The Rise and Fall of Marcio Maximo...Discuss.

Namuonea huruma Maximo kufundisha watu wasiokuwa na pre-requiste ya mafunzo anayotoa. Tanzania hata kama tutaletewa makocha wawili walioandaa timu za taifa za Italy na Ujerumani wakati wa kombe la dunia 2006, bado tutabaki kuwa "mbuzi wa shughuli tu."

Wachezaji wetu wengi hawana ile discpline ya training; wanamfundishwa hiki, wao wanafanya kile. Kosa letu ni kuwa tunaokota wachezaji wetu wengi kutoka mitaani badala ya kuwachukua kutoka mashuleni wakiwa wamejengwa kuwa trainable. Utagundua kuwa wachezaji wetu wazuri wa zamani miaka ya sabini na themanini walitokana na michezo ya mashule ya sekondari na msingi; leo hii hakuna kitu cha namna hiyo tena labda kama kimeanza jana tu. Bila kuwa na foundation nzuri ya kupokea training, hapa hatutapa kitu kwenye timu yetu. Tukumbuke kuwa mpira ni teamwork; inawezekana kuwa kuna wachezaji wawili au hata watano ambao ni trainable na ni wazuri sana, lakini wakishachanganywa na kundi lile jingine basi timu yote inakuwa hivyo tena.
 
kheee kumbe tunaye mpaka July 2010?huyu alikuwa ni wa kuondoka now..July ni mbali sana
 
Wametangaza leo.anaondoka july.

Maximo aliajiriwa kutupeleka kwenye fainali za African Cup na aliposhindwa tulisema aondolewe haraka sana lakini kwa sababu ya Fisadi moja anaekaa pale magogoni kuwa na uswaiba ndio bado anadunda tena hadi mwakani. Kazi kweli kweli pesa ya walipa kodi haina mwenyewe. Tena hata aibu hawana watakuja humu na kusema hiyo sio pesa ya walipa kodi! Sijui waliichimba wapi?
 
Wabongo kama kawaida yetu tunataka mafanikio ya haraka haraka katika soka bila kuwekeza. Soka ni kama shughuli nyingine, inahitaji uwekezaji sahihi na wa muda mrefu ili uanze kupata mavuno mazuri. Haitoshi kufikiri kuwa tatizo la msingi ni kocha. Tunahitaji kuanza kukuza vipaji toka shule za msingi ili baadaye waweze kuchezea kilabu na hatimaye taifa. Aden Rage aliwahi kusema kuwa "watanzania wanataka kwenda peponi bila kufa" - akiwa na maana kuwa hatutaki kuingia gharama za kukuza soka lakini tunataka mafanikio katika soka. Kocha Maximo amejitahidi kwa kiasi chake licha ya mapungufu kadhaa aliyonayo. Kiwango cha timu ya taifa kwa kiasi fulani kimepanda ukilinganisha na kabla ya ujio wake. Tangu atue nchini, Stars imecheza mechi 57 chini ya Maximo na kufungwa na kutoka sare mechi 17, hivyo kushinda mechi 40 - hii ni sawa na ushindi wa asilimia 70. Tukilinganisha na makocha waliotangulia, naweza kusema kwa kiasi kikubwa amejitahidi. Kama tusipobadili mfumo wa kuendesha soka kwa kuanzia chini, tutaendelea kubadili makocha huku tukiendelea tukisuasua.
 
Wametangaza leo.anaondoka july.

Duh! mzee mbona unakatisha tamaa hivyo?? Yaani mimi nilijua ndo ameshafungashiwa vilago, kumbe hadi july? Si tutaendelea kulizwa vilevile tu, tena sasa ndo atavurunda zaidi. noma sana!
 
