The reason to why I didn't marry you!

The reason to why I didn't marry you!

INAENDELEA...
Tumeishia kwenye mahusiano na JF member mwenzetu, (no.7) ila sijamtaja jina ili kulinda heshma yake...

8. JF MEMBER 02.
Huyu pia naomba nisimtaje jina,katika kujadilijadili mambo ya JF moyo wangu ukiwa mfu kabisa kwenye mambo ya mahusiano,tulikuwa tukijadili a b c,za maisha na member mmoja (tukiwa mikoa tofauti) baadaye akaniambia ana safari ya Dar nikamkaribisha, nikamuuliza kama ana mahali pa kufikia akasema nimuandalie tu,nikatafuta hotel, tukakubaliana kwenda kucheck tulipocheck wote tukiwa salama tukajiachia kwa usiku kucha, akanisimulia mengi aliyopitia nikamhurumia sana lakini nikamwambia mimi sina mpango wa ndoa kwa wakati huo akasema pia si kitu anachokiwazia hata chembe, basi tukawa tunakutana tunamaliza haja za miili yetu kila mmoja anaendelea na maisha yake, baada ya miezi kadhaa nikashangaa sana, kumbe mdada alikuwa mke wa mtu na mumewe alikuwa anafanya kazi CRDB-BANK moja ya mikoa ya nchi yetu, nikashangaa zaidi imekuwaje????

Huyu sikumtafuta tena baada ya kujua ni mke wa mtu, (iliniumiza sana kihisia hii) kwa sababu sikuwahi kufikiria ku-date mke wa mtu maisha yangu yote! Japo aliniandikia sana kutaka tuendelee kwa madai kwamba yeye na mumewe walikuwa wamesha achana but I never looked back tukaishia hapo (najua lazima atasoma huu Uzi, ajue tu aliniachia maumivu makali mno)

Baada ya hapo sijapata tena kuanzisha mahusiano yenye malengo, najikuta nipo tu, hisia za kujenga mahusiano serious sina tena, I'm dating nimejifunza kutumia condoms japo sizipendi sana!

Japo kuna wakati nafikiria nifanye maamuzi serious nioe tu lakini ule moyo wa kuamua umekuwa mgumu...

Na ukweli hao 7 nilikuwa na malengo ya kuoa kabisaaa, ila baada ya hayo na kukata tamaa nadhani kuna wengine kama 13 ambao nime-date nao bila kuwa na malengo yoyote, we date thereafter kila mtu anaendelea na maisha yake, hii Hali siipendi sana pia as nakosa ujasiri wa kuingia ibadani kumuabudu Mungu nikijitazama kwenye hiyo angle, niombeeni sana nitoke kwenye huu mfumo wa maisha ndugu zangu...

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
Nasubiri no 2 wa jf atajwe me nikuombe umtaje tu na jina tunogeshe story..... ila hii list sitamani kukosaa kbsaaa
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
I can simply conclude kwamba ulikua hujui unachotafuta kwenye mahusiano na ni mtu unaefanya maamuzi kwa kukurupuka
Maamuzi anafanya kwa kukurupuka?..Evidences zote anazo ila still unasema kakurupuka...Madam HR..hapa umeyumba kidogo kwa mtazamo wangu.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
1614894061686.jpeg

Tunashukuru hujataja majina ubarikiwe sanaa
 
INAENDELEA...
Baada ya Kuamua kuachana na Mariam wa UDSM...

4. Veronica
Huyu alikuwa anasoma MZUMBE university, alikuwa mpole sana, lakini pia tulikuwa tunatokea kijiji kimoja, tulishibana kiasi fulani, lakini tayari nilikuwa sina imani sana na wanawake (hasa nikikumbuka nilichokiona kwa Mariam)
Tuli-date vizuri sana, mawazo yangu yalikuwa kujiridhisha then nimuoe!

Baada ya muda wa kama miezi 7 ya mahusiano alipata kazi mkoani Rukwa Kalambo) matumaini yakaanza kupungua japo alisisitiza sana kuwa hawezi kuivunja ahadi yetu, nilimsindikiza akaenda kuanza kazi, miezi mitatu baadaye alirudi jijini, tukatafuta hotel maeneo ya Tabata segerea, tukapata wasaa wa kukumbushia mipango yetu lakini wakati huo huo alikuwa "very careful" na simu yake, basi ilipofika majira ya saa 3 usiku nikamwandikia msg jamaa yangu mmoja kuwa anipigie simu, tuzungumze very serious issue, then jamaa aliponipigia katikati ya mazungumzo nikaizima simu, lengo ni mimi kuchukua simu yake (wakati huo nilikuwa nimeshameza password zake bila yeye kujua)

