The Rise and Fall of Ancient Egypt: Tracing its Enduring Legacy in Western Civilization

Zulu Man Tz

Member
Sep 23, 2020
73
99
Alexander The Great harakati za kutawala Ulimwengu.

Ili uweze kufahamu zaidi ni jinsi gani Alkebulan (Bara la Afrika ya sasa) ilivamiwa na Wakoloni inakupasa kujua historia ya Mfalme Alexander The Great(Mgiriki) na siasa zake za kumiliki himaya mbalimbali Afrika na Asia.
Historia ya Alexander The Great.

Alexander The Great alizaliwa mwaka 356 BC katika Himaya ya Macedonia, sehemu hiyo kwa sasa ni Nchi ya Ugiriki. Alikuwa ni Mtoto wa Mfalme Philip wa II huko Macedonia na ***** aliitwa Malkia Olympia. Alexander akiwa na miaka 20 alimrithi Baba yake ufalme na akaanza kampeni zake za kupanua wigo wa himaya yake ya Macedonia.

Alexander alianza kwa kuvamia Tawala zote za Ugiriki (Greece City states) na kisha baadae kuangalia fursa ya kupanua utawala wake katika Himaya za Persia. Mnamo mwaka 334 BC Alexander alikatiza Hellespont (Kwa sasa inajulikana kama Dardanelles) ili kuivamia Persia. Alexander alishinda vita kwa mfululizo dhidi ya majeshi ya wapersia, vita maarufu ilikuwa ni vita vya Issus mnamo 333 BC na kutwaa miji ya Syria, Lebanon na Misri.

Alexander kufanikiwa kuwa Farao Mpya wa Misri.

Mnamo mwaka 332 BC Alexander The Great alifanikiwa kuichukua Nchi ya Kemet (Misri) kutoka kwa utawala wa kimabavu wa kipersia. Kuja kwa Alexander ilikuwa ni kama mkombozi kwa watu wa Kemet kutoka chini ya utawala wa wapersia. Alexander aliingia Misri kupitia Oasis za Siwa, alipata ushauri au unabii kutoka kwa kuhani wa kikemet ambaye Mungu Zeus- Amun aliongea kupitia uyo kuhani. Mungu Amun aliabudiwa karibia Nchi yote ya Misri na kuheshimiwa zaidi.
Oracle (Kuhani wa Kemet) alitoa unabii ya kuwa Alexander ni Mtoto wa Mungu Zeus-Amun, ambaye amepewa mamlaka ya kimungu mbele ya macho na mustakabhari wa wamisri. Hapo ndio inakuja nadharia ya Incarinition yaani Mungu Amun akavaa mwili akatenda makuu kimwili kupitia Alexander The Great.
Alexander alitawala mpaka uko Delta za Mto Nile Nchini Misri ambako alitengeneza mji maarufu kati ya miji ya Ulimwengu wa Kale zaidi uliofahamika kama Jiji la Alexandria. Pia Alexander alifanikiwa kutembelea mji wa kale wa Memphis ambako alitawazwa na kupakwa mafuta na kuwa Farao Mpya wa Nchi ya Misri. Baada ya kujihakikishia ushindi Misri akaanza kupanua wigo wa kutaka kuvamia Tawala za India na Asia ya kati.

Jinsi Alexander alivoheshimu Tamaduni za Misri.

Baada ya kuwa Farao wa Misri Alexander aliendelea kuheshimu desturi na Tamaduni za kale za watu wa Misri. Pia alitekeleza alama mbalimbali za Utamaduni wa wamisri na kufuata mitindo ya wafalme wa kimisri(Mafarao) wanavyopaswa kuishi. Kwa kufuata maelekezo ya makuhani wa wamisri wakale Alexander aliweza kutoa sadaka na Kafara zilizonona kwa miungu ya Kimisri hivyo ilimfanya aheshimu Dini za asili za wamisri aliowatawala.

Alexander alitumia Nguvu Kubwa katika kurekebisha Mahekalu yaliyoharibiwa vibaya wakati wa vita na kukusanya vitabu na nyaraka mbalimbali za wamisri katika jiji alilolijenga la Alexandria Nchini Misri. Jiji la Alexandria lilikuwa mwambao mwa fukwe za bahari ya Mediterranean lilikua kwa haraka na kuwa kitovu Cha ujifunzaji ambapo wanazuoni kutoka Ulimwenguni walifika hapo kuchota maarifa ya mtu mweusi wa Misri(Kemetian).

