The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

Mrema alipobanwa maswali na waandishi wa habari aeleze kama kuna kitu amepewa ili azungumze hayo aliyoyasema alisema yeye hatarajii chochote kutoka kwa Kikwete wala hana mpango wa kutaka kurudi CCM.
Vizuri sana, kwani huna tena nafasi chamani...!
 
Let the dead bury their dead.

Its just unfortunate that hata sisi ni wafu tu!! wacha tuzikane hivyohivyo... tumeachia hazina ya taifa letu na sasa tunahesabu maganda tu!!!
 
"Nikirudi CCM, nihukumiwe kunyongwa" - ALM
Atakuwa amesahau alichoahidi huyu. Bahati mbaya nimesahau mwaka, ila kama sikosei ni between late 90's au early 00's
 
The very same Mrema ambaye alipata kura nyingi za urais '95 ambazo mpaka leo hazijafikiwa tena! ndiye aliyewatetemesha CCM wakati bado Nyerere yuko hai!

Very same Mrema leo ni msaliti, mchovu, hafai, anaharibu mageuzi, shushushu!

Ikiwa tusipokaa chini na kujua matatizo yetu watanzania kila leo tutamtafuta mchawi tu

Mrema amechoka na watanzania ambao. hawapigi kura wala hawajui wanaowaita wapinzani wanakula na kuishi vipi

Mrema hawezi kufa na njaa au kusihi maisha anayoishi leo kwa tiketi kuwa akiishi hivyo ndiyo anatukuza upinzani

Tunalia mageuzi humu kila kukicha, ili hali wanaojitoa kuwenye mageuzi sio sehemu ya sisi kujishughulisha nao!

Gharama ya mageuzi ni kubwa jamani, inaanzia kwa mmojammoja na kwa umoja, kesho atatokea Mrema mwingine ambaye naye baada ya miaka 10 au 15 atakuwa kama Mrema. we have problem somewhere.

Mrema alifanya kosa la kuondoka haraka CCM angeondoka kwa style ya kukivunja aondoke na kondoo wachache, CCM na watanzania wamemwacha ajifie.... na tunanyoosha mkono kuwa ni KOSA LAKE!

In short hakuna mwenye time nao hawa watu..

Only made in Tanzania
 
tatizo ni sisi watanzania wenyewe kama alivyosema waberoya, wananchi kupiga kura hampigi, kujiandikisha kwenyewe tabu, mimi naamini ni asilimia chache sana hapa JF wamewahi kupiga kura. tanzania tunasumbulia na umaskini, maradhi na ujinga. hapio lazima uwe na moja na hapa JF wengi ni wajinga maana wanatoa kauli ambazo hazileti maendeleo kwa wana JF wengine au watanzania kwa ujumla. tanzania tunasahau tulipotoka na hatujui tunapoelekea.

kama kuna wanasiasa wanawavutia ni heri tuwaunge mkono sio tu kwa kuandika huku kwenye forum. mrema malengo yake ni kurudi bungeni maana anaamini kabisa vyama vya upinzani haviwezi kushinda bila wanachi kuwaunga mkono. nani hapa JF hajui kuwa mwakani kikwete atashinda tena kwa kishindo na CCM kwa ujumla. ndio ilivyo siasa za afrika. sasa mnataka mrema, mbowe na wenzio wafanye nini!!!

change starts with you. sio kuwaonyeshea wengine vidole. mrema wengine watajitokeza. Mrema cannot be the change or make the change lakini amesha sparkle the change and its up to us to finish and make the change happen.

tuache ujinga ndio maana CCM wana take the advantage
 
Mrema aingia rasmi mtandao mpya wa JK

na Hellen Ngoromera na Humphrey Shao

MTANDAO mpya wa kumsafisha na kumjenga upya kisiasa Rais Jakaya Kikwete, huku ukiwasakama wanaomkosoa, unazidi kupanuka baada ya kuwanasa baadhi ya wanasiasa wa upinzani kuongeza nguvu ya wanaCCM katika azima hiyo.

Mbali na wengine waliojitokeza katika wiki chache zilizopita, jana ilikuwa zamu ya Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema, ambaye aliwashambulia wakosoaji wa Rais Kikwete, hasa wanasiasa wastaafu na makada wa CCM waliojitokeza hadharani kumpinga katika kongamano la siku tatu lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) mwezi uliopita.

