The Rise and Fall of Marcio Maximo...Discuss.

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Marcio Maximo amesema atatumia ujio wa Kombe la Dunia kuwajenga kisaikolojia wachezaji wa timu yake watambue kuwa na wao wanastahili kutwaa kombe hilo.

Alikuwa anasubiri nini siku zote?

Hizi ni ndoto za mchana au kuna dalili za uwezekano wa Tanzania kutwaa kombe la Dunia siku za usoni?
Dalili ya mvua ni mawingu.
Mbona sioni mawingu yoyote hadi sasa?
Wadau mwasemaje?

 
kitu cha kwanza kama napata nafasi ya kuingia TFF ni kuvunja mkataba na MAXIMO hana jipya
 
me nahisi mpira si fani yetu, nadhani tujikite zaidi kwenye riadha maana imeshaonekana mpira hata hela ikiwa nyingi na facilities zikiwepo bado hamna kitu mfano Canada, japan, qatar,na nchi nyingine hamna mpira huko lakini angalia Brazil mambo mswano
 
me nahisi mpira si fani yetu, nadhani tujikite zaidi kwenye riadha maana imeshaonekana mpira hata hela ikiwa nyingi na facilities zikiwepo bado hamna kitu mfano Canada, japan, qatar,na nchi nyingine hamna mpira huko lakini angalia Brazil mambo mswano
Tulime viazi........soka la nini wakati masikini tu sisi? huo mshahara wa maximo wangenunulia power tillers.....matrekta watu turudi shamba.
 
Maximo ni kocha wa aina ya pekee, anataka kuifanya Tanzania iwe ya kwanza kwenye FIFA ranking hata kama hatushiriki mashindano makubwa wala kuchukua ubingwa. Obrigado Maximo!!!!!!!
 
hivi jamani, ishu ni kwa vile analipwa na serikali au? kwa wafuatiliaji wa soka, Maximo kazidiwa kidogo sana na Santana aliyetimuliwa South, ni aina ya makocha ambao wanatengeneza 'make-shift' like teams, au kwa wale ALCHEMISTS, kwamba anatengeneza dawa, tester mgonjwa!!!...kwa mwendo huu hatufiki..nionavyo mimi huyu bwana apewe timu za vijana, labda ndio atatengeneza timu...otherwise, itakuendelea kuwa ni shauku tu na si mikakati...
 
hakuna kocha hapo takataka tupu...sitaki hata kuweaza kuwa maximo ni kocha..
 
Wewe kocha anateua kipa ambae ajacheza hata mechi moja.pia kiungo aliye juu kwa sasa ni banka,nsajigwa akwekishwa kabisa-hapa kama kufulia tumefulia sna maximo sio kocha kabisa ni mbabaishaji tu.muuza matikiti brazil.
 
ndo manake..muaza mapera na mchicha..kocha gani hana CV inayoeleweka,,ni sanaa tupu ..TZ bwana
 
Maximo ni mbabaishaji! Huyu alitakiwa atimuliwe mara baada ya kushindwa kuipeleka timu Ghana kwenye fainali za mataifa ya Afrika mwaka juzi. Uteuzi wake wa timu unatia shaka sana. Ana mambo ya kiswahili na chuki kwa wachezaji ambao sisi wenye nchi yetu ndio tunaona wanafaa kutuletea mafanikio katika soka. Anaacha kuwaita star players kama KASEJA, ATHUMANI IDDI na HARUNA MOSHI pasipo na sababu yoyote ya msingi. Aondoke timu apewe PATRICK PHIRI akisaidiana na SYLERSAID MZIRAY mtaona matokeo yake...
 
Mi naona ana akili nzuri. Anaendelea kujitengenezea ajira. Akili nzuri sana hiyo. Anahakikisha anatengeneza katimu ambako kanashinda kidogo na kulete matumaini, kisha anapangua tena! Ni kama fundi wa gari, ambaye anakarabati radiator vizuri tu, halafu analegeza oil system, gari ikidont unarudi tena kwake!
 
Maana ya timu ya taifa na kuwa kocha wa timu ya taifa.. ni kuwa unawaita wale wachezaji ambao wako katika kiwango cha juu... usi unawiata wachazaji kufanya majaribio au kwasaabu huwa wanakuabu... sio club ile kusema utamuinua mwingine... maximo anaifanya timu ya taifa kama club inayoshiriki ligi kuu... huwezi ukawaacha key players na kisha ukamuita mtu ambaye hajacheza mechi hata moja.. hao akina owen huko england wanaomba kila siku wapangwe wafanye vizuri..

We want RESULT now and NOt Strategies... tooo much Broken Promises

Tanzania bwana kila kitu hatuko makini... yaani tunaishi kama watu wanaofanyiwa majaribio...

**************************
ISHI KAMA MTU ANAYECHEZA DRAFT/CHASE... SIO KILA PENYE NAFASI UNASUKUMA KETE... UTAPIGWA SUPER
 
me nahisi mpira si fani yetu, nadhani tujikite zaidi kwenye riadha maana imeshaonekana mpira hata hela ikiwa nyingi na facilities zikiwepo bado hamna kitu mfano Canada, japan, qatar,na nchi nyingine hamna mpira huko lakini angalia Brazil mambo mswano

Hapo umenena mpwa; tunalazimisha fani tusiyokuwa nayo!!!
 
Back
Top Bottom