DrWho, nashukuru kwa majibu yako hata hivyo maswali yangu bado yanabakia:
- Kwanini Tanzania iliamua kununua rada hii ya matumizi ya kijeshi na kiraia?
Hili sina jibu ambalo ni conclusive lakini inawezekana kuwa ma consultants waliwaambia kuwa ni bora kwani tutakuwa tunaua ndege wawili kwa jiwe moja na itakuwa ni bargain nzuri tuu....vile vile usisahau kuwa inawezekana ikawa WU(Wizara ya Ulinzi) waliulizwa msimamo wao wa kushare lakin kwa jinsi ninavyowajua wanajeshi sidhani kama hili walikubaliana nalo nadhani unaelewa wanajeshi wanavyopenda kufanya mambo kivyao bila kucompromise kazi zao
- Ni tishio gani la anga ambalo lililazimisha serikali kung'ang'ania lazima iwe ni rada hii? Ni nchi gani iliyotupa tishio hilo na kwanini Watanzania hawakuambiwa kuwa tunatishiwa kijeshi!?
Yeah hili ni rahsi sana kwani tumezungukwa a maadui wa kila namna mfano MUSEVENI na pesa zake za mafuta kila kukicha ananunua militari kits toka CZECH REPUBLIC,CHINA,UKRAINE pamoja na ISRAEL sasa kwa hali ya kawaida sisi kama majirani tuna kila sababu ya kuwa attention kwani tuna historia ya kwenda vitani na hawa jamaa,the same applies to KENYA na hao magaidi ambao sasa hivi wanauwezo mkubwa sana tu wa kijeshi.
La kwa nini hatukuambiwa kuwa tunatishiwa kijeshi linatofautiana kwani kuna issue zingine za kiusalama wa Taifa ambazo hazihitaji kuwa katika PUBLIC DOMAIN unless necessary,pili nchi yetu hatuna culture ya kuwa transparent na issue kama hizi,tatu uzembe wa wabunge wetu kuuliza mambo haya bungeni sasa waliopo juu nao wanaona hakuna haja ya kudisclose mambo haya...nadhani mtiririko mzima unavyofanya kazi ndio wenye matatizo kwani naamini sheria ziko ambazo zinawapa wananchi right ya kujua haya lakini of course kuna namna ya kuget around them
- Ni kwanini rada hiyo imegharimu Dola milioni 40 wakati kuna mabenki na wafadhili wengine ambao walikuwa tayari kutusaidia kupata rada ya kiraia, ya kisasa na ambayo ingetupa usalama wa anga kwa bei ya robo ya hiyo?
Kwa sababu hiii ilikuwa ni BILATERAL agreement kati ya serikali yetu na serikali ya UK, na hiii ingetupunguzia mzigo mkubwa wakugo around kubeg kwa benki zingine ambazo zingetutoza interest rates kubwa zaidi ya Barclays,pili be very wary na hao wanaoitwa waWAFADHILI kwani huwa wanakuja na smal prints ambazo zinatumaliza zaidi kuliko initial deal.Vile vile sisi tunauhusiano mzuri na wasikunyingi wa kununua kits toka kwa waingereza sasa hili nalo nadhani walilitake into consideration lakini sisemi ni excuse ya sisi kupata bad side of of the deal (kama ni hivyo)
- Katika ununuzi unaomhusisha dalali, dalali hulipwa aidha na mnunuzi au na muuzaji. Hadi hivi sasa dalali amekiri kupokea malipo ya dola milioni 12 toka kwa muuzaji. Je mnunuzi (Tanzania) alimlipa dalali huyo malipo yoyote, kiasi gani, na nje ya hizo Dola milioni 40?
Hii sitegemei kama inaweza kutoka japo bwana Mwanakijiji IDEALISTICALLY uko right lakini REALISTICALLY uko wrong kwani hii ni business na siku zote kuna kitu kinaitwa confidentiality ambayo sheria zipo kuilinda hii hivyo usitegemee kama information hii ikawa disclosed kwani kuna watu wata SUE na COUNTER SUE na matokeo yake tutapoteza pesa nyingi kuliko ambazo tayari tumeshapoteza na hili la kulipa kamisheni kwa jamaa ni halali yao kwani ni sisi ndio tuliongia contract nao na tulijua kuwa we have to honor oursede of the deal
sasa kama hili ni kosa au la hilo si tatizo la dalali
- Je, kuna ofisa yeyote wa Tanzania ambaye amepokea malipo toka kwa dalali huyo nje ya nchi na maofisa waliohusika na ununuzi wako tayari serikali iwatake waidhinishe akaunti zao nje ya nchi zichunguzwe kujua pesa walizonazo humo zimetoka wapi?