Baadhi ya wanasiasa, waliojitokeza kuwashambulia washiriki wa kongamano hilo na kuisakama MNF kwa kumkosoa Kikwete, ni pamoja na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Pius Ngeze, ambaye aliwahi kujitangaza kuwa katika mtandao wa awali wa Kikwete kusaka urais mwaka 2005.

Wengine waliojitokeza hadi sasa ni Rais wa TADEA, John Chipaka, Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa, Mwenyekiti Mwenza wa REDET, Dk. Benson Bana na Sheikh Yahya Hussein aliyeibuka hivi karibuni na kutisha wanaotaka kugombea urais kwamba watakufa ghafla kama watashindana na Rais Kikwete.

Mrema jana aliongezeka katika kuilaumu taasisi hiyo na wanaomsakama Rais Kikwete.

Katika kauli ya kutovumilia siasa za kukosoana ndani ya chama kile kile, Mrema aliongeza kuwa makada wa CCM wanaotaka kumkosoa rais wajiengue na kuanzisha chama chao.

Alisema iwapo watashindwa kufanya hivyo wajiunge na vyama vya upinzani ama kuzungumzia hayo katika vikao vya Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ya Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mrema alisema vitendo vinavyofanywa na viongozi hao vinatishia na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa taifa.

“Kuongoza nchi si kazi rahisi, hivyo ikiwa wanaona sera za kupambana na ufisadi hazitekelezeki wasipinge wakiwa ndani ya CCM, basi wao ndio wanaotakiwa wafanye maamuzi magumu, ama kwa kuanzisha chama chao ama wajiunge na vyama vya upinzani kama mimi nilivyofanya, lakini kutoa kauli za uchochezi wakati bado ni wanachama wa CCM, wananchi hawatawaelewa,” alisema Mrema.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo wa TLP, ambaye amewahi kushika nyadhifa nyingi serikalini zikiwamo uwaziri wa mambo ya ndani na unaibu waziri mkuu kauli zilizotolewa na makada hao wa CCM kuwa rais amezungukwa na kundi la wezi na kama anashindwa kuchukua maamuzi magumu atoswe, ikiwa zitaachwa zinaweza kuleta uchochezi.

“Kutokana na uzito wa kauli hizo na mahali zilipozungumziwa, mimi kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Naibu Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia nimewahi kuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Wilaya, naelewa wazi athari zake…nchi isitawalike. Ndiyo maana nimeona niwaiteni kuzungumza juu ya suala hilo. Wala sijatumwa na mtu yeyote.

“Wapo watakaosema kwamba nimeingilia mambo ya chama tawala wakati mimi si mwanachama wa CCM, lakini suala hili lisipokemewa linaweza kusababisha uvunjifu wa amani,” alisema Mrema.

Kwa mujibu wa Mrema anavyoelewa malengo ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere ni kukuza amani na utulivu nchini na Afrika nzima, lakini wao walilitumia kongamano hilo kutoa kauli za uchochezi na uzandiki.

Mrema alisema kuwa waliosema rais kazungukwa na kundi la wezi wanamaanisha kwamba naye ni mwizi, jambo ambalo alilipinga.

Alisema kuwa kitendo cha kuchochea na kufanya uzandiki ni kuvunja sheria ya usalama wa taifa na kwamba adhabu yake iko wazi, hivyo ingefaa vyombo vya usalama vifanye kazi kuliko kuacha watu waendelee kuchafua amani kwa kisingizio cha demokrasia.

“Wengine watasema namfagilia rais au pengine nataka kurudi CCM. Mimi simfagilii wala sina mpango wa kurudi CCM isipokuwa rais ni mpambanaji katika vita ya ufisadi kama nilivyokuwa mimi wakati nilipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu, hivyo siwezi kuona rais wa nchi hii anaonewa nikanyamaza,” alisema Mrema.

Mrema aliongeza kuwa kama Rais Kikwete angekuwa madarakani wakati ule yeye asingefukuzwa kazi kwa sababu malengo yake ni sawa na ya rais kupambana na ufisadi, hivyo hamfagilii Kikwete na wala hana mpango wa kurudi CCM bali atagombea ubunge wa jimbo huko Vunjo kwa tiketi ya TLP bila msaada wa CCM na kwamba akiingia bungeni atashirikiana na rais yeyote yule iwe kutoka CCM au chama pinzani.

