mawaziri wote waliokuwao kwenye utawala wa Benjamini mkapa wanahusika na ufisadi njia moja au nyengine.
JK atakuwa bado hana serikali mpaka pale atapowauzulisha wote waliotoka enzi zile. ikiwezekana na ubunge pia
Si kama kawaida ya waandishi wetu wa habari na slogan yao "jina tunalo lakini tunalihifadhi"
Cha ajabu ni kuwa kwenye gazeti la majira wamemtaja Mwakyembe hajalipa bill ya maji...angalia hawa ma hypocrites
Na yeye JK vipi hakuwa waziri serikali ya mkapa?
Lowassa, Chenge, Karamagi, Msabaha achieni hata ubunge
Nkwazi Nkuzi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
BAADA ya 'nguvu ya umma' kuviangusha vigogo ambavyo havikutarajiwa kwa kasi ya ajabu na namna ya pekee, ni wakati muafaka kuwapa shime wananchi kushikilia uzi ule ule.
Haikuwa kazi nyepesi wala jambo lililotarajiwa kufanyika kama ilivyotokea. Lakini si hadithi wala dua la kuku, vigogo vimepukutika kama kupe kwenye mgongo wa ng'ombe.
Nani alidhani vigogo kama Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani; mawaziri, Nazir Karamagi, Ibrahim Msabaha, Andrew Chenge, Basil Mramba, Zakia Meghji, Kingunge Ngombale-Mwiru na wengine wangeporomoka bila hata kufurukuta kama ilivyotokea?
Sasa imetokea na nguvu ya umma imebainisha makali na jeuri yake.
Tusibweteke na mafanikio haya kidogo tuliyopata dhidi ya ufisadi na mafisadi. Lazima tuzidi kuhoji na kushinikiza ili nchi yetu iwe safi na vikwazo vya maendeleo na utu wetu viangushwe.
Baada ya kuwatimua wahusika kwenye ofisi nono na kubwa, kuna haja ya kuwafuata hata huko kwenye ofisi za umma wanazoendelea kuzishikilia. Tusiwe na simile wala nini bali kufanya kazi moja tu-kuisafisha Tanzania.
Huwa siachi kujiuliza mantiki ya kumfurusha mtu uwaziri tukambakizia ubunge. Kufanya hivi ni kuendelea kufuga ndwele na kutoa nafasi kwa wahusika kurejea tena kutuguguna kwa kasi ya ajabu.
Tusimwachie Rais jukumu hili. Maana Rais hana anachokosa kuanzia usingizi hadi maslahi yake. Tunaoumia ni sisi tunaowagharimia wakwasi hawa wasio na udhu wala lengo la kututumikia bali kututumia.
Hapa ndipo hitaji la kuwataka wahusika waachie na ubunge wetu linapokuja.
Ubunge ni uwakilishi wa umma sawa na uwaziri. Ofisi ya waziri na nafasi ya ubunge ni mali ya umma. Sasa anafukuzwa uwaziri anabakiziwa ubunge kwa lipi na kubakia kwa lipi?
Kwangu ubunge ndiyo mama wa vyote. Hivyo kuna haja ya kuangalia namna ya kuwawajibisha watu hawa ambao wamebainika kwenda kinyume na sheria na taratibu za utumishi katika nchi yetu.Kuna haja ya kujiuliza. Kama mtu ameweza kuiibia taasisi yenye wataalamu lukuki, inakuwaje inapokuja kwa wananchi maskini wengi wa vijijini wanakotokea hawa wabunge?
Nafahamu. Chama Cha Mapinduzi kimekuwa mstari wa mbele kuwatetea na kuwalinda wahalifu hawa wa kisiasa. Lakini ikubalike. Nchi hii si ya CCM wala Rais. Ni mali na nchi ya watanzania.
Ingawa kuna sheria chafu zilizotungwa na kupitishwa na watu hawa zinazowalinda watu wabovu kama hawa, bado wananchi wakijua uzito wa nguvu yao wanaweza kuwangoa licha ya kuwapo sheria chafu zinazowalinda.
Tusiogope mamlaka ya Rais na dhamana ya CCM kama vinatumika vibaya.
Rais yupo kwa ajili ya wananchi lakini wananchi hawapo kwa ajili yake. Yeye ni mtumishi wao. Si ndivyo alivyotwambia wakati akituomba tumchague? Sasa inakuwaje anapoingia madarakani awe mtumikishaji badala ya mtumishi?
Nani anataka kumwajiri mtumishi mwenye kiburi na mamlaka kupita yake muajiri?Hapa ndipo Rais anapopaswa kuwa makini.
Kama umma utajua haki na wajibu wake na jinsi ya kuvitumia vitu hivi hatakuwa na lake. Na hii ndiyo silaha iliyowakomboa wenzetu kwenye nchi tunazoziita zimeendelea.
Kitu muhimu ni kuelewa kuwa nguvu ya umma huwa haiji kwa kubembeleza au kupewa na watawala bali hujitokeza na kuziba ombwe.
