The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Halafu mwenzie kajivua ushirika. Yaani mwizi anaiba na wenzake wakishagawana mali ya wizi yeye anasema "siibi tena" lakini mali waliyogawana anaishikilia...
 
Halafu mwenzie kajivua ushirika. Yaani mwizi anaiba na wenzake wakishagawana mali ya wizi yeye anasema "siibi tena" lakini mali waliyogawana anaishikilia...

worthless.gif
 
hahaaaaaaaaa, haki ya nani bana sikutaka kuchangia hapa, lakini imebidi tu ! naona umevamia kila kona !

"Muache Mzee Wetu Apumzike"-JK
"Mie Nimestaafu"-BWM
 
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini
TAKUKURU imemtuhumu Bw Sailesh Vithalan kwa kuhusika
na tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada
iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania mwaka.

Aidha TAKUKURU imesema jalada la kesi ya mtuhumiwa
huyo tayari limekwishafunguliwa katika mahakama ya
hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam tokea Novemba mosi, 2007 (Siku ambayo THISDAY waliandika story yao).

Akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za
TAKUKURU jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa Idara ya
Elimu na Umma wa Taasisi hiyo Bi Mary Mosha amemtaka
muhusika huyo popote pale alipo kujitokeza mara moja
ili kujibu tuhuma hizo.

Amesema kuwa Mtuhumiwa huyo ni Raia wa Nchi mbili
ikiwemo Tanzania na Uingereza, TAKUKURU hadi sasa
hawajui alipo mtuhumiwa huyo ingawa tayari wamekwitoa
taarifa kwa polisi wa kimataifa (interpol) ili
kufanikisha kumtia mbaroni.

Ameongeza kuwa kupatikana kwa mtuhumiwa huyo pia
kutasaidia kuweza kupatikana kwa baadhi ya watu
wengine walioshiriki kwa namna moja ama nyingine
katika rushwa hiyo ya ununuzi wa Rada.

Takukuru imewaomba wananchi pamoja na waandishi wa
Habari kutoa ushirikianao katika mapambano dhidi ya
Rushwa.

Kashfa ya ununuzi wa rada hiyo iliyogharimu mabilioni
ya shilingi ilianza mwaka 1999 baada ya serikali ya
tanzania kuingia mkataba na kampuni ya BAE Syatems ya
Uingereza kwa manunuzi ya rada hiyo.

Aidha manunzui hayo yaliyodaiwa kughubikwa na tuhuma
za rushwa yalizua mijadala mikali nchini Tanzania na
Uingereza kuhusu umuhimu wa rada hiyo na gharama zake
kwa nchi.
---------
 
hapa ndipo wanapokosa kila siku,yaani hata kudanganya wanashindwa,sasa huyu wa nchi mbili sindio kazi kweli kama tumeshindwa kumkamata kishimba wa imalaseko itakuwa huyu baniani
 
hakuna raia wa nchi mbili hawa TAKUKURU hawajui sheria? Halafu tulizungumza tangu wiki iliyopita, ina maana hakuna surveillance katika Tanzania.. mbona alikuwa anatembea mitaani wiki iliyopita tu..?
 
hapa ndipo wanapokosa kila siku,yaani hata kudanganya wanashindwa,sasa huyu wa nchi mbili sindio kazi kweli kama tumeshindwa kumkamata kishimba wa imalaseko itakuwa huyu baniani

Well said, hawa mabaniani tayari wapo India au Canada na Jina Jingine, Kenya kuna Ufisadi kama huu, na jamaa anaye husika hajampata anaitwa Kamani na ana nduguze Uingereza.
Labda kama waiengereza walichukua alama zake za Vidole, na zaidi ya hapo tunajua hakuna dual citizenship Bongo sasa huyu ni VIpi?
 
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU imemtuhumu Bw Sailesh Vithalan kwa kuhusika
na tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada
iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania mwaka.

Binafsi nadhani huyu jamaa kama hana watu wa kumlinda itabidi ndiyo awe kafara!

Akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za TAKUKURU jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa Idara ya
Elimu na Umma wa Taasisi hiyo Bi Mary Mosha amemtaka
muhusika huyo popote pale alipo kujitokeza mara moja
ili kujibu tuhuma hizo-

Je ni nani mwenye akili timamu ambaye anaweza kujitokeza, katika skandali kama hii?

Amesema kuwa Mtuhumiwa huyo ni Raia wa Nchi mbili ikiwemo Tanzania na Uingereza, -

Je tanzania tulisharuhusu uraia wa nchi mbili?, kwani naona huyu mama amemuhalalishia huyo mtuhumiwa kuwa raia wa TZ pia UK

Ameongeza kuwa kupatikana kwa mtuhumiwa huyo pia kutasaidia kuweza kupatikana kwa baadhi ya watu
wengine walioshiriki kwa namna moja ama nyingine
katika rushwa hiyo ya ununuzi wa Rada--

Ufuatiliaji mzuri nadhani inabidi uanzie wizara ya fedha na jinsi jamaa alivyopewa hiyo tenda na siyo kinyume chake. Zabuni ya ununuzi wa Radar ilitolewa na nani na ushindani wake ulikuwaje?
 
hao sijui kularushwa narudia tena hakuna jipya,kwani ile sheria waliyopewa na ccm ya kufunga watu midomo sasa ndio inaanza kutumika rasmi.
 