“Kuna watu wanasema kwamba najipendekeza ili CCM iniachie Jimbo la Vunjo na wengine wanasema mimi ni kibaraka wa CCM, lakini kama ni hivyo mbona CCM wameshawarubuni na kuwachukua wenyeviti wangu wa vijiji viwili wa TLP mara tu baada ya kuchaguliwa, hata kabla hawajaapishwa?” alihoji Mrema.

Mrema aliwasuta makada hao akisema wanataka rais achukue maamuzi gani magumu.

“…Ili makada hao waone, alikubali aliyekuwa Waziri wake Mkuu na swahiba wake, Edward Lowassa kujiuzulu kufuatia kuhusishwa na kashfa ya Kampuni tata ya kufua umeme wa dharura ya Richmond.

“Wengine waliochukuliwa hatua kwa kujiuzulu ni mawaziri wake wawili, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha sambamba na kuwafikisha mahakamani viongozi wengine kwa kuhusishwa na sakata la EPA,” alisema na kuongeza kuwa EPA ilikuwapo tangu 1992.

Mrema alisema makada wanaomsakama Rais Kikwete kwa kushindwa kusisimamia vizuri sera nzuri za Mwalimu Nyerere kama vile vijiji vya ujamaa, madaraka mikoani, mashirika ya umma na nyingine, inashangaza sasa wanapomwandama na kumchafua rais wakati wao walishindwa na kuhoji kuwa pengine ni uchu wa madaraka hivyo wanataka kurudi madarakani kwa mlango wa uwani.

Alipoulizwa sababu ilivyomfanya azungumzie suala hilo jana wakati alikuwa mmoja wa walioudhuria kongamano la Mwalimu Nyerere, Mrema alimtupia swali hilo Katibu wa chama hicho Hamad Tao ili alijibu ambapo alisema kuwa alinyimwa nafasi ya kuzungumza kwa siku zote tatu za kongamano hilo pamoja na kunyoosha mkono kwa muda mrefu.

Zipo tetesi kwamba Mrema, ambaye afya yake imekuwa ikitetereka katika miaka ya karibuni, na ambaye sasa hivi anaonekana kuimarika upya, anatibiwa kwa gharama za serikali; na kwamba hiyo ni moja ya njia zilizotumika kumnasa, na sasa analipa fadhila kwa kuwashambulia wanaomkosoa Rais Kikwete.

Alipohojiwa na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Mrema alisema serikali haijawahi kumgharamia matibabu yoyote na wanaoeneza maneno hayo ni waongo na wazushi.

“Juni 2009 nililazwa wiki moja katika hospitali ya KCMC ambayo ni hospitali ya serikali nikapatiwa matibabu ambayo hata hayafiki sh 100,000 na risiti ninazo. Sasa hapo nilichofadhiliwa na serikali ni kitu gani? Mbona watu ni wazushi na waongo? Huo ni unafiki, tutaendelea na mambo haya hadi lini?
“Kwa kifupi sijawahi kutibiwa kwa gharama za serikali, hivyo watu wasizushe mambo,” alisema Mrema.

Akizungumzia kuhusu kuhusishwa na serikali ya awamu ya nne, Mrema alikanusha vikali suala hilo na kusema ametoa kauli dhidi ya wanaomsakama Rais Kikwete kwa kuwa ni haki na wajibu wake kama mzalendo wa nchi hii.
“Sijaingia katika mtandao wa serikali, nimezungumza hayo leo kama mwananchi mzalendo, kwani kuna ubaya gani kusema hayo? Mtendeeni haki Rais Kikwete jamani,” alisema Mrema.

Alipoulizwa Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi, Premmy Kibanga kuhusu serikali kumhudumia Mrema matibabu, alisema hafahamu yanayoendelea kwa kuwa yupo likizo.

“He! siku hizi rais ndio anapeleka watu hospitali? Waulize Wizara ya Afya, kwa sasa niko nyumbani likizo, sijui yanayoendelea,” alisema Premmy.

