Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 1,211
- 233
Ni kina nani hao?Tukiwafahamu,tujiulize je waliopo madarakani sasa hawakuhusika?Na kama walihusika kwa njia moja au nyingine watajiepusha vipi na hilo au watajiingiza vipi katika saga hiloWakati hukumu yeyote itakayotolewa huenda ikawagusa?Wakukabwa koo na masikio ni hao waliokubali kulipa kodi yetu huko BAE...ohha nimekumbuka pengine hawakuwa na UTAALAMU wa kutosha.[/B]
Ama kweli haya yapo Tanzania peke yake. Wakati rais wa Jamhuri hii akiwaomba wananchi wamwache mzee wa watu APUMZIKE, huyu Mkapa anakuja na majivuno kuwa HABABAISHWI na mtu...
SFO head on bribery probe. The head of the Serious Fraud Office speaks about the decision to end a probe into alleged bribery involving BAE. Tazama video hapa:
http://news.bbc.co.uk/player/nol/newsid_6420000/newsid_6425500/6425537.stm?bw=nb&mp=wm
Katika sakata la kununua Rada Tanzania ilipewa mkopo wa US Dollar 40 milioni. Milioni $12 zimeingia mfukoni kwa mdosi mbongo ambaye inasemekana alikuwa kama wakala wa mkataba huo kati ya Tanzania na BAE. Mkopo wowote ule huwa ni lazima utozwe riba (interest). Swali langu ni kama hili lifuatalo, je Tanzania bado inalipa riba ya mkopo wote wa milioni $40 au milioni $28?
Katika sakata la kununua Rada Tanzania ilipewa mkopo wa US Dollar 40 milioni. Milioni $12 zimeingia mfukoni kwa mdosi mbongo ambaye inasemekana alikuwa kama wakala wa mkataba huo kati ya Tanzania na BAE. Mkopo wowote ule huwa ni lazima utozwe riba (interest). Swali langu ni kama hili lifuatalo, je Tanzania bado inalipa riba ya mkopo wote wa milioni $40 au milioni $28?
Afadhali umechukua muda kidogo Kumjibu kwa undani Lakini Yeye anafahamu walikopa ngapi na anafahamu wanahitajiwa kulipa riba Lakini ktk swali lake inaonesha anataka walipe million $28 tu na riba yake,Lakini wasilipe Mil$12 na riba yake.sasa sijui benki walihusika kuwaambia wampe dalali mil.12 na hawazihitaji wazirudishe na wala hawatazitolea riba.Mzee Bubu,
Heshima mbele mkuu, uliposema kuwa "...Tanzania tulipewa mkopo wa dola millioni 40...." ina maana kwamba tutaulipa mkopo mzima yaani dola millioni 40,
Hizo za mdosi ni tatizo letu kama Tanzania sio la waliotukopesha!
HATIMAYE Serikali imetoa kauli kwamba suala la ubadhirifu wa fedha unaodaiwa kufanywa wakati wa ununuzi wa rada, litajadiliwa na Bunge baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi kutoka serikali ya Uingereza.
Sambamba na hilo, serikali imesema kuwa, zaidi ya sh bilioni 17 ya mapato ya ziada, zimepatikana tangu rada hiyo inayolalamikiwa kunununuliwa kwa ulanguzi, ianze kutumika nchini.
Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk. Maua Daftari alitoa kauli hiyo bungeni jana, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kigoma Vijijini, Zitto Kabwe (CHADEMA), aliyetaka kujua endapo serikali ina mpango wa kuleta hoja ya rada ijadiliwe bungeni.
Akijibu swali hilo, naibu waziri huyo alisema kwa vile Serikali ya Uingereza bado inaendelea na uchunguzi wa kashfa hiyo, serikali kwa sasa haiwezi kuleta hoja hiyo bungeni.
Kuhusu mapato ya ziada yaliyopatikana tangu rada hiyo ianze kutumika, Dk. Maua alisema takwimu za mapato katika kipindi cha miaka miwili kabla ya rada na baada ya kununuliwa zinaonyesha zimeongezeka.
Alisema kabla ya rada hiyo kuanza kutumika, hasa katika shughuli za kuongoza ndege, mwaka 2000/2001, mapato yalikuwa sh bilioni 2.3 na mwaka 2001/2002, yalikuwa sh bilioni 2.8.
Alisema baada ya rada kununuliwa na kuanza kutumika, mwaka 2002/2003, mapato yalikuwa sh bilioni 3.4, mwaka 2003/2004 yalikuwa sh bilioni 3.9, mwaka 2004/2005, sh bilioni 4.1 na mwaka 2005/2006, yalikuwa sh bilioni sita na hivyo kufanya kiasi cha pesa kilichokwishapatikana kutokana na huduma ya rada, kufikia sh bilioni 17.5.
Rada hiyo ilinunuliwa kwa zaidi ya sh bilioni 40 na muuzaji kudaiwa kupata kamisheni ya sh bilioni 12, jambo ambalo Serikali ya Uingereza inafanya uchunguzi kubaini waliohusika katika ulanguzi huo.
"Kwa hiyo, kumekuwapo na ongezeko la mapato kwa asilimia 113.7 kutoka mwaka 2002 kabla ya rada haijaanza kutumika hadi mwaka 2006. Ni dhahiri kuwa ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa ndege zinazotumia anga na viwanja vyetu kwa jinsi huduma zilivyoboreshwa," alisema Dk. Maua.
Alisema kuwapo kwa rada, kumesaidia pia ongezeko hilo kwani wateja wamekuwa na uhakika wa usalama zaidi wa ndege na abiria wakati wanapitia kwenye anga na viwanja vya Tanzania.
Mbali ya kuongeza pato, Dk. Maua pia alisema wastani wa gharama za uendeshaji wa rada kwa mwaka ni sh milioni 234.7.
Alitaja gharama hizo kuwa na kiasi cha pesa kinachotumika kwenye mabano kuwa ni mishahara ya waongoza ndege na wahandisi (sh 145,597,121.30), mafunzo ya waongoza ndege na wahandisi (sh 50,000,000), matengenezo madogo madogo (sh 6,704,330,00), matumizi ya umeme (sh 28,002,443,00) na usafiri wa wafanyakazi na matumizi mengine, sh 4,419,147,00.
"Tangu rada hii inunuliwe, haijafanyiwa matengenezo makubwa. Hata hivyo, kulikuwa na utengenezaji wa Uninterruption Power Supply - UPS (ununuzi wa betri), mwaka 2006 na matengenezo ya Motor ya Antenna. Jumla ya gharama ya vipuri na matengenezo hayo ilikuwa sh 47,861,632," alisema.
Waziri Daftari alitoa ufafanuzi huo kutokana na swali la Msingi la Mbunge wa Ole, Bakari Shamis Faki (CUF), aliyetaka kujua mapato za ziada yaliyotokana na huduma ya rada, gharama za uendeshaji wa rada hiyo kwa mwaka na kwamba imefanyiwa matengenezo mara ngapi.
Mbali ya kutumika kuongoza ndege, rada pia husaidia kupunguza ucheleweshaji wa safari za ndege, huwezesha kuelekezwa kwa ndege ili kukwepa maeneo yenye hali mbaya ya hewa na husaidia marubani kuona uwanja wa kutua.