Baada ya ku-act simu kuzima charge nikatumia simu yake kuongea na jamaa, baada ya muda mfupi nikamwambia jamaa namtumia pesa,(nikatoka na simu yake) nikijifanya nakwenda Tigopesa,nilipotoka nikazama inbox, nakuta text za HR wao anamuuliza kama ameshathibitisha kama yupo pregnant,na bibie akawa anamwambia amethibitisha ndiyo, jamaa ana-demand atoe, wakati bibie hataki kutoa na akawa ametia msimamo kwamba kama jamaa hataki mtoto basi yeye atajua Cha kufanya ila asije akamsumbua kudai mtoto wake baadaye...(niliishiwa pozi kujua kwamba sio tu ame-cheat, ila amesha-conceive yaani...)

Nikamyuti,nilichofanya ni ku-screen short na kuzi-forward kwangu zile texts, then nikanyamaza zangu kimya, nililazimika kutoonyesha hata dalili ya kujua chochote!

Ilipofika asubuhi tuliagana, baada ya siku mbili nilimsindikiza ubungo asubuhi sana, alikuwa akilia kwa hisia sana kwa madai kwamba anaumia kwenda kukaa mbali namimi, moyoni nikijiuliza hisia zinatoka wapi huyu ilhali anajua ukweli ulivyo?

Mwezi mmoja baadaye akaniambia anahisi ni mjamzito, aikumjibu kwanza, baada ya siku mbili akaanza kunishambulia kuwa kwa kuwa amesema habari za ujauzito basi nimeanza kumchunia...nikamuuliza kama ana uhakika kuwa mimba aliyo nayo ni ya kwangu, kwa msisitizo akasema hana hata chembe ya shaka, nikamfowadia zile charts, akaniomba sana tukae tuzungumze kwani vinginevyo angejiua, sikuwahi kukubali kukaa naye kwa mazungumzo yoyote, nilisikia tu kwamba kutokana yaliyojiri pale kalambo basi alipewa uhamisho, akahamia MWANZA, baada ya kujifungua akaniomba sana turudiane kwa dhana kwamba alipitiwa tu na shetani,nilikataa ikawa end of the story!


Ukweli ni kwamba baada ya hapo hisia za kupenda zilikufa nikajikuta nikiingia kwenye mahusiano nakuwa nipo tu, sijali tena kama zamani Wala nikawa sifikirii sana habari za kuoa!

5. ROSE
Huyu alikuwa mpole afu hata kufanya naye mahusiano sikutaka ila nilimtamani, niligusa for just a day sikurudi tena, akaniambia amenasa mimba yangu, nikamwambia zaa tu ila sina mpango wa kuoa, akalia sana Rose na kuhama kabisa mkoa, (sikujali kihivyo) mtoto alipozaliwa ilikuwa copyright na mimi...nikaanza kutoa matumizi,(Rose alinitaka tuishi wote baada ya kujifungua, nikakataa) ndo ikawa basi tena, mpaka leo tunalea mtoto tu...

6. MARY
Alikuwa na asili ya Kondoa, mzuri wa sura,rangi na umbo , nikajiweka mzima mzima,nikiwa committed kuwa namuoa,(kumbe kwao alikuwa ameacha watoto wawili, mimi aliniambia ana mmoja) tukafanya mambo lukuki kwa pamoja, nilijikuta haiwezi kupita siku sijaenda kwake, hata ningekuwa busy kiasi gani ila lazima nitakwenda kwake hata usiku wa manane!

Mary alisafiri akaniachia funguo, lakini ilikuwa lazima niende kwake nikae kae pale ndani then najisikia vizuri narudi kwangu, siku moja nikiwa nimejilaza kitandani kwake nilipigwa mwanga mkali sana machoni (ile hali sijui ilikuwaje na sijawahi kuielewa), baada ya pale nilinyanyuka mpaka kwenye mikoba yake mingi aliyoining'iniza kwenye hang'er, nilichomoa mkoba mmoja na kufungua ndani, nilikutana na dawa za kienyeji na manuwio kibao yakilenga kunifanya boya, kila kitu atakachotaka basi nifanye tu, nilipata mshtuko mkubwa kwani manuwio mengine yalikuwa hatari na yenye mlengo wa kuua kabisa! Kilichonishangaza zaidi ni pale nipotoa vitu vyote nje na kuviwasha Moto, alinipigia simu akaniambia anajua nilichokifanya ila anaomba sana nimsubiri arudi tuongee...

Akili yangu ilikuwa imeshaamua kuachana naye, lakini moyo wangu ulishindwa kabisa, nikamsubiri arudi akaja akaniomba msamaha kwa kulia sanaa, tofauti na wengine kwa Mary nilijikuta nalegeza kamba nakumsamehe huku akili yangu ikikataa kabisa kumsamehe....

