba atawatafuta ili kupata ukweli na sababu za kitendo hicho.

"Niano msimamo wa chama, lakini siwezi kusema kwa sababu sijajua wamefanya nini. Bila shaka wanayo sababu," alisema Makamba baada ya kuuliza maswali mengi kuhusu kitendo hicho cha UVCCM Bukoba.

Katika halfa iliyofanyika mjini hapa, mwenyekiti wa UVCCM wa Bukoba Mjini, Chifu Kalumuna alimkabidhi mwenyekiti wa CCM wilayani Bukoba Mjini, luteni mstaafu Ally Shamte hundi ya fedha za kuchukulia fomu hizo.

Katika hafla hiyo, Kalumuna pia alimkabidhi mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki hundi ya Sh 100,000 kwa ajili ya kuchukulia fomu za kuwania ubunge katika uchaguzi huo.

Akizungumzia sababu za kutoa fedha kwa Kikwete na Kagasheki kwa ajili ya kuchukulia fomu, katibu wa vijana wa Bukoba Mjini, Yusuph Kaliat alisema wamefanya hivyo kutokana na kuridhika na ufanisi katika utekelezaji wa ilani ya CCM.

“Sisi kama vijana na nguzo ya taifa, tumeamua kutoa zawadi hiyo ili viongozi hao waendelee kuongoza, kila mmoja kwa nafasi aliyokuwa nayo,” alisema Kaliat katika hafla hiyo
iliyohudhuriwa na viongozi kadhaa wa CCM na UVCCM, akiwemo Kagasheki.
Chifu Kalumuna alikabidhi hundi zote mbili kwa Balozi Kagasheki ambaye naye alimkabidhi Shamte.

Hakuna maelezo yaliyotolewa kwa nini UVCCM wilaya ya Bukoba imeamua kutoa fedha hizo sasa, ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya mchakato wa uteuzi za majina ya wagombea na kuanza kampeni.

Kwa kawaida, CCM ina kipindi chake cha kuanza kampeni za ndani kwa wagombea wa nafasi zote za kuanzia serikali za mitaa, udiwani, ubunge na urais, lakini muda rasmi unaoruhusiwa na Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya kuanza kampeni ni miezi minne kabla ya tarehe ya uchaguzi.
Uchaguzi mkuu utafanyika mwezi Agosti mwaka 2010.

Kitendo cha wilaya hiyo kutoa fedha kwa ajili ya kuchukulia fomu kinaelekea kuwa ni mkakati mpya wa kumnadi Kikwete pamoja na Kagasheki, ambaye hivi karibuni alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema hatawania kiti hicho tena.

Fedha hizo za jumuiya ya vijana ya Bukoba Mjini ni sehemu ya kampeni kadhaa ambazo zimekuwa zikionekana katika miezi ya karibuni kumpigia debe Kikwete, ambaye alipata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa mwaka 2005.

Hivi karibuni Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Manyara ulimpendekeza Kikwete kuwa mgombea pekee wa nafasi ya urais katika chama chao cha CCM.

Umoja huo ulitoa msimamo huo Mei 30 katika mkutano mkuu wa mkoa uliofanyika kata ya Magugu wilayani Babati ambako mgeni rasmi alikuwa katibu mkuu wa UWT, Hasna Sudi Mwilima.

Risala ya akina mama hao iliyosomwa na katibu wa mkoa, Venosa Mjema ilisema wamenufaika zaidi na uongozi wa Rais Kikwete tangu alipoingia madarakani mwaka 2005.

Pia mkoa wa Rukwa ulionyesha kuridhishwa na uongozi wa Kikwete katika hafla ya kuchangisha pesa kwa ajili ya ujenzi wa shule za mkoa huo.

Katika hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam na ambayo mgeni rasmi alikuwa Kikwete, kiasi cha Sh 1.4bilioni kilichangwa kwa fedha taslimu au ahadi.

Wanachama wengine wa CCM waliowahi kutoa kauli za kutaka Kikwete awe mgombea pekee wa chama hicho ni pamoja na makamu mstaafu wa rais, Samuel Malecela, mwenyekiti wa zamani wa CCM mkoani Dodoma, Pancras Ndejembi na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoani Dar es Salaam, Mzee Hemed Mkali.

Baada ya wazee hao kutoa kauli hiyo mapema mwaka huu, Mbunge wa Sumve, John Shibuda alidai kwamba atachukua fomu kuwania urais mwaka 2010. Shibuda pia alikuwa miongoni mwa wana-CCM 11 waliochukua fomu kuwania urais mwaka 2005.

Wengine ni makamu mwenyekiti wa zamani wa CCM, Malecela, waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof Mark Mwandosya, Balozi Patrick Chokara, Balozi Ali Karume, Dk Abdallah Kigoda, Dk William Shija, Dk Salim Ahmed Salim na Idd Simba.

