ELNIN0
JF-Expert Member
- Nov 26, 2009
- 4,161
- 1,460
Waungwana, hivi huyu Maximo ni hakuna halichotufanyia watanzania au tulikuwa tumeweka IMANI KUBWA SANA KWAKE. Nadhani tujaribu kuangalia mahali alipotukuta ndipo tulipo? kama jibu ni ndiyo BASI HANA JIPYA, kama jibu ni hapana, je ametusogeza mbele au ameturudisha nyuma. nadhani kama ameturudisha nyuma basi hana sababu hata ya kuaga ni kuchapa lapa kwa kwenda mbele kama ametusogeza mbele basi tunayo sababu ya kuangalia hiyo hatua utuliyosogea tulistahili kwa hiyo hatua au la. Haisaidii kila siku kuhoji swala la kaseja, boban na chuji kuwezpo stars, sitaki kuamini kwamba matokeo mabaya inayoyapata stars ni kukosekana kwa hao wachezaji watatu. Naamini kila kocha anachagua wachezaji kutoka na mfumo anaotaka kuutumia, na vilevile hakuna kocha ambaye atachagua wachezaji ili timu ikose ushindi.
Tujaribu kunyoosha vidole kwenye vilabu vyetu kwanza, vipi mafanikio ya vilabu vyetu katika michezo ya kimataifa? Kama vilabu havifanyi vizuri sidhani kama timu ya taifa itafanya vizuri kwani ndio hao hao wacheza tutakaokuwa nao kwenye national team.
Mkuu, with all resorces and support given to him, he is waste.