INAENDELEA...
Tumeishia kwenye mahusiano na JF member mwenzetu, (no.7) ila sijamtaja jina ili kulinda heshma yake...
8. JF MEMBER 02.
Huyu pia naomba nisimtaje jina,katika kujadilijadili mambo ya JF moyo wangu ukiwa mfu kabisa kwenye mambo ya mahusiano,tulikuwa tukijadili a b c,za maisha na member mmoja (tukiwa mikoa tofauti) baadaye akaniambia ana safari ya Dar nikamkaribisha, nikamuuliza kama ana mahali pa kufikia akasema nimuandalie tu,nikatafuta hotel, tukakubaliana kwenda kucheck tulipocheck wote tukiwa salama tukajiachia kwa usiku kucha, akanisimulia mengi aliyopitia nikamhurumia sana lakini nikamwambia mimi sina mpango wa ndoa kwa wakati huo akasema pia si kitu anachokiwazia hata chembe, basi tukawa tunakutana tunamaliza haja za miili yetu kila mmoja anaendelea na maisha yake, baada ya miezi kadhaa nikashangaa sana, kumbe mdada alikuwa mke wa mtu na mumewe alikuwa anafanya kazi CRDB-BANK moja ya mikoa ya nchi yetu, nikashangaa zaidi imekuwaje????
Huyu sikumtafuta tena baada ya kujua ni mke wa mtu, (iliniumiza sana kihisia hii) kwa sababu sikuwahi kufikiria ku-date mke wa mtu maisha yangu yote! Japo aliniandikia sana kutaka tuendelee kwa madai kwamba yeye na mumewe walikuwa wamesha achana but I never looked back tukaishia hapo (najua lazima atasoma huu Uzi, ajue tu aliniachia maumivu makali mno)
Baada ya hapo sijapata tena kuanzisha mahusiano yenye malengo, najikuta nipo tu, hisia za kujenga mahusiano serious sina tena, I'm dating nimejifunza kutumia condoms japo sizipendi sana!
Japo kuna wakati nafikiria nifanye maamuzi serious nioe tu lakini ule moyo wa kuamua umekuwa mgumu...
Na ukweli hao 7 nilikuwa na malengo ya kuoa kabisaaa, ila baada ya hayo na kukata tamaa nadhani kuna wengine kama 13 ambao nime-date nao bila kuwa na malengo yoyote, we date thereafter kila mtu anaendelea na maisha yake, hii Hali siipendi sana pia as nakosa ujasiri wa kuingia ibadani kumuabudu Mungu nikijitazama kwenye hiyo angle, niombeeni sana nitoke kwenye huu mfumo wa maisha ndugu zangu...
Sent from my Z9 using
JamiiForums mobile app