NOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO! msekwa he is right kikwete amefanya mambo mazuri sana sana bila yeye nchi hii pangekuwa hapakaliki hebu fikiria angeruhusu Mkapa ashitakiwe au angesema mifisadi yote iende mahakamani na isipewe hata dhamana kwa sababu wameihujumu nchi unafikiri ni nini kingeendelea???????????????????
Amefanya mazuri kwa watu matajiri wenye pesa zao na kwasababu nchi hii inamilikiwa na wenye fweza msekwa yuko right....., naamini mimi na wewe hatujaona mazuri yake kwa sababu sio makada wa CCM, sio majambazi, sio wauza madawa ya kulevya, sio mafisadi hata tukifa kikwete hata kuja kwenye msiba wetu.. yani tupotupo tuuu.
Alivyosema CCM inakusudia kumpitisha Kikwete alitaja ni kikao gani kilifanyika na uamuzi huo ulifikiwaje?
Ikiwa chama kinaruhusu watu kuwania uarais, chama kitakusudiaje kumpitisha mgombea mmoja bila ya kuwasikiliza wagombea wengine? Hawawezi hata kufanya a sham process? Sasa ukifika muda wa kuwasilisha majina na Shibuda akisema alipigwa vita na viongozi wa juu wakiwamo kina Msekwa wataweza kujitetea kwamba walikuwa neutral na objective katika process?
Tunaendesha mambo kienyeji kweli!
Ushindani wa kweli kutoka kwa Shibuda?!
Majina tunayo lakini si busara kuyataja sababu ya usalama wao. Nadhani lililo la busara kwa wakati huu ni kuweka wazi mbele ya Watanzania kuwa mpangaji wetu wa sasa pale ikulu HATUFAI na hivyo tusimpatie miaka mingine mitano. Amechafua kuta za nyumba yetu kwa kupikia ndani ya nyumba kutumia kuni za miti mibichi. Yaani kuni (mawaziri) wa kupikia chakula watoto wake (Watanzania) ni wabichi (washikaji). Mpangaji mwenyewe (Rais) haoni hilo (uwezo mdogo). Nyumba yetu (Tanzania) inazidi kuharibika rangi (umaskini) kwa moshi (ubadhirifu/ufisadi).
Nadhani tuthibitishe hayo kwanza. Watanzania wajue muungwana hatatufikisha kwenye kauli mbiu yake ya maisha bora kwa kila Mtanzania ili mwaka 2010 tutafute mpangaji mwingine. Let's be serious. Yes, we can.
Mimi nampendekeza Salim Ahmed Salim,Makamo Asha Rose Migiro na Waziri mkuu awe John Pombe Magufuli.