The reason to why I didn't marry you!

The reason to why I didn't marry you!

Maamuzi ya kukurupuka hapo juu ni kama yepi best yangu au unekuwa wewe ungeamuaje kuanzia huyo namba moja mpaka tano...

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
Ulikua unampenda mary with all your heart yet ukaenda kumlipia mahari mwanamke ambae bado ulikua humjui vizuri na at the same time akili yako ndio iliamua though moyo ulikua kwa Mary, ungejipa muda kidogo wa kutafakari na kupata uhakika wa maamuzi unayotaka kuchukua

Kila mahusiano unayoingia unatia mimba au unabambikiwa mimba, ni kama you did not learn from the past ukachukua tahadhari badala yake ulikua inarudia kosa hili hilo, lets say wote wangekua na mimba zako, how could you describe your fatherhood to the kids au kwa kizazi chako? Being a farther is not about providing the needs its more than that

Kama utaendelea hivyo you will end up with unsettled life kwa sababu hata mwanamke utakaemuoa bado atakua na usumbufu wa kuwaza watoto wa nje, i mean hamtakua na utulivu wa kufocus kwenye famikia ila mtajikuta mnaanza kuwaza na watoto wa nje ambao they need equal rights na hao wa ndoani, hapo hujahesabia usumbufu wa mama zao
 
stori nzuri sana na inafundisha sana.
inatia hamasa sana.
 
Ulikua unampenda mary with all your heart yet ukaenda kumlipia mahari mwanamke ambae bado ulikua humjui vizuri na at the same time akili yako ndio iliamua though moyo ulikua kwa Mary, ungejipa muda kidogo wa kutafakari na kupata uhakika wa maamuzi unayotaka kuchukua

Kila mahusiano unayoingia unatia mimba au unabambikiwa mimba, ni kama you did not learn from the past ukachukua tahadhari badala yake ulikua inarudia kosa hili hilo, lets say wote wangekua na mimba zako, how could you describe your fatherhood to the kids au kwa kizazi chako? Being a farther is not about providing the needs its more than that

Kama utaendelea hivyo you will end up with unsettled life kwa sababu hata mwanamke utakaemuoa bado atakua na usumbufu wa kuwaza watoto wa nje, i mean hamtakua na utulivu wa kufocus kwenye famikia ila mtajikuta mnaanza kuwaza na watoto wa nje ambao they need equal rights na hao wa ndoani, hapo hujahesabia usumbufu wa mama zao
Ni kweli kabisa nilimpenda Mary, lakini mwisho wa siku kukutana na ushirikina haikuwa jambo rahisi kulivumilia, na sijui alikuwa amenifanya nini...

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
I feel you man,niliwahi pitia situation kama hiyo ila nikakutana na single father mmoja ana miaka 37 ana watoto watatu kila mmoja na mama yake.Watoto wote kawakatia bima yeye ni mtumishi wa umma na hajaoa,watoto wanakaa na mama zao safii jamaa ana maisha ya amani hadi kitambi
 
Kwa uzi huu nitaandika meeengi sana,kwa wote ambao tuliwahi ku-date but hatukufikia malengo ya kujenga familia, Kati ya watu nilio- date nao, wawili wapo humu (mmoja tulifika mbali sana na mwingine hatukuwa na mahusiano ya kiviiile) ila wote naamini watasoma uzi huu, kama kuna mahali nitakuwa nimemsingizia mtu ruksa kunikosoa...

1. Bertha...
Huyu alikuwa msichana wangu wa kwanza kabisa, tukiwa kidato cha tano, (alikuwa Iringa girls na mimi nilikuwa MINAKI) tulipendana sanaaa, I felt to be loved and I submitted all of my emotional strength

Nakumbuka wakati wa likizo tulikutana hostel za UDSM zilizopo ubungo nyuma ya NBC BANK, (bro aliniacha hapo nikiwa tution yeye akiwa masomoni nje ya nchi), kwa mara ya kwanza tulichezeana sana,lakini hatukufanya mapenzi kwa mimi kuwa na hofu sana ya UKIMWI, nayeye pia alikuwa mwenye hofu sana tukaishia hivyo, she was a very good girl,baada ya shule kufungua maisha yaliendelea, tulipofanya mitihani ya kidato cha sita mahusiano yalipungua na hatimaye yakapungua hatimaye kupotezana....