Wabongo kama kawaida yetu tunataka mafanikio ya haraka haraka katika soka bila kuwekeza. Soka ni kama shughuli nyingine, inahitaji uwekezaji sahihi na wa muda mrefu ili uanze kupata mavuno mazuri. Haitoshi kufikiri kuwa tatizo la msingi ni kocha. Tunahitaji kuanza kukuza vipaji toka shule za msingi ili baadaye waweze kuchezea kilabu na hatimaye taifa. Aden Rage aliwahi kusema kuwa "watanzania wanataka kwenda peponi bila kufa" - akiwa na maana kuwa hatutaki kuingia gharama za kukuza soka lakini tunataka mafanikio katika soka. Kocha Maximo amejitahidi kwa kiasi chake licha ya mapungufu kadhaa aliyonayo. Kiwango cha timu ya taifa kwa kiasi fulani kimepanda ukilinganisha na kabla ya ujio wake. Tangu atue nchini, Stars imecheza mechi 57 chini ya Maximo na kufungwa na kutoka sare mechi 17, hivyo kushinda mechi 40 - hii ni sawa na ushindi wa asilimia 70. Tukilinganisha na makocha waliotangulia, naweza kusema kwa kiasi kikubwa amejitahidi. Kama tusipobadili mfumo wa kuendesha soka kwa kuanzia chini, tutaendelea kubadili makocha huku tukiendelea tukisuasua.
Hilo ni sahihi kabisa lakini kocha naye ana mchango wake, hivi uliona Simba walivyovurunda mwaka jana? Baada ya kubadilishiwa kocha siunaona mambo yalivyobadilika? sasa wamewekeza nini? akina mgosi, haruna, nyagawa ni walewale!
 
Nani kasema kuwa stars kashinda mechi 40???!!!!.Umesahau kwamba katika hizo mechi 40 kuna sare nyingi zaidi ya ushindi!!!! Nafikiri sare ni 30 na ushindi ni 10.
 
Hilo ni sahihi kabisa lakini kocha naye ana mchango wake, hivi uliona Simba walivyovurunda mwaka jana? Baada ya kubadilishiwa kocha siunaona mambo yalivyobadilika? sasa wamewekeza nini? akina mgosi, haruna, nyagawa ni walewale!

Mpashe huyo...
 
Jamaa analipwa 15,000$ kwa mwezi!!.....mimi nafikiria sababu muda umebakia mfupi...watafute kocha faster ili by jan amkabidhi team...hatumtaki hana jipya!!
 
hayawi hayawi hatimaye yamekuwa,
sasa maximo anaondoka rasmi february 2010 at least tupate faraja na timu yetu ya taifa ianze kufanya vizuri na kuleta vikombe.

Huyu baba kocha/kimeo wa ki-brazil alitukera sana mpaka tusijuwe cha kufanya(hasa ikichukuliwa TULILETEWA KAMA ZAWADI YA URAIS) tukaamua kumwachia MUNGU hatimaye kilio chetu wapenzi na wadau wa soka la kitanzania kimesikika..sasa tutapumzika...UENDE UENDAKO MAXIMO HUNA LOLOOOTE
 
umefurahi eeh?!
 
umefurahi eeh?!

Kaka nitakuwa muongo nikisema SIJAFURAHIA MAXIMO KUONDOKA...nimefurahi sanaaa pamoja na watanzania wenzangu woote wenye mapenzi ya kweli na timu yetu na taifa letu kwa ujumla...pole sana kama wewe hujafurahia hili.
 
na unazungumziaje kujituma kwa wachezaji wetu wakiwa mazoezini?ulevi,matumizi ya madawa ya kulevya(bange)?kitu gani kikifanyika kulikabili hili UTAFURAHI?
 
haya sasa mziray, mkwasa,julio na wengineo wazao...tunawapa 1st priority kwa ajira hii mpya iliyotangazwa...

na nyie kina tenga...mtuletee tena kimeo kama maximo ndio mtatujua sie ni kina nani...tafuteni makocha wazuri wapo telee...kina scolari, mourinho, wenger sir, fergie, pep guardiola na wengineo...sio mnakimbilia walima matunda wa brazili au mashujaa wa vita wa serbi...cheap stuff
 
Back
Top Bottom