Baada ya siku kadhaa akaja jamaa nyumbani kwa Mary akitaka kuchukua fridge kama fidia ya deni alilokuwa anamdai(380,000/=) nilijikuta automatically nahesabu pesa kumlipia, baada ya kulipa akaniita chumbani akaanza kulia na kunishukuru sana kwa kulipa deni, akanikumbatia na kuanza romance, I couldn't resist, tukaishia kufanya mapenzi, baada ya mwezi mmoja akaniambia yupo pregnant, wakati wote huo akili ya kumuacha ipo pale pale ila moyo ukafeli kabisa...

Nikajisemea moyoni ili kufanikiwa kumuacha nalazimika kuanzisha mahusiano mengine...(which started costing me mpaka leo)

Niliamua kuhama eneo nililokuwa naishi, nikawa busy sana na kazi na ku-interact sana na social media...kupitia hiyo nikakutana na mtu mwingine member wa jukwaa hili hili...(kwa heshima yake naomba nisimtaje jina kabisa)
Tulikutana kwenye moja ya mada zikiwa moto sana hapa jukwaani, tukaenda zetu PM kuendeleza mazungumzo yetu...

Baada ya muda fulani tukapanga kuonana, alikuwa Dodoma kikazi (moja ya wilaya za Dodoma) nilimfuata tukaongea mengi na kuanza rasmi mahusiano,(kumbuka wakati huo natafuta kumuacha Mary kwa nguvu zote,akili imemuacha ila moyo hautaki na tayari alikuwa mjamzito)

Nikawa nimetumia zaidi akili kuanzisha mahusiano mapya, ndani ya miezi mitatu tu ya mahusiano mapya huyu JF member akaniambia AMENASA...(Frankly speaking nilikuwa siwezi kabisa kufanya mapenzi kwa kutumia condoms, ilikuwa tukianza mahusiano nakimbilia kucheck afya kwa kupima,baada ya kupata uhakika wa afya habari za condom nakuwa sina habari nazo kabisa...

Baada ya huyu mtoto wa watu kuniambia anahisi ana mimba, tukakaa kujadili tufanye nini, option ikawa twende kwao tusawazishe mambo kwa maana ya kulipa mahari na mengineyo, tukiwa kwenye makubaliano hayo akili yangu ilikuwa willing kabisa ila moyo ukawa hautaki kabisa, afu wakati wotenikawa namfikiria Mary tu, kwa hali hiyo concentration kwa huyu tuliyekutana JF ikawa inapungua japo mambo mengine yote tunafanya, (maandalizi ya kwenda kulipa mahari)

Ilipofika January 2018, tulitia timu malangoni kwa huyu mtoto wa watu tukalipa mahari,kikapikwa chakula cha kutosha nikapokelewa, baada ya mahari nikaondoka!

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
Hapo kweny hr nmchk xn
 
Dogo hana ajira, ameamua akumbushie ya kishule shule!

AKITUMWA DUKANI, ANA BANA BANA CHENJI ILI AWEKE BANDO AJE TENA......!

haya uwanja ni wako!


Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
Hahahaaa, "dogo hana ajira" hizi mentality za ajabu sana, aisee have been working for some years now, na biashara pia nafanya...karibu sana kwa juice na biscuits

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
Kwanini akili za kitoto mkuu, hao wote ilikuwa kwa nyakati tofauti tofauti...so nilikuwa na right dream kabisaaa

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app

Right dreams ni ndoto nyevu tu, labda zile za kwenye filamu... yaani demu wa kwanza kutafuna tu uliamini utaoa!!

Ikafeli, ukaenda wa pili kwa gia ile ile ya kuoa... hukujua kwanini kuna 'mazoezi' kabla ya pambano?
 
Right dreams ni ndoto nyevu tu, labda zile za kwenye filamu... yaani demu wa kwanza kutafuna tu uliamini utaoa!!

Ikafeli, ukaenda wa pili kwa gia ile ile ya kuoa... hukujua kwanini kuna 'mazoezi' kabla ya pambano?
Aiseee hiyo dhana ya kuchezea watoto wa watu sikuwa nayo kabisaa,nilikuwa najisikia vibaya kumbe wao ndo walikuwa wananichezea mimi yaani

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
Aiseee hiyo dhana ya kuchezea watoto wa watu sikuwa nayo kabisaa,nilikuwa najisikia vibaya kumbe wao ndo walikuwa wananichezea mimi yaani

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app

Mimi hadi leo bado najifua, na sijioni kama nimeiva kuingia ulingoni.... silaumu ila nimechezewa sana na mademu kisha wao wakaolewa kwingine.
 
Back
Top Bottom