Tangu kuibuka kwa mtandao huo, watetezi wa Rasi Kikwete wamekuwa wakiwaita wakosoaji majina kama wehu, wahuni, genge na watu wenye wivu, huku baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari vikiishambulia Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa kuiita genge la Butiku.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo walitoa kauli kali za kukosoa uongozi wa Rais Kikwete, huku Askofu Msaidizi Method Kilaini, akikemea kwa ukali ufisadi serikalini na kusema ‘nchi inatembea uchi’. Waziri mstaafu Mateo Qares, ambaye pia aliwahi kuwa mkuu wa mkoa, alitoa rai kwamba kama rais atashindwa kushughulikia mafisadi, asigombee tena mwakani. Wengine waliokosoa utendaji wa Rais Kikwete ni makada wa CCM, akina Fred Mpendazoe, Stephen Mashishanga, Nape Nnauye, Joseph Warioba na washiriki wengine walioonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa serikali.
 
Duuh sio mchezo.Hawa spies wanatuchezesha ngoma ya kuuzunguka mbuyu
 
viongozi wa kitanzania ni bendera kufuata upepo...wako wako tuu hawana msimamo kabisa wako kama wacheza sinema vile bana ona sasa...hawako kutetea maslahi ya wananchi bali wanaangalia wapi kuna msosi kama mafisi vile

kweli mwanakwetu ...maana hata prezidenti alishasemaga 70% ya watanzania wanafuata upepo tu
 
Achana na hilo fara la kichaga limeisha jichokea . Linafata upepo kama bendela . Hao ndio wezi wakubwa . MWake akaungane na mafisadi wenzake kuendelea kuiangamiza nchi yetu. angekua ana akili angejiunga chadema . na hao wanaojifanya vinara wa ufisa di waiache ccm wajiunge na chadema.
 
Mkuu, unasahau kuwa kosa alilofanya Mrema ni kutojua kuwa alikuwa anafuatwa kila siku na watu wa uslama wa taifa, ambao walikuwa wanafanya kila wanaloweza kuvuruga mipango yake kisiasa. Ukiangalia migogoro yote ya NCCR na TLP si yeye aliyeianzisha bali ni watu waliotumwa kumvuruga. Marando anajulikana wazi kuwa ni mtu wa uslama ambaye alifanya kazi ya kumdhibiti mMrema alipotoka CCM, Jaffu ni mtu wa usalama aliyefanya kazi ya kumvuruga alipoingia TLP hii sio siri,
migogoro sio ya Mrema ili iliapangwa. Habari zaidi anaweza kukupa George Liundi yeye anajua wazi ni nini klikuwa kinafanyika. Hata kama akirudi CCM Mrema atakuwa mrema.
 
Mkuu, unasahau kuwa kosa alilofanya Mrema ni kutojua kuwa alikuwa anafuatwa kila siku na watu wa uslama wa taifa, ambao walikuwa wanafanya kila wanaloweza kuvuruga mipango yake kisiasa. Ukiangalia migogoro yote ya NCCR na TLP si yeye aliyeianzisha bali ni watu waliotumwa kumvuruga. Marando anajulikana wazi kuwa ni mtu wa uslama ambaye alifanya kazi ya kumdhibiti mMrema alipotoka CCM, Jaffu ni mtu wa usalama aliyefanya kazi ya kumvuruga alipoingia TLP hii sio siri,
migogoro sio ya Mrema ili iliapangwa. Habari zaidi anaweza kukupa George Liundi yeye anajua wazi ni nini klikuwa kinafanyika. Hata kama akirudi CCM Mrema atakuwa mrema.

huyo george lIUNDI ana mengi ya kusema...kwani ccm wamemuacha afe njaa..pale mabibo uswahilini pamoja na kujua wazi kuwa yeye ndiye alikuwa anajuwa siri zote za kuangamiza NCCR na watu wote alikuwa anapenyeza yeye na kuwalipa yeye kwenye payroll ya msajili...,aanajuwa siri ya kuenguliwa kinara wa kwanza wa upinzani JAMES MAPALALA na kumstarve kwa njaa.....nani anamkumbuka mapalala hapa na sera yake ya UTAJIRISHO......

Jamani kuna watu wengi genuine wameumizwa na haya mageuzi...sasa wanakufa njaa....na sisi tunawacheka na kuwatukuza wale ambao walirubuniwa na leo wanakula raha na kupewa vyeo kwa kuuuuwa mageuzi...tunawaona wasaliti heros!!!