Akionekana kunogesha kampeni za chini kwa chini hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Shinyanga, Rais Kikwete mwenyewe alisema haoni sababu kwa nini akina mama waliofaidika na mradi huo wamnyime kura mwakani. “Nasema, kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kupata usingizi… mimi sioni kwa nini akina mama walionufaika na mradi huu waninyime kura alisema Kikwete huku akishangiliwa na akina mama waliofika kwenye uzinduzi huo.
Nice drop!
Playa!
Now! it'z tyme 2 go!
15p49a8.gif

 
Mjomba Eeeh!
Ulipoanguka Jangwani walisema ni uchovu wa kampeni mfululizo bila mapumziko. Hatukuhoji sana
Sasa tumesikia tena na huko Magogoni unaanguka anguka hovyo. Eti unashindwa masharti ya mwezi mchanga! Toba
Si siku zote mwasema; utamaduni wetu vijiti kupokezana?! Sasa vp wewe wang'an'gania?
Kuachia kiti kitamu si upumbavu; Afya ni bora kuliko cheo, waache nao wachukue tu......!
Natania tu Mjomba; Nikipata nauli nitakuletea wapiga dua.
 
Kwamba Kikwete gonjwa inajulikana, and I am not talking about the ngoma reports which are unverifiable.

Kwamba anaanguka anguka Ikulu is news. Vi nzi vinaweza kuthibitisha labda.

Actually hii ilikuwa bonge la point ya kutokea, akawa ex president baada ya term moja kwa sababu za kiafya na kujipumzikia kwenye mansion lake, bila ya kudanganya kuhusu hizo sababu za kiafya. Maana nchi imemshinda, afya matatizo, basi tabu tupu!
 
haya sasa mmeanza kuchafua hii blog.haya ya jk kuanguka ikulu mmetoa wapi. Hivi nyinyi tu mmnamacho na wengine hawana,
nadhani tuanze kuwa na mashaka na tabia hii mana waungwana wanasema ukicheza na nguruwa atakufuata msikitini. Sasa hili naona litatupeleka pabaya.
Mwanangu thibitisha usemi vyenginevyo blog hii bye bye, halafu tutasema tumeonewa.
 
Eee Bwana eee!!! Du, du, du, dudu!!! Tufanunulie tafadhali, cha mno???

La muhimu sasa, nichangieni nipate nauli nimpelekee Mjomba dawa.
Dawa yenyewe haiku kokote kule zaidi ya kwake aliyekuwako, aliyeko na atakayekuwako.
 
haya sasa mmeanza kuchafua hii blog.haya ya jk kuanguka ikulu mmetoa wapi. Hivi nyinyi tu mmnamacho na wengine hawana,
nadhani tuanze kuwa na mashaka na tabia hii mana waungwana wanasema ukicheza na nguruwa atakufuata msikitini. Sasa hili naona litatupeleka pabaya.
Mwanangu thibitisha usemi vyenginevyo blog hii bye bye, halafu tutasema tumeonewa.

Huyo JK hapa kaingiaje??
Mimi nazungumzia Mjomba, na si mjomba wako bali Mjomba wangu.
 
Mpwa salam
Na asante kwa kufikiria hali ya mjomba wako. Nimeamua kukuandikia kukupa ushuri ili uweze kumsadia, sitaweza kupata nauli nije nimueleze, basi ukiona mtu anelekea huko kwake basi mpe maagizo yangu.

mwezi mchanga huweza kudhibitiwa, ingawa wataalam wengi wanasema umri unamata sana, lakini mwambie Mjomba wako anicontact niao mzizi unaweza kusimamisha atahari za mwezi mchanga, swala la mwezi kuchomoza na mjomba wako kujikkamua, kugeuza macho na kutoa povu mdomoni lipo ndani ya uwezo wetu. Ugonjwa ukicheleweshwa huenda kichwani, na wasi wasi kama mjomba wako ataweza kuwa katika form na kumaliza kipindi cha pili cha mkataba na mwajiri wake, kwani haka kamwezi kataathiri perfomance yote. Kuna dawa za wachina zina punguza madhara yake, lakini zitamuongezea uzito usiotarajiwa, baadaye mtaona anapoteza rangi ya kung'aa usoni na kuvia kwa rangi nyeusi. Kutokana na kuingilia ufanyaji kazi ya ubongo, basi mdokeze mwajiri wake kuwa akimaliza kipindi cha kwanza cha makataba basi asimwongeze kipindi kingine.

Pia wafikishie salam majirani zako, waambie yule Major Jenerali aliyekuwa anamtaka mwajiri ampe nafasi badala ya mjomba, aitishe kikao cha familia wakubaliane nani afikiriwe badala yake kwa kupewa nafasi ya kutunza mji badala yake, maana naona upepo wa kwa yule dada wa kisukuma kujirudia tena kama haitaletwa sura mpya kwenye majadiliano ya mkataba.

