Tanzania imekuwa ikigubikwa na majanga ya wizi wa mali za umma kupitia makundi ya kialifu na baadhi ya wanasiasa. Mpaka sasa hivi kuna hali ya kuchelea katika kupambana ‘kikweli' na janga hili. Tukielekea Uchaguzi wa 2010, Je kuna Mwanasiasa mwenye ubavu wa kutupa karata ya kuanzisha ‘Kunde la Ng'e' kupambana na majanga haya? [habari zaidi kuhusu kundi hili la ng'e soma hapa: http://en.wikipedia.org/wiki/Scorpions_(South_Africa)]
Dondoo: Nimelichulia kundi la Ng'e la Afrika Kusini kwa kazi yake nzuri iliyofanywa kuanzia mwaka 2001 mpaka pale lilipovunjwa mwaka huu. Kundi hili lilikuwa mwiba mchungu kwa wabaka uchumi, wanasiasa mabazazi et al.