Nadhani kwa kuwa CCM wanamuuwa njaa Liundi [walikuwa wamemuahidi ubunge akistaafu]...wapinzani wanaweza kupata siri nyingi kwake...HISTORIA YA NCHI HII IWEKWE SAWA!!
 
hii heading ya thread Msanii! ilinishtua kweli...mi nilidhani Mrema arudi ccm inamaanisha yaani ndio amesharudi ccm!!!
 
Mrema umekua msemaji wa Kikwete?
ban.mtazamo.jpg


Irene Mark

amka2.gif
NAAMINI Augustino Lyatonga Mrema, Mwenyekiti Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP), ameamua kuwa msemaji asiye rasmi wa Rais Jakaya Kikwete kutokana na sababu za siri anazozijua mwenyewe.
Ndiyo maana kwa siku za hivi karibuni, ameamua kujipa madaraka ya usemaji wa rais japokuwa anakanusha hadharani tena kwa msisitizo, jambo linalonifanya niamini kwamba dhamira yake inamsuta kwa kujitwika msalaba wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu na kuendelea kunishawishi kwamba anachokifanya si kingine bali ni ‘kumsafisha' Kikwete na kujijengea mazingira bora zaidi ya kisiasa.
Ukweli ni kwamba, hivi sasa Mrema huyu hauziki. Amepauka kisiasa ndiyo maana anatafuta pa kutokea. Anahisi amepata lakini hali halisi iko wazi, amekalia kuti kavu ndani ya chama anachokitawala cha Tanzania Labour (TLP).
Kwa kauli yake hadharani, Mrema anasema, "Sijaingia katika mtandao wa serikali, nimezungumza hayo leo kama mwananchi mzalendo, kwani kuna ubaya gani kusema hayo? Mtendeeni haki Rais Kikwete jamani."
Ni kweli kama anavyosema kwamba hajaingia kwenye mtandao wa serikali kwa sababu hakubaliki huko na yeye anafahamu hilo. Mrema anaishawishi jamii kumtendea haki Kikwete, anasahau kwamba hata kukosolewa pia ni haki tena iliyoainishwa kikatiba?
Mrema ameingia kwenye mtandao binafsi wa Kikwete na wapambe wake ambao wako tayari kwa lolote kuhakikisha sifa mbaya na nzuri za Kikwete zinapata mapokeo chanya machoni pa jamii.
Hapa kuna mambo mawili, kwanza ni Kikwete kama mtu binafsi, anasimama kwa kuwa ndiye mgombea uras kwa tiketi ya CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao na huko ndiko tuendako.
Pili, serikali ni ile inayomtambua rais kama mkuu wa taasisi muhimu kwa ustawi wa taifa bora lenye mkusanyiko wa watendaji wakiwemo usalama wa taifa, jeshi, polisi na idara nyingine.
Wachambuzi makini wa siasa, wanashtushwa na kauli hiyo ya Mrema aliyekuwa mwiba mkali kwa wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na watawala wa serikali inayotokana na chama hicho katikati ya miaka ya 1990 hasa baada ya kuingia rasmi kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.
Mrema huyu ambaye ni mwenyekiti wa taifa wa TLP alianza kampeni za kujikita kwenye kundi la utetezi wiki chache zilizopita alipokaririwa akisema utendaji wa Kikwete (hakusema serikali) kwa kipindi cha miaka minne, umekua bora sana hasa katika mapambano dhidi ya ufisadi.
Kwa Mrema, hii ina maana kwamba Kikwete anaweza bila urais alionao sasa. Kwangu si kweli, ndiyo maana alishindwa kupambana nao alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka 10 mfululizo kwa sababu mafisadi wa leo, hawajazuka tu, wameanzia mahali ambapo Kikwete anapafahamu.
Siku moja baada ya mnajimu, Sheikh Yahya Hussein, kutumbukia kwenye mtego huo kwa lengo la kubadili mwelekeo wa wananchi kuhusu utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne inayoongozwa na Kikwete, Mrema alinukuliwa akiushabikia utabiri na kuwaonya wanasiasa wengine kutafuta kazi za kufanya kipindi hiki ili kumpisha Kikwete amalizie muda uliobaki.
Sheikh Yahya aliwaogopesha watu kwamba atakayempinga Kikwete, atakufa ghafla. Mrema akaunga mkono kwa asilimia 100 kisha akawashauri wale wanaofikiria kuwania urais kwenye uchaguzi ujao kuacha kiherehere.
Wote tunafahamu kwamba kifo kipo na kila mwenye pumzi lazima atakufa. Lini, wapi na kwa sababu gani, hilo ni fumbo kutoka kwa Mungu. Lakini sheria za nchi haziruhusu mtu kumwambia mwingine atakufa. Huko ni kutishana kusikostahili.
Yote yaliyosemwa na Sheikh Yahya, vyombo vya usalama wa taifa na polisi vimenyamaza kimya. Hivi leo, mnajimu huyo angeamua kusema Kikwete atakufa, sina hakika kama angeendelea kulala usingizi mnono nyumbani kwake. Angekamatwa na sheria ingechukua mkondo wake.
Sasa uko wapi usawa kwa raia wote. Wale wanaotaka kutumia haki zao kama John Shibuda kugombea urais wanatishiwa kifo na hakuna anayewatetea, halafu tunajinasib kwamba tunaongozwa kwa utawala wa sheria. Si kweli.
Kwangu, Sheikh Yahya anastahili kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya jinai kwa kutishia kuua kwa maneno. Mshtakiwa wa pili kwenye kesi hiyo ni Mrema. Adhabu yao ni kifungo kisichozidi miezi 12; faini ama vyote kwa pamoja.
Hivi, ni kipi hasa kinachomsukuma Mrema kujitwika majukumu mazito ya ‘upambe' kwa Kikwete wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi ilhali mambo si shwari ndani ya chama chake? Kwa nini asitumie nguvu hizo kuwahutubia wana wa Vunjo anaotarajia kuwaomba ridhaa ya kuwawakilisha?
Binafsi, hoja za Mrema katika kujenga utetezi dhidi ya Kikwete ni dhaifu. Hazina mashiko wala ushawishi kwa jamii. Namshauri ajipange kwa ajili ya kampeni zijazo ili ajiweke kwenye nafasi nzuri ya kuwa mbunge wa Vunjo kwa mara nyingine kuliko kupoteza muda kumtetea mwenyekiti wa CCM taifa. Naamini kwamba wananchi ambao ndiyo wenye maamuzi makubwa, wana uwezo wa kumpima Kikwete mwenyewe, iwapo amefanikiwa ama la, si Mrema wala Shekhe Yahaya.