Hili nilishakujibu katika post yangu hiyo hapo juu kuna hiyo BANKING CODE huwezi kupata kitu na kwa taarifa yako siku hizi si lazima ulipwe pesa inawezekana ikawa pesa ziko interms of STOCKS au PREMIUM BONDS sasa mabenki nao hawataki kuwa sued kwa sababu wamebreach CONFIDENTIALITY AGREEMENT kwa sababu y uzembe wa serikali
- Wakati wa ununuzi wa rada hii aliyekuwa Waziri waa Mambo ya nchi za nje alitetea kwa kusema kuwa tunahitaji rada hii kwani itatuongezea mapato na kuongeza utalii. Je tangu rada hii inunuliwe ni kiasi gani kimekusanywa kwa sababu ya rada hii (tukikusanya mapato toka nchi zinazopita katika anga letu). Je ni watalii kiasi gani ambao wameongezeka sababu ya matumizi ya rada hii?
HII NISHAIJIBU KATIKA POST YANGU YA AWALI HAPO JUU
- Lengo la rada hii tuliambiwa na Rais Mkapa ni kuongeza usalama wa anga. Je kabla ya kununuliwa kwa rada hii ni ajali ngapi zimetokea au nusura kutokea angani, na kununuliwa kwake kumepunguza ajali hizo kwa kiasi gani?
Details ainzaweza kupatikana toka idara ya Anga ambao nao ni part ya seriakali lakini usisahau kuwa viwanja vyetu vingi havina mitambo ya kisasa ya anga ,na evidence ziko za kuonyesha near miss incidents lakini sijui kama zilitokana na uzembe wa RUBANI wetu au RADA. vile vile nadhani unaelewa kuwa haya juzi tu tumempoteza naibu waziri(ofisa mkubwa serikalini) kwenye ajali ya ndege
- Rada hii tuliyoinunua ina uwezo wa kuangali theluthi moja tu ya nchi na hususan viwanja vya ndege vya Mwalimu Nyerere na kile cha KIA. Ili kuweka ulinzi na usalama kwa nchi nzima tunahitaji rada nyingine mbili zenye uwezo kama huo. Je tuko tayari kununua rada nyingine kwa gharama hiyo hiyo kila moja ili kutimiza lengo la kuilinda anga letu na kutupa usalama? Tuko tayari kutumia dola milioni 80 kufanya hivyo?
Capability ya rada hii iko QUESTIONABLE lakini vile vile usisahau kuwa suala hili linahitaji consultation toka idara mbali mbali za serikali na personally nadhani dola milioni 80 ni ndogo sana when it comes to national security lakini hii si semi kuwa nina ENDORSE rushwa na mabaya mengineyo AMBAYO INAWEZEKANA YALITOKEA
- Kuna uhusiano gani kati ya kununua ndege ya Rais kwa karibu kiasi hicho hicho cha rada na kumtumia dalali yule yule, dalali ambaye anafanya biashara ya silaha na serikali yetu kwa muda mrefu? Ni nani anampa dili hizo dalali huyo na mtu huyo ananufaishwa vipi?
Hii ni biashara na pale mjini wako jamaa wengi ambao nao wanadeals zao, sasa kama huyu mhindi anacontacts zake ambazo yeye anazitazama na anawatake care vizuri sidhani kama ni tatizo kwake kupata access...ni biashara na yeye ni mtafutaji hivyo siwezi kumlaumu kwa hilo
- Kama tumeweza kumfikisha mahakama Balozi kwa kughushi na kutumia vibaya nafasi yake na kununua nyumba ya ubalozi kwa bei ya chini wakati akitoa stakabadhi za kuonesha bei ya juu, ni kwanini hatufikiri kuwa kuna mtu katika serikali ambaye inawezekana kabisa amefanya jambo hilo kwenye rada? Mtu huyo ni nani?
Kumfikisha mtu mahakamani hakumaanishi kuwa kafanya kosa kwani sheria bado inamlinda as HE IS STILL INNOCENT UNTIL PROVED OTHERWISE BY THE COURT OF LAW....na huwezi kuwafikisha watu waserikali mahakamani kwa kuwa na hiyo CISRCUMSTANTIAL EVIDENCE...otherwise wanaweza kucounter sue na itaicost serikali zaidi sasa cha muhimu ni kuziba hiyo mianya ambayo inapelekea hali hiiikutokea
- Uchunguzi wa SFO ni kwa ajili ya serikali ya Uingereza. Uchunguzi huo hata kidogo hautuzuii sisi kuanzisha uchunguzi wetu wenyewe. Je serikali iko tayari kufungua uchunguzi huru? Je kuna chombo chochote kinachoweza kuanzisha uchunguzi bila ya kutaka ruhusa kwa Rais?
Hili nakubaliana na wewe na last time niliambiwa kuwa uchunguzi unafanyika na labda tu jamaa hawajaiweka katika public domain lakini uchunguzi tayari uko mbioni
Hayo ni maswali yangu na ya Watanzania wengine wengi.