Baadhi ya Wanazuoni maarufu waliochota maarifa kutoka kwa Misri ya Kale.

Aristotle alikuwa ni mwanafunzi wa Plato ambae alizaliwa mwaka 384BC jiji la Stagira, kaskazin mwa Nchi ya Ugiriki kwa sasa. Aristotle alitumia mda wake mwingi wa maisha yake uko Athens na pia alitumika kama tutor (Mwalimu) kwa Mfalme Alexander The Great alievamia na kutawala Ancient Egypt (Kemet) na Dola za sehemu nyingine kipindi Cha utawala wake.

Mgiriki Pythagoras alisafiri mpaka kwa watabe na mafundi wa elimu enzi hizo huko Misri ya Kale(Kemet) waliobobea zaidi kwenye Hisabati, fizikia,kemia kiufupi sayansi kwa ujumla na falsafa. Pythagoras alipendelea kujifunza zaidi Hisabati na falsafa, mafundisho hayo alipata kutoka kwa makuhani wa Kemet. Pythagoras hakuwa peke yake alikuwa na anajifunza na walimu wengne kama Chaldeans. Huko Pythagoras ndiko alikopata maujuzi ya formula zake kwa kukopi maarifa hayo kutoka kwa ancestors wetu wa Misri.
Formula hizo ndizo wamisri walizitumia katika kujenga Makaburi ya mafarao (Pyramids).
Hahaha hatari mtu wangu Muafrika noma A²+B²=C² jamaa akapata umaarufu kwa kuiba Nakala za Mababu zetu. Ila mashuleni hautoambiwa ukweli kuhusu ilo ndio maana formula kwa baadhi ya watu hazikai kichwani, ebu fikiria ungeambiwa hiyo kanuni ndio kaivumbua mababu zako wa kale, siungekuwa na uchungu zaidi ya kujifunza na ww uvumbue kitu. Eeeh eeh iyo ndio "Matrix" ukweli hauaminiki ili uongo ndio unaoaminika zaidi.

Mgiriki Aitwae Archimedes alizaliwa Syracuse, Sicily huko Ugiriki yapata mwaka 287 BC. Akiwa na umri wa miaka 18 alipata udhamini (Scholarship) kwenda kusoma Nchini Misri katika Maktaba Kubwa ya Alexandria. Makuhani wa Kimisri walimfundisha Archimedes haswa Hisabati pamoja na fizikia na kumuelewesha nakala zote ambazo Mizimu ya misri iliitoa kupitia makuhani hao. Nalala hizo zilichorwa kwny mawe ya Makaburi ya mafarao (Pyramids).

Archimedes alikuwa mwepesi zaidi kwenye kujifunza na kushika elimu aliyofunzwa uko Jiji la Alexandria -Misri. Akitoka darasani akifika nje Archimedes alijukumbusha alivyofundishwa kwa kuchora chini ya ardhi kwa kidole, ustadi huo ulimpa kujiamini sana na kuzidi kuvumbua maarifa yaliyofichwa kimafumbo na Mizimu.
Baada ya kumaliza masomo yake Archimedes alirejea nchini kwao Ugiriki huko sasa akavumbua Archimede's Screw pamoja na ile kanuni yake ya buoyancy (Archimedes principle). Kipindi akiwa Misri, wamisri walitumia izo screw za miti kuteka Maji kutoka kwenye Mto Nile kwa ajili ya kilimo Cha umwagiliaji ila yeye alienda kuipeleka iyo teknolojia kwa Mara ya Kwanza Ugiriki na wakaikubali wakamuona ni mvumbuzi. Hali ya kuwa izo elimu alifunzwa na wamisri ila yeye pia alikuwa na taranta kwnye izo maeneo na ikapelekea kuvumbua vitu vingi mno.

Utawala mpya wa Ptolemy I Soter kwa Wamisri.