Mapinduzi tunayopigia mifano kama yale ya Urusi (1903-05 na kuendelea) na yale ya wafanyakazi wa Ufaransa (1789-1799) hata ya hivi karibuni ya Poland (Septemba 1980) na ya Romania (Desemba 1989) hayakushushwa kutoka mbinguni.
Yalisababishwa na dhuluma ya watawala kwa watawaliwa. Yalianzishwa na kuchochewa na ufisadi na kiburi cha watawala waliowaona watawaliwa kama vyombo vyao vya kuneemekea na kutanulia kama ilivyo kwetu.
Mapinduzi haya yalikiuka imani na itikadi za kisiasa na kidini kiasi cha kujichimbia kwenye ukombozi wa kweli kiuchumi. Hakuna anayekula itikadi ya dini wala chama chake bali mkate. Je, bila kuwa na haki mkate ambao ni keki ya taifa utaipata wapi?
Hii ndiyo siri ya heshima na ustawi wa nchi tajwa, hasa mwananchi wa kawaida mitaani-msukuma mkokoteni, omba omba wa kutengenezwa, mwanafunzi, mjamzito maskini asiye na pa kwenda kutibiwa.
Chuki dhidi ya wale waliokuwa wakiishi maisha ya uhakika na wale waliokuwa wakiishi bora liende ndicho chanzo na chachu ya wenzetu kufanya mapinduzi hasa kuanzia kwenye fikra na malengo yao kama jamii.
Leo Watanzania wamegeuzwa kunguru kula vya kudandia na kudokoa! Haya si maisha ni kiama.
Si maisha anayostahili kuishi mtanzania juu ya nchi yenye kila neema na utajiri.
Kuendelea kujiweka utumwani kwa watawala ni ukondoo na ukuku.
Haya si majaliwa ya binadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu mwenyewe. Haya siyo majaliwa wala maisha yanayomfaa Mtanzania.
Kwa nini kwa mfano Watanzania tuishie kuwa makapuku huku hata wakimbizi wa kiuchumi kutoka India na China wakiishi vizuri miongoni mwetu?Sina haja ya kuleta ubaguzi wala hisia zake.
Ndiyo ukweli tunaopambana nao kila siku mitaani. Rejea Wahindi kuwa karibu katika kila kashfa ya wizi wa mabilioni yetu walipa kodi.
Rejea kuanza kuongezeka kwa idadi ya wabunge wafanyabiashara wa Kihindi ili kulinda maslahi yao ambayo kimsingi yanaua maslahi yetu.
Hapa ndipo ilipo siri ya akina Jeetu Patel kutuibia. Wanatumiwa na watawala kwa kujua fika mambo yatakapoharibika watawatorosha. Rejea kwa mfano kuwa vigumu kuwatorosha akina Maregesi na Lukaza. Hawa wangekuwa Wahindi kisingepatikana kitu.
Tukirejea kwa walengwa wa makala hii, ni wakati muafaka kuwatendea na kujitendea haki kwa kuwataka waachie ubunge kama taasisi ya umma.
Wakikataa tuandamane kuwazuia wasiingie kwenye Bunge letu. Maana watalitia najisi kutokana na kuendekeza ulafi na maslahi yao binafsi kinyume na yale ya umma.
Vita hii ni do or die au kufa na kupona. Kuondokana na watu kama hawa kwenye taasisi hakutupi hasara bali kurejesha haki zetu za kuishi kama watu.
Si chuki wala chuiu.Watawala wabovu wamekuwa chanzo kikuu cha umaskini wetu kuliko hata majanga ya kimaumbile kama vile ukame.
Hebu rejea kitendo kichafu cha Rais wa zamani na walafi wenzake kuleta, kwa mfano, kampuni ya Kikaburu kuja kuua TANESCO lililosababisha kupandishiwa umeme.
Rejea hata hili sakata la Richmond ambapo tunalazimika kulanguliwa umeme kuwalipa matapeli wanaoshirikiana na baadhi ya watawala wetu.
Hatuwezi kama nchi kuendelea na jinai hii na tukajidanganya kutakuwa na maisha bora kwa Mtanzania.
Sasa ni miaka mitatu tangu tuambiwe maisha bora kwa Mtanzania. Nini kimefanyika zaidi ya kuishia kuwa usanii wa kisiasa?
Kuna haja ya kuanza hata kupambana na rais wetu kwa kumbana atimize tuliyokubaliana na kama atashindwa hata mwaka 2010 asiruhusiwe hata katika chama chake kugombea tena kiti cha urais maana amefeli vibaya sana.
Tuhitimishe.
Wakati sasa umefika kuwataka kiutu mzima watajwa na wengine wanaofanana nao kujitoa haraka kabla ya umma kuwachukulia hatua ambazo matokeo yake hayatakuwa mazuri kwao.
Hapa ni kuwaomba wabunge wenye uchungu na nchi kutokubali kuburuzwa na chama kilichokwisha onyesha wazi kuishiwa na kupoteza mwelekeo.