Posted Date::11/5/2007
Mtuhumiwa kashfa ya rada afikishwa kizimbani Dar
Na Festo Polea

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (Takukuru), imekamilisha upelelezi wa tuhuma za rushwa kuhusina na utata wa ununuzi wa rada na mmoja wa watuhumiwa katika kashfa hiyo, Shailesh Pragji Vithlani, amefunguliwa mashitaka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar salaam, ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za taasisi hiyo, Mkurugunzi wa Idara ya Elimu kwa Umma wa Takukuru, Mary Mosha, alisema mshitakiwa huyo alibainika kushiriki katika mlolongo wa ununuzi wa rada kutokana na uchunguzi uliofanywa na taasisi hiyo.

Alisema taasisi hiyo imeshafungua kesi namba 1474/2007 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya mtuhumiwa huyo, itakayokuwa chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Sivangilwa Mwangesi.

Kwa sasa natangaza rasmi kuwa mshitakiwa popote alipo duniani anatafutwa kwa ajili ya kujibu mashitaka yanayomkabili na asipofanya hivyo tutamkamata kwa vile hati ya kumkamata imeshatolewa na mahakama? alisisitiza Mosha

Mosha alisema Mshitakiwa huyo anayetafutwa ana uraia wa Tanzania na Uingereza, hivyo wamewasiliana na Polisi wa Kimataifa (Interpol), ili popote alipo duniani aweze kukamatwa na kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo alipotakiwa kuwataja watuhumiwa wengine waliobainika kuhusika na ununuzi huo wa rada, alikataa kwa madai kuwa taasisi hiyo imeanza kumfungulia mashitaka mtuhumiwa mmoja kwa kufuata taratibu na sheria za Takukuru na kwamba baadaye wataendelea kuwashughulikia wengine.
 
Huyu mtu alikuwapo Tanzania, lakini kwa uzembe na urasimu wa hali ya juu wa vyombo vyetu vya dola wameng'aa macho mpaka ameingia mitini!!! Na sia jabu kutokana na waziti walioshiriki kucheza ile deal ya rada inawezekana kabisa huyu amesaidiwa na watu wa juu kabisa kuingia mitini. Mtu ana bulungutu la $12,000,000 na nyingine ambazo hatuzijui. Bongo inakatisha tamaa!!
 
Lifuatalo ni tamko toka TAKUKURU kwa waandishi wa habari kuhusu kufunguliwa mashtaka kwa Vithlani...
 

Attachments

  • JAMHURI1.JPG
    JAMHURI1.JPG
    35.8 KB · Views: 111
Hadi hapo watakapo balidilisha sheria kuhusu kesi za rushwa .. hii yote ni ndoto za alinacha. Huwezi kutumia law of evidence kum-prosecute mla rushwa! Ni hapo watakapo sema kuwa tuhuma na circumstances zikielekea kwenye rushwa hiyo ni tosha then tutakuwa tumepiga hatua amasivyo tusome magazeti!!
 
Kama alivyosema Mwanakijiji hiki ni kiini macho cha mwaka, tunafanywa wajinga hapa, huyu "mtanzania" mwenzetu ametumiwa kama leverage. Huyu Jamaa inafahamika kuwa for long time now is in his hide out in India, ambako hata interpol hawawezi kumtrace. Inawezekana kabisa kuwa hao wenzake alioshirikiana nao walimwambia akajifiche huko.
Uraia wa nchi mbili??? Yes ana uraia wa nchi mbili. Hii inawezekana kwa baadhi ya watu Tanzania kwa meleongo fulani, lakini sio kwa watu kama mimi na Maganga. THIS IS TANZANIA
 
Akina Mkapa wataanza kusema sasa hili suala liko mahakamani hatuwezi kulizungumzia. Kiini macho cha mwaka!
 
Time will tel. We shall wait and see the aftermath. The most important aspect here is for the MONEY to be returned back to TZ, otherwise ni usanii tuu.
 
African politics the real nightmare, i thought Tanzania constitution does not allow dual citizenship? Give me a brake, i expect one more charge to be added on his counts.

I thought investigators need to find all people that are bounded in the allegation, then turn to federal prosecutor. Things look vise-verse, they need Muhindi so he can name other suspects, what the hell is this? This is what we call Law loopholes, they know the guy will run loose. All this wining does not make any difference.
 
Hapa kinachofanyika ni kupunguza hasira za wananchi na ikipoa basi wataliacha sakata hili. Lakini ukweli uko na tabia moja kuna wakati unajidhihirisha wenyewe na cha kushukuru watanzania pia wameanza kuamka kwenye usingizi mzito na viongozi bado wanfikiria wananchi bado wamelala,Viongozi wanapaswa kusoma majira ya nyakati na kujitahidi kuacha mzaha katika masuala ya nchi yetu.
 
Wakuu mi nakubaliana na fact kuwa hiki ni kiini macho. Deal ilifanywa na kampuni (Merlin International) sasa iweje shareholder mmoja tu ndo ashitakiwe? Au kwa sababu mwingine kakwiba halafu kajitoa?Maana pesa silishatoka na ndio akajitoa?
Shareholders na Directors wote na kampuni hii wanastahili kushtakiwa.
Mtazamo wangu ni kuwa muhindi mmoja hawezi kuconclude deal kubwa kama hili bila kuwa na syndicate kubwa ndani ya serikali.
 
Back
Top Bottom