2. Grace...
Alisoma Ruvu girls, tulianza mahusiano baada ya kumaliza kidato cha sita, (tuli-date kwa muda mfupi lakinitulifanya Mambo mengi sana,kwa mara ya kwanza nikajua mpaka kulala lodge..

Baada ya muda kidogo nikagundua Grace anakunywa pombe ile mbaya, moyo wangu uliumia mno, nikahisi na-date na mti asiyefaa kabisa kuwa mke wangu tukaachana, (tulipokutana Udsm tukawa marafiki wa kawaida as if hatukuwahi kuwa na mahusiano) kwa sasa sijui yuko wapi hata...

3. MARIAM
Huyu nilikuwa na uhakika wa asilimia 80 kuwa nitamuoa, tulianza mahusiano mwishoni mwa semista ya kwanza, tukashibana sana,mwaka wa pili tukaamua kukaa Chumba kimoja (anapika anafua boom tunaweka pamoja na kufanya mipango mingi ya maisha yetu baada ya shule) eeeeh bwana wee, kumbe alikuwa na mahusiano mengine na jamaa alikuwa anasoma Duce...(nilijuaje? ni story ndefu ila nitaifupisha kwa kadri niwezavyo)

Ilikuwa siku ya Alhamis, (tukiwa mwaka wa pili) nilikuwa na ratiba ya practical nayeye alikuwa anajua, so aliniaga kwamba angeenda kumtembelea rafiki yake anaitwa Mariana, sikuwa na shaka hata kidogo,bahati mbaya kwake siku hiyo practical ikaahirishwa, nikawahi kutoka, ile nafika utawala (packing ya UDSM) naona Mariam anaingia kwenye gari ya mawasiliano, nikaamua kumfuatilia bila yeye kujua, alipofika mawasiliano alimfuata mshkaji mmoja wakaongozana kuelekea njia ya sinza, nikawa nawafuatilia na kuwapiga picha pasipo wao kujua, wakaingia moja ya lodge maeneo ya Mugabe, niliumia kwa viwango vizivyoelezeka nilisubiri kama nusu saa baada ya wao kuingia lodge nikaingia pia, nilipofika mapokezi nikachukua kitabu Cha wageni nikaandika majina yangu bandia lakini lengo ikiwa kutaka kujua chumba walichoingia Mariam na mshkaji, nikapiga picha ile daftari, (jamaa aliandika na namba yake ya simu) nikadhani atakuwa ameandika namba ya uongo lakini kwa bahati alikuwa ameandika namba yake halisi, nilichukua information zake nikaishia...

Ilipofika jioni narudi home nokamkuta Mariam anapika, nikamuuliza habari za rafiki yake Mariana akasema ameenda na ameonana naye ananisalimia...(nilikuwa na hasira muda huo asikwambie mtu, lakini sikutaka kumwonyesha kuwa nina hasira, though chakula sikuweza kula.

Baada ya siku mbili,niliamua kumtafuta jamaa bila Mariam kujua, nikaongea naye meeengi na hatimaye tukaamua kila mmoja ambwage Mariam (akili za shule shule bhana...)

Niliporudi home nikamuuliza Mariam ana wapenzi wangapi, like swali lilizua tafrani za hatari, alilia Mariam asikwambie mtu, akanituhumu kuwa namuonea kwa kutokumwamini ilhali yeye amejitoa kwa moyo wote kufanya maisha na mimi, hapo nilijifunza kitu kikubwa sana kwake.

Wakati wote akinishambulia kwa maneno makali nilikuwa na hasira mno,nilijizuia kwa kiwango cha juu kumpiga hata Kofi moja kwani nilijua kufanya hivyo kungepelekea madhara mengine makubwa zaidi, nilimwambia najua kila kitu kuhusu yeye na jamaa, nikamtajia lodge waliyokwenda na chumba walichoingia nikamtumia na picha za siku ya tukio, hapo ndiyo akaanza kuniomba radhi, SIKUWEZA KUMSAMEHE, nilimuacha, alinitafuta sana baada ya miaka 2 kupita sikutaka tena kumrudia.

ITAENDELEA....

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
Nakaa siti ya mbele kusubiri ujio wa ferooze
 
Inategemea NTU na NTU na hili la dunia ya sasa Mkuu umeexaggerate mapenzi bado yapo yapo sana tu katika nchi nyingi duniani.
Kwa dunia ya sasa Ndoa au mapenzi ni overrated,tuna sexual desire tu.Cha msingi una amani na furaha pia unatimiza ndoto zako na kuweka akiba ya uzeeni.
 
Back
Top Bottom