Mungu ibariki Tanzania.
mpayukaji@yahoo.com
Mwenye Kutaka Kuwatoa Ubunge Watu Hawa Ni Wananchi Walio Wachagua Kwa Kura Nyingi Sio Mwingine Wowote Yule
Hata Hivyo Hii Nchi Sio Ya Democrasia Huru Kwahiyo Vitu Hivyo Ni Bado Sana Kuwa Kama Sheria Kwa Sababu Hata Wananchi Wenyewe Hawajui Haki Zao
..wananchi wa Bariadi,Kibaha,Bukoba Vijijini, ndiyo wenye haki ya kuwavua Ubunge kina Chenge,Msabaha,na Karamagi.
..wananchi kumkataa mbunge wao siyo jambo la ajabu Tanzania. miaka ya 1980 wananchi wa same walimshitaki mbunge wao Chediel Mgonja kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa wakati wa uchaguzi.
..asiyewataka Karamagi,Chenge,na Msabaha, aandae hoja ya kikatiba kwa kushirikiana na wananchi wa Bukoba,Bariadi, na Kibaha, na aipeleke mahakamani kwamba hao wamepoteza sifa za kuwa wabunge.
..asiyewataka Karamagi,Chenge,na Msabaha, aandae hoja ya kikatiba kwa kushirikiana na wananchi wa Bukoba,Bariadi, na Kibaha, na aipeleke mahakamani kwamba hao wamepoteza sifa za kuwa wabunge.
Warioba ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu amaeshatamka kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuandika katiba mpya na kipengele ambacho ni lazima kiwekwe ni kile kinachosema kwamba ukijiuzulu au kufukuzwa uwaziri moja kwa moja unapoteza na ubunge wako.
Mr. Andrew Chenge, who resigned from government last week, is a former Attorney General and had been promoted to cabinet to head the ministry for infrastructure development. The multi-million pound sterling scandal is under both local and international scrutiny. Chenge was Tanzanias Attorney General when the radar deal was sealed. East African Business Week has learnt that at the time the deal was negotiated, Tanzania had no money so it had to look for other sources to finance the project.
Reliable sources say the Tanzania government sought a legal opinion about the deal at which point the Attorney General office advised to continue with the project and above all advised the government to borrow money from a British bank, Barclays. According to a source within the ministry of legal and constitutional affairs, that legal opinion was by itself illegal because such a commercial debt was uncalled for as the World Bank and the International Civil Aviation Organisation had said the purchase was unnecessary and overpriced.
He said the Attorney Generals Chambers advised the government to borrow a huge amount of money well knowing that the price was on the higher side. Apart from an inflated price, Tanzania being a HIPC country was not supposed to enter such a debt burden with a two-digit interest rate, he said. The Serious Fraud Office (SFO) has shown concern after discovering that such a legal opinion was itself illegal, and could have been pushed by personal interests because the deal was wildly expensive, he said.
Although reports that Chenge is under investigations came out recently, East African Business Week has established that the SFO started a follow up on the matter three years ago. The radar was manufactured by Siemens Plessey, which then had become a BAE subsidiary. The local Siemens agent then negotiated the sale with the Tanzanian defence ministry. The radar deal has a long history. It all started in 1992 during President Ali Hassan Mwinyi when negotiators had put the price tag at 11o million pound sterling.
The deal was blocked on reasons that it was unaffordable and the first Tanzanian President, Julius Nyerere played a great role in discouraging it. However, when Nyerere died in 1999, the scheme was resurrected, with a smaller phase to be followed by the rest but both the World Bank and the International Civil Aviation Organisation were against the deal. In the UK, the then Development Secretary, Ms. Clare Short, temporarily blocked aid payments in protest and said openly that she suspected corruption.
It stank and was always obvious that this useless project was corrupt, she was quoted as saying. Short also made an attempt to prevent the sale by arguing that a British arms export license be withheld but was overruled in cabinet by the then Prime Minister Tony Blair. Britains Foreign Secretary then, Mr. Robin Cook and current prime minister Gordon Brown were also against the deal. The reasons put forward by both Short and Cook were that because Tanzania is one of the poorest countries in the world, there were no substantive reasons to enter into such an expensive deal.
Chenge, resigned on April 20, 2008 after the Guardian newspaper of the UK said the minister has stashed away $1 million in an offshore account and that the team investigating the sale of the military radar to Tanzania was tracing the account. Also discovered, was a $ 500,000 transaction shown to have been made (from Chenges offshore account) to one of the senior officers of the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco). Two weeks ago SFO conducted an in-depth search at both Chenges offices and residence in Dar es Salaam.
Chenge is now the fourth minister to resign in a period of two months. Edward Lowassa (Prime Minister), Nazir Karamagi (Minister for Minerals and Energy) and Ibrahim Msabaha (EastAfrican Cooperation) resigned in February after they were implicated in the irregular awarding of a multi-billion shilling tender to generate emergency electricity in 2006. The tender was awarded to a shadowy American company, Richmond.