 
2009-12-30 08:35:00
Politicians round in on TLP boss MremaBy Florence Mugarula

Political analysts have criticised the Tanzania Labour Party (TLP) chairman, Mr Augustine Mrema, for attacking some paatricipants of the Mwalimu Nyerere Foundation symposium.

Mr Mrema told a press conference in Dar es Salaam on Monday that remarks by some participants against the fourth phase government of President Jakaya Kikwete, threatened national security.

However, many politicians interviewed yesterday by this newspaper, explained that contributors during the symposium, were right to say what they said because they were exercising their rights and fulfilled their responsibilities as patriotic Tanzanians.

Mr Mrema said during his press briefing that criticisms by Mwalimu Nyerere Foundation officials jeopardised nation security by openly blaming President Jakaya Kikwete's leadership for failure to take drastic measurers against alleged corrupt leaders.

However, Mwalimu Nyerere Foundation executive secretary, Mr Joseph Butiku, declined comment on Mrema's remarks.

But political analyst, Prof Mwesiga Baregu, said there was a possibility that Mr Mrema was trying to forge close relationship with the ruling CCM for his political interests.

Prof Baregu told this newspaper that there was no need for people to discuss pertinent issues in secrecy, simply because they are members of the ruling party.

He said Mr Mrema who participated fully in the introduction of political changes in the country in 1992, is yet to understand the basic pillars of democracy -- which is freedom to expression, and expressing ideas without fear.

"It is very unfortunate that some politicians do not understand the meaning and basis of true democracy. Mr Mrema was a part of a group of people who brought political changes in the country, but he seems not to understand what democracy is," said Prof Baregu.

He said no country could boast of practising true democracy if members of the society are barred from expressing their views and ideas.

NCCR- Mageuzi secretary general Samwel Ruhuza, said Mr Mrema has confirmed that he is campaigning for President Kikwete's government.

