The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

Haya bwana Mrema tumekusikia..sema lingine maana hilo linajulikana
 
huyu ni nyoka wa demokrasia, msaliti wa watz, yeye ndiye aleyewavuruga na kuharibu upinzani, ili ccm iendelee kuwanyonya na kuwakandamiza wananchi
 
Bora ajiite usalama wa mafisadi badala ya kujibaraguza kwamba ni usalama wa Taifa. Nilikuwa naheshima kubwa kwa Mrema kama mwanasiasa pamoja na kwamba miaka mingi ilisemekana yeye ni pandikizi la CCM katika vyama vingi alivyopitia. Sasa ukweli unadhihiri kwa kumtetea Kikwete ambaye ameshindwa vibaya sana kama kiongozi wa nchi.
 
Amefulia hadi sabuni imempausha uso. Mpumbavu sana huyu dumuzi.
 
Alikua na jamani na hao huwa hawastaafu, sasa afiche nini wakati kila mtu anjua kuwa yeye ni usalama?
 
Na akipewa kura huko bungeni tutajua kweli wadanganyika muna akili timamu
 
yaaani hili zee sikujua kama ni jinga to that level
 
Maneno usalama wa Taifa ni matamu masikioni, lakini kivitendo yamekuwa abused; yamegeuzwa kuwa uhasama wa taifa. Mzee Mrema, wakati ule ulipotumwa kuichinja NCCR mbona hukusema? Mzee Mrema, kwa hiyo ndo maana unang'ang'ania uenyekiti wa TLP? Naamini TLP wana masikio, na wapiga kura wa Vunjo sio viziwi.
 
Anatapatapa ili wamkumbuke maana anaona kama wamesahau jinsi mambo yalivyo mengi yeye amewekwa pending!!!njaaa
 
wanatoka kwenye magamba yao taratiiiibu...who's next?
 
Namuonea huruma Mrema anatafuta huruma na wema wa ccm ili awe Mbunge 2010 kama alivyodhamiria anajidanganya ameomba aachiwe jimbo wakampuuza sasa anadhani akimtetea Kikwete watamuachia.Pole mzee inatosha ulivyotuvuruga
 
Kwani usalama wa taifa ndio nini? Wakati mabilioni ya fedha yanakwapuliwa kupitia EPA, Meremeta, Deep Green Finance, Kagoda, Mwananchi Gold, Richmond, etc, etc, mbona hatujaona mchango wowote wa Mrema kwenye kuibua madhambi haya? Anapoguswa bwana mkubwa ndio hisia za usalama wa taifa zinapojitokeza? Ama kweli Tanzania haina wanasiasa wazalendo!
 
3836722.jpg


Mrema alisema kutokana na taaluma yake ya Afisa wa Usalama wa Taifa anaamini kuwa kinachofanyika sasa kinaipeleka nchi pabaya na hivyo yeye hawezi kukaa kimya.

Mzee wa Kiraracha, wamekutuma?
Shughulikia mambo muhimu kwanza kama kujitibia na kwenda India!!
 
Mwaka 1992, Augustino Lyatonga Mrema, wakati huo akiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani, aliapa kuwa hawezi kuihama CCM na kwamba ni mwehu tu anayeweza kuchukua hatua hiyo.

Aliliongoza jeshi la polisi (FFU) kuwashambulia, kuwapiga na kuwapa vilema vya maisha wananchi wana mageuzi kosa lao likiwa kudai mfumo wa vyama vingi. Kama kuna kitu huyu shushushu aliyekubuhu anakihofia ni CCM kung'olewa madarakani - CCM ndiyo msitiri wake kwa vitendo vyake vya nyuma na ni hofu hii ndio inamtuma.

Ni siasa za nikune na mimi nikukune na hivi sasa they need each other kuliko wakati wowote ule uliopita. Tatizo la wengi wa wafuasi wa Mrema ni kuwa wanaamini wanamfahamu huyu shushushu wa kutupwa kumbe hawajui kitu sasa subirini muone watakavyoingia humu kumtetea, muda si mrefu.
 
Back
Top Bottom