Ptolemy I Soter alikuwa ni mmoja wa makamanda shupavu na Rafiki wa karibu sana wa Alexander The Great. Baada ya kifo Cha Alexander 323 BC, Ptolemy alipambana na kamanda mwenzie wa Macedonia aliefahamika kama Diadochi ili kugombania kutawala Misri, Basi Ptolemy akawa Gavana wa Misri na uko ndiko ukazaliwa utawala wa Wafalme kutoka kwa kizazi Cha Ptolemy (Ptolemaic Dynasty) ambacho kilitawala Misri kwa takribani miaka 300.
Ptolemy I Soter baada ya kujua kuwa wamisri wana uhusiano Mkubwa sana na ndugu zao waliokwisha fariki (Mizimu) ambao ndio chanzo Cha mafanikio Cha wamisri wa kale kielimu,kijamii, kiutamaduni na kiuchumi pia. Akaona kwamba mbinu ya kuwatenganisha nao ni kuweka masanamu yake katika Mahekalu na masinagogi ya wamisri ili wamuabudu yeye na wasahau mila na utamaduni wao na yeyote aliyepinga aliuawa chini ya utawala wake.
Ptolemy alikuwa kamanda mwenye ujuzi mno hasa mbinu za kijeshi pamoja na ushawishi wa kisiasa hivyo ndivyo vilivomfanya kufanikiwa kuitawala Misri ya watu weusi wa kale. Katika utawala wa Alexander, Ptolemy aliifanya misri iwe mji mkuu wa ufalme wa Alexander The Great na kuwa kitovu Cha Utamaduni na elimu, kuvutia wasomi, watu wa sanaa kutoka sehemu mbalimbali ya ulmwengu wa zamani.

Katika utawala wa Ptolemy Misri ilizidi kuwa kitovu Cha commerce na biashara na uchumi wake ulitegemea sana kilimo Cha umwagiliaji, uvuvi na manufacturing. Ptolemy alipanua mipaka yake na kutawala mpaka baadhi ya sehemu ya Ufalme wa Nubia/Kushi kwa sasa ni Sudani ya kusini, Libya, na Palestina. Kutokana na Gavana Ptolemy kupendelea zaidi kudhamini mambo ya Architecture (usanifu majengo), literature(fasihi) na uchonganyi hasa masanamu.

Kuanzishwa kwa Maktaba Kubwa ya kale Ulimwenguni.

Ptolemy I Soter alipata umaarufu kwa kukusanya legacy za vitabu vyote na Nakala zote walizikuwa wanatumia watu wa Ugiriki, Roma, Misri, Kushi/Nubia/Sudan, Libya,Syria na sehemu nyingne walizotawala. Ptolemy ndiye alieanzisha Maktaba kubwa kabisa katika Dunia huko Misri ikiyofahamika kama Maktaba ya Alexandria, katika Maktaba hiyo ndio Vitabu na Nakala vyote vilihifadhiwa hapo walipora vitu hivyo katika falme walipovamia na walipotawala hasa Misri, Sudan na Libya. Maktaba hiyo ilipatikana katika jiji kuu la Alexandria ambalo lilikuwa makao makuu ya utawala ufalme wa uzao wa Ptolemaic.
Maktaba hiyo ilijengwa kwa ustadi mkubwa mno yenye majengo makubwa yaliyofuatana yakiwa na sehemu za usomaji, mabwalo ya mikutano, maabara za kisayansi, Vifaa vya utafiti na sehemu za kuhifadhia vitabu na nakala nyingi kutoka sehemu mbalimbali mwa Ulimwengu wa Zamani. Kwa makadirio Maktaba ilikuwa na vitabu vya kukunjwa, miswada na nyaraka mbalimbali takribani 400,000 mpaka 700,000. Maktaba ilivutiwa zaidi na wasomi nguli waliofika hapo Misri kujifunza kama vile Pythagoras, Homer, Plato, Aristotle, Euclid, na Archimedes.
Kuingia kwa Utawala wa Warumi Afrika.
Inakadiliwa mwaka wa 146 BC Mkuu wa Jeshi la jamuhuri ya Kirumi alieitwa Scipio Aemilianus Africanus alianza harakati za kuvamia Kaskazin mwa Afrika ili kupanua Utawala wa Kirumi. Haya mashambulizi yalijulikana kama vita vya Punic.
Kuingia kwa warumi katika maeneo ya Mediterranean walianza kuivamia Ngome/Ufalme wa Carthage ambayo kwa sasa ni Nchi ya Tunisia, Warumi wakafanikiwa kuiteka Ufalme wa Carthage na hapo ndio ikawa mwisho wa vita vya Punic. Kutokana na uhamasishaji na Nguvu za kivita Warumi baada ya kutawala hayo maeneo waliyapa majina kutokana na watawala wake. Basi Kaskazin mwa Alkebulan pakaitwa Afrika Kutokana na mtawala huyo Scipio Aemilianus Africanus. Ila pia kuna uwezekano mkubwa pia jina Afrika kwa sasa inatokana na kabila la Afri huko Tunisia au yote kwa pamoja.

Warumi kuvamia Misri ya Kale (Kemet).

Mnamo mwaka 30 BC utawala wa kirumi chini ya amri ya kamanda Octavian ambae baadae alifahamika kama Kaisari Augustus. Kamanda Octavian alieanzisha uvamizi na alifanikiwa kuichukua Misri kutoka kwa Wagiriki iliyoongozwa na Utawala wa watu wa ukoo wa Mfalme Ptolemy uliotawala Misri kwa kipindi Cha miaka takribani 300 baada ya kifo Cha Farao Alexander The Great. Kipindi Warumi wanavamia Misri, Misri ilikuwa inaongozwa na Malkia kutoka ukoo wa Ptolemy alieitwa Malkia Cleopatra wa VII huyu ndio aliyejisalimisha kwa Warumi baada ya kuona ameshindwa vita.

Mwisho wa Ukuu wa watu wa Misri.

Warumi walishangilia sana na kufurahi kuchukua Misri nchi yenye utajiri wa maarifa, Mali nakadhalika. Waliendeleza utawala wao wa mabavu dhidi ya wenyeji na pia waliingiza masanamu ya Miungu yao kama vile Isis kwenye Mahekalu ya watu wa Misri ili waiabudu na ukipinga Kifo ndio hatima yako. Jiji la Alexandria lenye Maktaba iliyohifadhi nyaraka za Wamisri nalo lilikuwa chini ya Warumi hao. Kipindi Warumi wanavamia kupitia mwambao wa bahari ya Mediterranean ambako ndiko ngome kuu ilikuwako huko jiji la Alexandria, Warumi walitega baruti za kulipua kando kando na Ngome kuu. Moto huo uliwaka na ukafanikiwa kuteketeza Maktaba kuu ya Alexandria ila pia baadhi ya Nyaraka Warumi wakifanikiwa kuokoa.
Baadhi ya Nyaraka walizoziokoa Warumi walizihifadhi kwenye ilo jumba walivofanikisha kurekebisha Maktaba hiyo baada ya kuungua vibaya. Mizimu ya Misri ilishachora kila kitu kupitia waaguzi wa jadi mifumo kama vile ya Magari ya kisiasa, Ndege, vifaru, Simu janja, falsafa, vifaru vya kivita na mengine mengi yaliandikwa.
Ndio maana kwa sasa uvumbuzi unachukua miaka na miaka kwa kuwa izo tamaduni sio zao waliiba huko walipowatawala inawachukua miaka mingi kuzielewa ili kuvumbua ubunifu wa Mizimu. Maktaba hiyo ilizidi kuaribiwa kwenye uso wa Dunia toka Warumi watawale Misri, mpaka kufikia Karne ya 3 AD kipindi Cha Mtawala Aurelian na kuendelea Maktaba ilizidi kuharibiwa zaidi. Hicho kikawa chanzo Cha kupotea kwa maarifa ya mwanadamu na Tamaduni zake.

Watu wa Kemet hapo mwanzon wengi wao walikuwa ni wenye rangi nyeusi ila kutokana na uvamizi wa mwanzo wa Wagiriki, warumi na Kisha waarabu hii ilipelekea mabadiliko makubwa sana kwa watu hao kupoteza uhalisia wa kale.

Asante kwa kusoma uzi huu 🤝🙏
 

Attachments

  • 11c97ca0fd0100f6f26560bf7d0c197c.jpg
    11c97ca0fd0100f6f26560bf7d0c197c.jpg
    16.1 KB · Views: 30
  • b386ec9237d5064c0b4f8e842f25ab28.jpg
    b386ec9237d5064c0b4f8e842f25ab28.jpg
    15.7 KB · Views: 28
  • d8c296619427f804759db12de1f244b9.jpg
    d8c296619427f804759db12de1f244b9.jpg
    34.1 KB · Views: 27
  • images (11).jpeg
    images (11).jpeg
    62.5 KB · Views: 26
  • images (1).jpeg
    images (1).jpeg
    59.4 KB · Views: 25
  • images (2).jpeg
    images (2).jpeg
    10.2 KB · Views: 25
Back
Top Bottom