According to Mr Ruhuza, the Mwalimu Nyerere Foundation had the right to discuss any issue concerning the Government and that pointing an accusing finger that what was discussed, was crime, is indeed against freedom of expression.

"It is quite clear that all who talked about Mr Kikwete's government were trying to show the right path to be followed for the benefit of all Tanzanians, and they have the right to do so. But Mr Mrema fails to differentiate between challenges and accusations," said Mr Ruhuza.

Mr Ruhuza said opposition does not mean enmity and that it was possible Mr Mrema was interested in forging alliance with CCM.

Commenting on the matter, the leader of opposition in the National Assembly, Mr Hamad Rashid Mohammed, said Mr Mrema has forgotten that the Constitution provides the right to freedom of expression and allows every Tanzanians to join any registered political party in the country.

Mr Mohamed said views discussed during the Mwalimu Nyerere Foundation symposium had nothing to do with national security, but to unearth truth and to remind the Government of its responsibilities.

"I think speakers at the symposium were exercising their constitutional rights, and not threaten national security," argued Mr Mohamed.

The representative of Non Parliamentarian Parties, Dr Emmanuel Makaidi, said Mr Mrema has failed to see that political differences are acceptable in a democratic country.

Dr Makaidi who is also the chairman of the National League for Democracy (NLD), said the Mwalimu Nyerere Foundation has nothing to do with jeopardising national security but is there to set agenda for public discussion.
 
Kahahidiwa utatu mtakatifu mkuu
umjui huyu
tuulizeni wachaga tuliopitia shule kidogo
 
3836722.jpg


MWENYEKITI wa Chama Cha Siasa Tanzania Labour Party (TLP) Augostino Mrema

MWENYEKITI wa Chama Cha Siasa Tanzania Labour Party (TLP) Agustine Mrema amesema kitendo cha yeye kujitokeza kumtetea Rais Jakaya Kikwete ni kufuatia taaluma yake ya Usalama wa taifa ambao anaitumia kuilinda nchi

Alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika ukimbi wa Idara ya Habari Maelezo.

Mrema alisema kutokana na taaluma yake ya Afisa wa Usalama wa Taifa anaamini kuwa kinachofanyika sasa kinaipeleka nchi pabaya na hivyo yeye hawezi kukaa kimya.

Mwenyekiti huyo alisema shutuma zinazoelekezwa kwa Rais zikifumbiwa macho matokeo yake ni machafuko ambayo yataigharimu taifa.

Alisema kinachosikitisha zaidi ni shutuma hizo kutolewa na makada wa Chama Tawala CCM jambo ambalo linaonyesha kuwa kuna mpasuko.

Mrema alisema iwapo makada hao wanaona kuwa Mwenyekiti wao hatendi kazi katika ufanisi unaohitajika ni vema wakajitoa na kujiunga na vyama vingine au waunde vya kwao.

"Kwa kweli nimejitoa muhanga kumtetea Kikwete kwa kofia mbili mimi kama Mwenyekiti na Mtanzania lakini pia kama Usalama wa Taifa natambua madhara ya kinachojadiliwa kwa sasa," alisema

Mrema alitumia fursa hiyo kukanusha habari za kuwa anamtetea Kikwete kwa lengo la kuhitaji Ubunge ambapo alisema hawezi kuwa na fikra hizo kwani Jimbo la Vunjo ana uwezo wa kulichukua bila msaada wa CCM.

Alisema ni vema Watanzania kuweka uzalendo mbele na kuachana na vishawishi kutoka kwa baadhi ya watu ambavyo vinaweza kuhatarisha amani na usalama wa Taifa.

Aidha Mwenyekiti huyo amewashutumu viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa kuandaa kongamano aliloliita la uchochezia dhidi ya Rais JK.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi sababu ya kutoongea maneno hayo wakati wa kongamano hilo alijibu kuwa hakupewa nafasi ya kuchangia.

Mrema alisema kuwa washiriki walio wengi hawakuwa watu wenye sifa za kumsema Rais kiasi hicho kwani katika uongozi wao walifanya vibaya na hawakuhukumiwa kama wao wanavyofanya sasa.
 
Naona anazeeka vibaya huyu mzee wa kiraracha.
 
Back
Top Bottom