Halafu unaambiwa hilo ni deal moja tu! bado kuna deal kibao ambazo hatujazifahamu! kweli wajinga ndio waliwao! hapo bado hujajua madeal ya Mramba,Mkapa,Sumaye,Karamagi,Rostam Aziz,Lowasa na wengineo!..ndiyo maana hawa watu huwa wanakiburi sana kumbe ni kwa sababu ya mimali waliyojilimbikizia.
Halafu na Rais Kikwete bado hajui ni kwanini nchi yetu ni masikini?
-Wembe
Kama Tanzania ni nchi inayoomba omba mpaka Rais wetu kila Siku yuko kwenye Nchi za watu anaemea inakuwaje kumbe tu matajiri mpaka Milioni za dola ya USA tunayaita vijisenti?
Chenge anataka kutwambia nini hapa? Kumbe ndo alivyo na kiburi
Jamani msing'oane meno bure. Habari mpya nilizozipata hapa ni kwamba kumbe hizo hela za Chenge ni dola za Zimbabwe. Du, tuendeleeni na mijadala mingine tuachane na hivi vijisenti vya chenge.
Huuu....!!
Bila wahalifu police watakosa kazi!!...Bila kesi mahakimu Watakosa kazi...
Bila mafisadi!!!?............sijui
Nafikiri tuanze kutathimini haya mambo kwa logic!!Tusi jiachie sana!! kama kiongozi ana iba basi hata mimi mfuasi nitafanya hivyo!!
viongozi wangu!!
Im sorry
Shilingi bilioni moja na laki mbili kwa fisadi Chenge ni vijisenti sasa sijui hao waliopata mshiko mnono akina fisadi Mkapa, Mramba na wengineo wana balance kiasi gani katika bank accounts zao za nje.
Itabidi bajeti ya mwaka huu hayo mapesa Chenge aliyoyaiba yaingizwe kwenye bajeti kwa vile wafadhili wanaelekea kugoma kucontribute
Hahahahh Chenge, Lowassa alisema tukiamua kufatilia hakuna mwanasiasa atakayepona na aliye msafi....Chenge amepitiwa na kimbunga, more are coming, RA, Mkapa, Yona, Mramba, Karamavi etc etc...
Hahahahh Chenge, Lowassa alisema tukiamua kufatilia hakuna mwanasiasa atakayepona na aliye msafi....Chenge amepitiwa na kimbunga, more are coming, RA, Mkapa, Yona, Mramba, Karamavi etc etc...
Kwa hakika huyu nadhani ni mtu mzito sana kuliko hata alivyokuwa gavana wa benki kuu!!!
Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa nchi kama kweli akijulikana bila shaka ametuibia... Then kama taifa tuna tatizo kubwa... maana kama ni ethics, kufuata sheria mwanasheria mkuu wa serikali ndiye angekuwa mtu wa kwanza kwa usafi immediate after head of the state... sasa kama yeye kweli atajulikana ametuibia... du kazi ipo...
Mwanakijiji,
Fafanua maana nimetoka kapa hapo.
Naona Wazungu wamekosea, hizo milioni ni shilingi sio pounds au dola
kwi kwi kwi!!!!!
Si ajabu Chenge alikuwa analundika tu, alisahau ni dola na akadhani ni pesa za madafu.
Vinginevyo, mwaka ujao tutaendelea kuwakalia kooni kama nira na kama ndege wanavyotua juu ya wanyama malishoni ndivyo na sisi tutavyotua katika migongo yenu. Tutawadonoa kwahoja na kuwaparua hadi makupe na viroboto yaishe kati yenu. Kama mwaka huu mmetushinda kwa kuwarudisha vijana wetu toka Ukraine kusoma na kuwaacha Solemba, na mkatangaza ushindi, basi mwaka ujao ni zamu yetu! Tunawatangazia mapema kuwa kama mlifikiri Tanzania ni yenu peke yenu na sisi wengine ni wakimbizi tu na wahamiaji mjue kuwa wakati wa njozi yenu hiyo umefikia kikomo!
Unapokuja mwaka mpya, hatutakubali tena kuzugwa kwani kuzuga kwa miaka 46 iliyopita kumetosha na wananchi wanajiandaa kwa mwaka 2010! Mmepewa nafasi nyingi ya kusahihisha na kujisahihisha na mara zote mmekuwa na majibu na mikakati ya kizugaji. Watanzania wamechoka, na wakati waja na tena upo ambapo wataonesha uchovu wao kwenye sanduku la kura. Safari ya kuelekea huko ndiyo imeanza. Mtatuzuga tena? I dont think so!
Mzee Mwanakijiji;176063 Nakulilia na Mtanzania; nilichozungumzia ukiondoa hii ni suala la RA (kuna makala mbili ziko Mwanahalisi)...[/QUOTE said:JF raha tupu maana magazeti yote yanakuja na habari ambazo tayari tumeshazipata hapa. JF always behind the news maker
Hawa walio leak data za Chenge ku-divert attention from Richmond na EPA wanadhani Mwanahalisi nalo halina data dhidi yao. Wamefungua Pandoras box, maana Chenge hataanguka mwenyewe hivi hivi, lazima afe na mtu. Sit back and enjoy the show.
Wakuu,
Hivi hawa watu ni akina nani?
Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere.
Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.
Hapa kuna ndoa za watu zitaota mchanga. Mtu unaweza kufikiri mama anajituma, anakuja na mlo safi, kumbe ni mafisadi yamekuingilia hata nyumbani kwako.