Mateso
JF-Expert Member
- Aug 6, 2008
- 259
- 19
Wana Jf naomba niwashukuru wote ambao wamekuwa wakitoa changamoto zao mbalimbali kuhusu uchaguzi wa 2010 kwa sababu wamesaidia kwa namna moja au nyingine kuelimisha kwa kiasi kikubwa sana umma wa wawatanzania kuhusu uchaguzi wa mwaka huu. Najua siyo wote wanaosoma JF lakini ninafurahi na kujivuna kuwa kuwa kuna baadhi ya ndugu zetu wa agazeti wanaowakilsha yale yanayotolewa ndani hapa kwa wananchi kwa kupita magazeti yao. Jambo hili linanipa imani kuwa asilimia kubwa ya yanayoandikwa hapa ndani yanawafilia watanzania wengi kupitia magazeti mbali mbali. Nawashukuru sana ndugu zetu waandishi wa magazeti kwa juhudi zao na naomba waongezi juhudi ili kuhakikisha kuwa yale yote muhimu yanayoandikwa na JF yanawfikia watanzania wasioweza kuifikia au kuipata kona ya JF. Baada ya kusema hayo naomba nirudi kwa mzee wangu wa kiraracha bwana AUGUST LYATONGA MREMA A.K.A MZEE WA SIKU SABA. Naamini wengi wanakumbuka enzi zake za siku saba hata kwa waume za watu alipokuwa ndata mkuu pale mambo ya ndani hadi kuoewa unaibu waziri mkuu kwa mikiki yake mpaka waziri wa kazi hadi alipoanjia ngazi kwa manufaa ya wadanganyika . Kwa ukweli alifanya maamuzi ya kijasiri ambapo kila mtanzania alimwopna shujaa wa wanyonge hata asilimia kubwa walikuwa tayari kumpa urais wa nchi 1995 kama siyo CCM kuwa na mbinu kubwa. Nilichokiweka akilini mpaka leo ni pale wakati wa kutangaza nia ulipotimia siku moja Mrema akatamka hadharani kuwa '"Nyerere huyu ndiye alityeniambia nihamie upinzani ili niimarishe upinzani na Nyerere huyu huyu ndiye anayeniambia nisigombee urais nikagombee ubunge''. Hapa nilijiuliza maswali mengi ambayo ndo napata jibu sasa hivi.
Awali baada ya kauli hii nilijiuliza kwamba Mrema ni kivuli cha CCM kilichopandikizwa na Nyerere ili kuonekane kuna upinzani? Kabla sijapata jibu Mrema kaivuruga NCCR Mageuzi akishikiana na Mabere Marando akahamia TLP. Tangu aingie TLP hajafanya jambo lolote la maana zaidi ya kupiga domo kama mchungaji yule anayeongea anapokuwa amechacha ijapokuwa na mheshimu kwa kuweza kuitetea katiba ya Jamhuri kuliko mtanzania yeyote ili isipokuwa hayati Nyerere. Tangu JK aingie madarakani Mrema amekuwa akijikomba sana kwa kwake kwa kumsifia na kusifia CCM. Wote mnaona yote yaliyotokea Dodoma na kwenye mkutano mkuu wa TLP juzi. Mrema huku akijua chama chake kimeshamteua mgombea urais alisimama na kudiriki kusema mbele ya wanachama wenzake kuwa '"CHINI YA UONGOZI WA JK NA GHALIB BILAL SERIKALI ITAKUWA NZURI SANA'' Hivi mtu mwenye akili anamwelewaje huyu mtu? Hii ndiyo sababu kubwa ya kumwita mrema kuwa ni fisadi wa siasa na kuwadi mkuu wa CCM. Anathubutu kupiga kifua mbele ya wanachama wa TLP kuwa CCM imemchangia 200,000/= za kwenda kuchukua form za ubunge Vunjo kupitia TLP. Hii inakuja akilini kweili? NAOMBA NIHITIMISHE KWA KUWAOMBA WANAVUNJO WASIJE WAKALOGWA KUMCHAGUA NDUMILA KUWILI HUYU. SIWAAMBII MUMCHAGUE NANI ILA NAASHAURI MSIMCHAGUE HUYU KIGEUGEU anayeweza keshokutwa akamtukana ahata rais huku akijidai anashinda kesi zote za kubambikiwa. PIGIENI kura hata koti lililotundikwa kwenye mti kuliko Mrema. Nawatakieni kila la heri na uchaguzi wa amani na wa kidemokrsia.