Asante
Nyumba Ndogo
 
Mpwa salam
Na asante kwa kufikiria hali ya mjomba wako. Nimeamua kukuandikia kukupa ushuri ili uweze kumsadia, sitaweza kupata nauli nije nimueleze, basi ukiona mtu anelekea huko kwake basi mpe maagizo yangu.

mwezi mchanga huweza kudhibitiwa, ingawa wataalam wengi wanasema umri unamata sana, lakini mwambie Mjomba wako anicontact niao mzizi unaweza kusimamisha atahari za mwezi mchanga, swala la mwezi kuchomoza na mjomba wako kujikkamua, kugeuza macho na kutoa povu mdomoni lipo ndani ya uwezo wetu. Ugonjwa ukicheleweshwa huenda kichwani, na wasi wasi kama mjomba wako ataweza kuwa katika form na kumaliza kipindi cha pili cha mkataba na mwajiri wake, kwani haka kamwezi kataathiri perfomance yote. Kuna dawa za wachina zina punguza madhara yake, lakini zitamuongezea uzito usiotarajiwa, baadaye mtaona anapoteza rangi ya kung'aa usoni na kuvia kwa rangi nyeusi. Kutokana na kuingilia ufanyaji kazi ya ubongo, basi mdokeze mwajiri wake kuwa akimaliza kipindi cha kwanza cha makataba basi asimwongeze kipindi kingine.

Pia wafikishie salam majirani zako, waambie yule Major Jenerali aliyekuwa anamtaka mwajiri ampe nafasi badala ya mjomba, aitishe kikao cha familia wakubaliane nani afikiriwe badala yake kwa kupewa nafasi ya kutunza mji badala yake, maana naona upepo wa kwa yule dada wa kisukuma kujirudia tena kama haitaletwa sura mpya kwenye majadiliano ya mkataba.

Asante
Nyumba Ndogo


Nyumba Ndogo,
Nakushukuru sana kwa nia yako ya dhati kuokoa maisha ya Mjomba wangu. Nimefurahi kusikia kuwa una mizizi ya kumtibu. Nakuwa na faraja kuwa panapo majariwa, mjomba anaweza kurudia hali yake ki-afya. Tunajitahidi kwa kadri kumshawieshi mwajiri ampumzishe Mjomba kwa kutomruhusu kuchukua awamu ya pili. Ila na mjomba naye kiburi. Tatizo zaidi uongo wa wapambe. Maana wao wanapata ugali hawajali afya ya mjomba wetu. Badala ya kumlipia ada ya cheti hospitali au bima ya afya wanachangia hela ya kurefusha matatizo “Part II”
Ni kweli zipo dawa za Mchina wa lile temple la pale Magomeni Mapipa. Na anazitumia sana hasa kabla ya kwenda safari. Kwa namna Fulani tunashukuru maana kama isinge kuwa hizi dawa, angekuwa anaanguka hata ugenini. Najiuliza angeanguka unyamwezini ingekuwaje?!
Kama utaangalia vizuri, utabaini tayari uso wa mjomba umeanza kupoteza rangi ya kung'aa kwake kwa asili.
Ila Nyumba Ndogo sikukupata vizuri kuhusu Major Jenerali na ujumbe mzima wa dada wa kisukuma. Naomba nieleweshe hata kwa PM
Salamu kwa majrani zimefika,
Siku njema,
Wako aliyembali na upeo wa mjomba wake,
Omutwale
 
Duh, huu utani mbona umeka kama ukweli? Kwani mjombako lile jipete analovaa halimsaidii?
 
Du ama kweli vichwa vya panzi watabaki gizani, labda atokee mtafasiri awaokoe!! Namuona jirani wa mjomba anapiga domo tu!!
 
jk kama anaumwa apumzike sio lazima yeye...maana alipania sana sana .................si ameshapataaa?ameshauza sura inatosha....
 
hivi anaitaji mchango kweli Rais Kikwete au mntaka kuchukua tu hela mpaka za ma bibi wa watu maskini ebu kuwa na huruma sema tu si hitaji mchango wenu nipe kura yako inatosha hiyo chenji babu kanunue kuku ujifurahishe.
 
This time there will be no open loop for memos to the bot to issue campaign funds
 
Mkataba wa kuugharimia uchaguzi mkuu wa 2010, wenye thamani ya zaidi shiling Bilioni 40, umesainiwa leo kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP ambapo fungu la nchi wahisani zimeunganishwa kwenye kapu kuu la kugharimia uchaguzi huo.

Mkataba huo umehusisha Tume za Uchaguzi za NEC na ZEK kusaidiwa kuendesha uchaguzi huru na wa haki huku vyombo vya habari vikipewa nafasi kama mdau muhimu kwenye zoezi zima la uchaguzi huru na wa haki.

Sherehe za utiaji saini huo, zimefanyika katika ukumbi wa UNDP huku ukishuhudiwa na mabalozi, wawakilishi wa vyama vya siasa, maofisa wa serikali na kundi kubwa la la waandishi wa habari.

Mgeni rasmi ni Waziri wa Mambo ya Nje, Benerd Membe.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom